NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Sunday, January 23, 2011

WAKATI MWINGINE "LOJIKI" INABIDI ITUMIKE !!!

5 comments:

 1. DUH!

  Nimekumbuka enzi hizo na baadhi ya watu ambao sitawataja hapa kwa kuwa siku hizi ni WAHESHIMIWA tulikuwa tunanunua gongo halafu tunaimix na FANTA na kuiweka kwenye chupa bomba halafu twainywa kwa maringo na yote ni kutokana na matatizo ya NGAWIRA pesa!:-(

  ReplyDelete
 2. Kaaaazi kwelikweli. Maisha haya jamani na wewe Simon umekunywa hadi gongo Duh!

  ReplyDelete
 3. Maisha kutapatapa, na kupata je? Nyongeza ya matapu tapu...hivi mwili una kazi sanaeee.

  Fikra zinabishana ila hakuna kugonga hodi, sasa hebu tuamue ni nini na kipi hapa, kuendeleza au kuendekeza.

  Ugumu ndio utaanzia hapo maana kila mmoja na alichozozea. Ngoja nikwambie Wakati mwingine tufikirie Hatma ya Maisha na hukumu ya MUNGU.

  Nipe 5 kama umesadiki.

  ReplyDelete
 4. Hii katuni inafikirisha. Ni suto kwa watawala wetu na polisi wao. Ajabu hawa ndiyo wanaopiga waandamanaji wanaoandamana kupinga chanzo cha matatizo haya ya kijamii! Je tatizo ni kufikiri kwa tumbo au kuuweka ubongo tumboni?
  Matondo unawachokoza kweli kweli! Ajabu huyo ndata akipewa chochote kitu hiyo gongo itageuka bia na kuwa halali. Ila asipokatiwa kitu gongo itageuka kuwa bange hata mihadarati!
  Hakuna kitu kibaya kama kutumia tumbo kufikiri.

  ReplyDelete
 5. Ndugu yangu, umerejesha fikra zangu wakati nikiwa kijijini. Tatizo la nchi yetu, madaraka mara nyingi huwa ni makubwa zaidi ya kipato halali. Nakumbuka wauza bia kijijini ilikuwa inasadikika walikuwa mpaka wanahonga polisi ili wakawakamate wauza gongo ili biashara yao ipate wateja kwa vile watumiaji wengi walikuwa wananunua gongo badala ya bia kutokana na bei ya bia kuwa ya juu ukilinganisha na gongo. Tatizo ni kuwa, polisi wengi walikuwa wanafumbia macho tatizo la uuzaji wa gongo kwa vile wengi wao walikuwa ni watumiaji kutokana na kipato chao kuwa ni kidogo au kwa vile walikuwa na uhusiano wa karibu na wauzaji.
  Kutokana na kipato kuwa ni kidogo na urahisi wa upatikanaji wa gongo, tulijenga msemo usemao, kama nia ni kulewa, kilevi ni kilevi hata kama ni mataputapu.
  Katika mazingira kama hayo sidhani kama rushwa inaweza kufutiliwa mbali!!

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU