NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Monday, January 24, 2011

WACHAGA WABAKI JINA TU. WENGI HAWAJUI MILA NA DESTURI ZAO !!!

 • Shemeji zangu Wachaga eti wamebakia jina tu. Wengi hawajui Kichaga - hata kile cha "kuombea maji".
 • Kati ya watoto 10, ni wawili tu wanaoweza kuongea Kichaga vizuri. Watatu wanaweza kuongea maneno machache tu na waliobaki hawawezi kabisa. Na wote hawa ni watoto wanaokaa vijijini.
 • Hali hii ikiendelea kwa muda mrefu, Kichaga kinaweza kuwa katika hatihati ya kutoweka. Vipi kuhusu lugha na tamaduni za makabila mengine? Swali lilishawahi kuulizwa hapa kwamba, watoto wanapokoma kuongea lugha zao za mama, wanakuwa nani? Ati, inawezekanaje mtu uitwe Mchaga wakati hujui lugha wala utamaduni wa Kichaga? Wachaga mnasemaje kuhusu suala hili? Pengine itabidi angalau msome hiki kitabu kizuri kilichoandikwa na Mangi Petro Itoshi Marealle. Habari kamili inafuata hapa chini.
 ***************

Wachaga wabaki jina, wengi hawajui mila na desturi zao


‘Shimbonyi’ ni salamu kwa kabila la wachaga, salamu ambayo imekuwa maarufu hata kwa  baadhi ya watu ambao sio wa kabila hilo, lililopo mkoani Kilimanjaro.

Lakini kinachoonekana kama dalili za kupotea kwa kwa lugha ya kichaga ni jinsi watoto wa kabila hilo ambavyo wameshindwa kuitumia lugha hiyo kutokana na kushindwa kuzungumza kichaga.

Iwapo utatembelea maeneo ya Marangu, Kibosho, Machame na sehemu nyingine za uchagani,  utashangaa kuona watoto wengi wa kichaga  hawaongei lugha yao ya asili.

Kati ya  watoto 10 ni wawili tu wanaoweza kuongea vizuri kichaga, watatu wanaweza kusema maneno machache na waliosalia hawawezi kabisa kukiongea.

Ukiwauliza wazee wa kabila huwezi kupata jibu sahihi la tatizo hilo, hivyo kupata ukweli wa mambo ni lazima kuangaliwe historia ya kabila hilo japo kidogo.

Inasemekana kuwa wachaga walifika Kilimanjaro karibu miaka 500 iliyopita wakitokea maeneo ya Afrika Magharibi kwenye pembe za Mto Niger.  Kutoka kwao huko inasemekana kulitokana na ugomvi wa kikabila ambao uliwalazimisha kuhamia maeneo yaliyokaribu na mto Kongo uliopo Afrika ya Kati eneo ambalo vitabu vingi vya historia hulichukulia kama ndio chimbuko halisi la wachaga.

Hali ya hewa kwenye bonde la mto Kongo haikuwa nzuri,  hivyo iliwalazimu tena kuondoka mpaka eneo lililoko chini ya milima ya Upare na Usambaa


Hapa walikutana na Wamasai ambao kiasili walikuwa ni wapiganaji vita, hao walikuwa wakilitumia eneo la uwanda mpana  kama malisho ya ng’ombe zao. Baada ya mapambano ya mara kwa mara,  jamii ya wachaga ililazimika kuondoka kwa makundi huku kila kundi likichukua njia yake.

Endelea kusoma habari hii ya kusisimua HAPA.

4 comments:

 1. mmmhhh kaka Matondo leo nimepata kujua wachaga kiundani zaidi kweli baba yangu baada ya miaka 20 hakuna kichaga!lakini waliona mbali na hawakuwa wachoyo na wakabila kwa wageni wakapata shule na hospitali mapema na mwingine anataka kuwa mchezaji wa juu ndoto zake zitafika tuu!
  aksante sana na Ubarikiwe!Tunasubiri na makabila mengine sasa.

  ReplyDelete
 2. Sio wachaga tu makabila mengi sasa hivi yanasambaratika, wengi wanasahamu `ukabila wao' kama lugha, desturi na tamaduni zao...`hayo yanaitwa yamepitwa na wakati' huoni sasa ile iliyokuwa ikiitwa jando na unyago, ipo wapi, tumeona tutafute ile inayofanana fanana na uzungu -kitchen party...!

  ReplyDelete
 3. hilo nalo ni neno. MILA zinatoweka.

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU