NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Monday, January 3, 2011

UCHAWI SASA NI KAZI HALALI NCHINI ROMANIA !!!

 Picha hii ni kutoka kwa wafalme wa udaku Bongo.
*********

Kuanzia juzi tarehe 1/1/2011, uchawi umetambuliwa rasmi kama kazi halali kule Romania na wachawi sasa wanatakiwa kulipa kodi kama wafanyakazi wengine. Kwa habari zaidi soma hapa. Kama nilivyowahi kugusia hapa, uchawi upo hata Ulaya na Marekani ingawa pengine ni kwa "rangi" tofauti na ile yetu ya kuua maalbino; na vikongwe kule kanda ya ziwa. Kwa habari zaidi kuhusu imani za uchawi Afrika, soma hapa na hapa.

4 comments:

 1. Hata mimii nilikuwa na wazo hilo kuwa hawo wanaoitwa wachawii wangeboresha huo uchawi wao, mfano kama wanaweza kusafiri na ungo , kwanini wasiiweke hadharani wakapata pesa, na kuacha `kuumiza watu' akisafirisha mtu mmoja toka Dar hadi mosho keshatajirika.
  Uchawi kuwa biashara, mbona inachekesha, lakin nasikia masharti yanawagonga...LAKINI HEBU TULIWEKE HIVI, MFANO UMEAMUA KUVUNJA masharti kwa nia njema, MCHAWI ikaboresha mambo yako siutakuwa umetenda mema, na hata hawo wanaoogopewa kuwa ukivunja masharti watakasirika, hatimaye watakuunga mkono..Zamani dawa za kienyeji zilikuwa hazitangazwi siku hizi zinztangazwa, ...wazo nii hilo, boresha uchawi uende na wakati ufaidike au sio
  Ni wazo tu mkuu MMN

  ReplyDelete
 2. uchawi bado ni kitu kipana zaidi na unadefinition nyingi japo ni nani wa kudefine! ni kitu tata bado

  ReplyDelete
 3. kuna haja ya kuanza na mapambano dhidi ya uchawi Tanzania pamoja na kuwa nchi kama Romania wameukubali. ila sasa tatizo ni kuwa uchawi hauna mipaka. kweli kazi ipo maana hata mchawi wa Romania anaweza kuleta maafa Tanzania, dunia hatuna budi kuungana kuutokomeza ikiwezekana.

  ReplyDelete
 4. Emu-three: Nakubaliana nawe. Kuna mambo mazuri yanayoweza kupatikana kutokana na uchawi kama utafanywa kwa uwazi. Kama ni kweli wanaweza kusafiri kwa kasi tena kwa ungo, kuna usafiri gani rahisi kama huu? Tufundishane tu mashuleni ili kieleweke.....

  Kamala - tunakutegemea wewe mtu wa utambuzi utufafanulie vizuri kuhusu suala hili.

  Albert - Mimi zamani nilidhani kwamba elimu ndiyo itaangamiza uchawi lakini cha kushangaza sasa ni kwamba mashule na wasomi wameongezeka na uchawi ndiyo umezidi. Kuna nini?

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU