NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Friday, January 21, 2011

TAMKO LA JANA KUTOKA UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM); NA MENGINEYO

 • Tamko hili la UVCCM "limewasha moto" kwani lina maneno makali (hasa kwa Dr. Slaa!) na inavyoonekana vijana hawa hawataki "mchezo". Magazeti mbalimbali yamelisifia na mengine yameliponda tamko hilo hasa kutokana na lugha yake kali ambayo inaweza kuendelea kuchochea moto wa chuki na uhasama miongoni mwa Watanzania. Hata wanablogu pia wamefanya hivyo hivyo. Kama alivyosema Profesa Mbele, tuendeleeni kufanya hivi kwa njia za amani. Mungu Aendelee kuibariki Tanzania!!!
Tamko hili ni kutoka Jamii Forum
 
***********
Inaonekana sasa ni mwendo wa  matamko tu. 
Kuna tamko jingine la Kamati Kuu ya CCM HAPA...

2 comments:

 1. Siku ya siku itafika, siku ambayo mawe yatageuka kuwa SMG na wala nchi watakavyowaachia watanzania nchi yao. Kutoka hapo kila chembe ya utajiri uliotokana na ufisadi utakapotaifishwa na kugawanywa kwa usawa kwa watanzania wote.

  Jengeni majumba yenu ya kifahari yenye mabwawa ya kuogelea lakini ipo siku kiongozi mfano wa Sokoine atajitokeza na kuwahoji mlizipata wapi hizi pesa wakati mtanzania wa kawaida anaishi kwa chini ya dola moja kwa siku. Ndipo hapo mtakapokwenda kumwaga mapesa yenu ya kifisadina haramu kwenye bahari ya hindi.

  Kilichotokea Tunisia ndicho kitakachotokea Tanzania na kwingineko katika bara la Afrika kwasababu ya ubinafsi wa viongozi wetu.

  ReplyDelete
 2. Mie sijaelewa. UVCCM, hivi inapinga au kuunga mkono mambo yaliyoparaganyika. Nimesoma wanawashambuliwa Sitta na Mwakyembe kwa kumpinga Ngeleja kuhusu malipo ya Dowans. Lakini wao wamejifanya wanayapinga. Kama kweli wanapinga si basi wangeunga na Sitta na Mwakyembe wanaowashutumu kueneza tofauti na chuki" Je wao kwa kupinga wamejenga mshikamano baina ya mafisadi na wasafi au wamewabomoa wapinga ufisadi wakiwapa ujiko mafisadi. Mie naona ni kama karata tatu au kuishiwa hoja na kudandia mambo.
  Slaa anajulikana kupinga na kufichua ufisadi. Ajabu kijana mdogo na nyemelezi kama Shigela eti anamuita kichaa kama ambavyo Rostam na Lowassa wangemwita. Je huyu kweli anapambana na ufisadi au anaupamba kinamna.
  Mie sijawaelewa hawa watoto wa mafisadi. wanapata wapi uchungu na nchi hii wakati ufisadi ndiyo umewafinyanga na kuwafikisha hapo walipo"
  Akili kichwani

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU