NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Thursday, January 6, 2011

TUHITIMISHE NINI KUTOKANA NA TASWIRA HIZI ZA MKE WA DR. SLAA?

 • Bila shaka picha hizi za anayesadikiwa kuwa mke au mchumba wa Dr. Slaa akibubujikwa na damu baada ya purukushani za maandamano ya Chadema jana kule Arusha zinasikitisha. Inasemekana kwamba kuna hata watu waliopoteza maisha. 
*****************
 • Je, huu ni mwanzo mbaya kwa mwaka 2011?
 • Ni kielelezo na kiwakilishi cha mapambano na upepo "mkali" wa mabadiliko na mwamko unaovuma?
 • Ni matokeo ya uvunjaji wa sheria kwa walioamua kutumia ubabe, kuonyesha dharau na kuamua kufanya maandamano bila kibali?
 • Ni ubabe wa wamiliki mfumo na ujeuri wao wa kushindwa kusoma alama za nyakati, kutumia busara na kuwa na subira?
 • Nani alaumiwe na hata kuwajibishwa? Kwa nini tumefikia hatua hii na vipi huko tunakoenda?
***************** 
 • Nimesoma maoni mengi yaliyotolewa na wasomaji katika tovuti ya gazeti la Mwananchi na Michuzi na yanaonekana kulaumu pande zote kwa kukosa busara na uvumilivu. Kuna mengi ya kujifunza na natumaini kwamba pende zote mbili zitatumia busara ili purukushani kama hizi zisitokee tena. Mungu Ibariki Tanzania!

4 comments:

 1. Je, katika dunia hii ya ushindani, washindani wa Tanzania katika mambo ya utalii, wakiamua kutumia picha hizi katika kuwaelezea walimwengu kuhusu Tanzania, tutawalaumu?

  Haya hayangetokea iwapo nchi ingekuwa na uongozi wa busara. Mwalimu Nyerere aliyabashiri hayo, na akatutahadharisha, katika kitabu chake cha "Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania," kilichochapishwa mwaka 1993.

  Kwa kuzingatia yaliyomo katika kitabu hiki, na maandishi na hotuba zingine za Mwalimu, wapiga kura wa Tanzania wangekuwa wanatumia akili wakati wa kupiga kura. Lakini kwa vile ujinga ndio chaguo la wa-Tanzania, wakubali matokeo yake.

  ReplyDelete
 2. Professor Mbele kasema yote yaliyokuwemo akilini mwangu hasa kuhusu utalii. Kwanza utalii Tanzania ndio umeanza kupanda baada ya kujitangaza kwingi and so on. Sasa a tourist generating area like Arusha then vurugu zote hizi zinatokea, ni hatari sana kwenye soko la utalii ila Tanzania kwa kweli sijui tunaelekea wapi. Sikudhani hata siku moja tungefikia huku kabisa.

  PS: I hope I don't sound rude but if you "ignore" the blood...the woman looks fine and so determined. Even with the blood she seem to want to protest even more...this scares me

  ReplyDelete
 3. Kevin (a.k.a. Mzee wa Busara)January 7, 2011 at 5:48 AM

  Huyu mama imekula kwake. Yeye alimkimbia mumewe wa ndoa kwenda kwa huyu padri mzinzi thinking that she would become a first lady. Matokeo yake ndo haya. Kweli chema chaji... na kibaya chaji... May be waingie msituni na padri wake kuendesha maombi lakini malengo yao ya kuleta vurugu katika nchi yetu KAMWE will never be realized.

  Hongera CCM kwa kuwashupalia hawa. They have to abide by the law. Hata huko Vatican kuna sheria. Pambafu kabisa!!!

  ReplyDelete
 4. Mwalimu Mbele. Hilo swali la utalii naona tayari limeshaanza kutajwa kama athari mojawapo ya tukio hili. Hata hivyo sina uhakika kama kuna anayejali sana. Wakenya wamekuwa wakidai kuwa Mlima Kilimanjaro na Serengeti viko kwao kwa muda mrefu na wizara yetu ya maliasili na utalii haijasema lolote kwa muda mrefu. Sidhani kama wanajali sana. Kila siku hapa ni kugombana na wanafunzi wanaotaka kwenda Kenya kupanda Mlima Kilimanjaro!!!

  Matatizo mengine ya Watanzania kweli ni ya kujitakia lakini mabadiliko yameanza kutokea na tumeanza kuyaona. Mabadiliko ya kifikra ni jambo la pole pole na tuyape muda kwani kasi ikiendelea hivi baada ya miongo kadhaa tu ijayo watu watakuwa wanafikiri mara mbilimbili kabla hawajaenda kuchukua fomu za kugombea urais!

  Candy1 - Angalizo zuri. Kumbe nilikuwa sijaiangalia picha hii vizuri lakini ni kweli. Japo mwanamke huyu amelowa damu lakini kabisa anaonekana hana hofu yo yote; na yuko tayari kusonga mbele tena kwa ujasiri na bashasha. Naweza kuyaona matumaini katika paji la uso wake. Pambazuko!!!

  Kevin (a.k.a. Mzee wa Busara) - no comment! Hufikiri kwamba nguvu kupita kiasi zimetumika hapa?

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU