NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Monday, January 17, 2011

WATANZANIA WATUMIA SH. BILIONI 555 (DOLA MIL.396) KWENYE SIMU KWA MIEZI MITATU TU !!!

 • Nani anasema Watanzania ni masikini sana? Ripoti iliyotolewa na Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA) inaonyesha kwamba kati ya Julai na Septemba mwaka jana, Watanzania walitumia jumla ya shilingi bilioni 555 (sawa na dola za Kimarekani milioni 396!) kwenye simu. Hii ni sawa na shilingi bilioni 185 kwa mwezi.
 • Ripoti hiyo inaonyesha kwamba kuna watumiaji wa simu wapatao 20,771,487 nchini Tanzania na kwamba katika kipindi hicho cha miezi mitatu kila mtumiaji alitumia shilingi 26,724 kwenye simu
 • Kampuni ya Vodacom ndiyo inaongoza kwa kuwa na watumiaji wapatao 8,426,097 ikifuatiwa na Airtel (5,901,634), Tigo (4,575,534), Zantel (1,586,516), TTCL (256,064) na SasaTel (23,071)
 • Kama vile mdau mmoja alivyodai, hapa bado hujaongeza bajeti ya bia na michango ya harusi. Pengine ni kweli kwamba tatizo letu siyo umasikini bali ni kushindwa kuelekeza nguvu zetu katika mambo ya msingi. Uboreshaji wa njia za mawasiliano hususani simu na mtandao ni hatua nzuri katika kujiletea maendeleo hasa kama zitatumiwa vizuri na kwenye mambo yanayohusu maendeleo. Inabidi sasa tukaze macho vijijini ambako ndiko waliko wananchi walio wengi. Kwa hakika takwimu hizi za TCRA zinafikirisha!
Picha na ripoti kamili ni kutoka gazeti la Citizen 
na vyote vinapatikana HAPA...

  10 comments:

  1. Nahisi kuwa sehemu kubwa ya mawasiliano yetu ni udaku, umbea, na majungu. Ingekuwa tunatumia mawasiliano hayo zaidi kwenye masuala ya manufaa, leo tungekuwa mbali.

   ReplyDelete
  2. Kevin (a.k.a. Mwenye busara)January 17, 2011 at 9:57 PM

   Simu kwa Watanzania ni ujiko tu hakuna la maana. Ni za kutongozea. Tazama kwenye facebook watu wanavyotoa namba zao hovyo hovyo ndo utajua kwamba ni ulimbukeni tu unatusumbua. Ni wachache sana wanaotumia simu kwa mambo ya maana.

   Mtandao ndo usiseme kabisaaaaaa. Ni kwa ajili ya kutazama picha chafu za ngono. Niliwahi kufanya research kidogo pale IFM na utashangaa nilichokigundua. Kila mtu anahangaika kutafuta picha na video za ngono na hasa hii inayoitwa TIGO.

   Japo tunapoteza mabilioni yote haya, tusije kuwa surprised kwamba hakuna mabadiliko yo yote katika maisha yetu. Tana bado hujataja ile tabia ya watu kupambana kununua simu za bei mbaya. Mtu yuko radhi akope ili anunue Blackberry kwa laki tisa au milioni moja. Kisa anataka kuwavutia mademu au kumzidi homie mwingine. Tutaendelea kweli? Mashindano yetu ya kipumbavu yapo kila mahali hata kwenye kununua magari, kujenga nyumba na hata idadi ya mademu.

   ReplyDelete
  3. Ni kweli matumizi ya simu ni makubwa sana kiasi kwamba kwa mtu asiyeweka kumbukumbu hawezi kuligundua hilo. Na kama walivyochangia wengine, mazungumzo yenyewe kwenye simu utakuta sio muhimu sana.
   Ingekuwa mtu anaweka kumbukumbu kwa matumizi yake ya simu, angeshituka sana, na huenda angejaribu kuangalia jinsi ya kubana matumizi, lakini wapi...mtu kabigiwa simu ndio anakohoa kwanza, anakunja nne, halafu ndio anaanza kuongea hajui gharama inakula kwa mwenzake!
   Siui kama hili linaweza kuwashitua watanzania na kuangalia njia ya kubana matumizi!

   ReplyDelete
  4. Gharama nyingi hata kwa Afya zetu pia!!!

   ReplyDelete
  5. Kelvin na Mbele mmenena ukweli. Ukitaka kujua kuwa watanzania ni wadaku tembelea nchi kama Kenya hata Zimbabwe. Kule hakuna magazeti ya udaku. The Daily Nation la Kenya huenda hadi kurasa 60 za habari na watu hununua na kulisoma lau nusu. Magazeti ya Tanzania ni kurasa ngapi?
   Tunazidiwa hata na viinchi vidogo kama Burundi na Rwanda hawana magazeti ya udaku!
   Hata ukisikiliza hotuba za watawala wetu zina mapungufu mengi ni ndefu za kutupiana vijembe tu.
   Nenda mitaani hata kwenye dala dala usikilize miziki ya uchafu inayochezwa huku watangazaji malimbukeni wakijaa kwenye runinga zetu wakionyesha uchafu mtupu na hakuna mtawala hata anayestuka kutokana naye kuwa mdau wa mambo haya!
   Mwisho angalia watu wanavyoshindana kuchangia harusi na kitchen party huku wakikimbiza watoto kwenda kusoma kwenye shule za vichochoroni kule Uganda na Kenya. Pia angalia wanavyoshindana kununua simu za bei mbaya bila kusahau wanavyowekeza kwenye mabaa na guest houses za short time badala ya shule.

   ReplyDelete
  6. Ndugu Mhango, nikiongezea kidogo kwa kutumia kofia ya ualimu, ni kuwa hayo magazeti ya Kenya utakuta mara kwa mara yanatumia kurasa kadhaa au nyingi kuongelea vitabu mbali mbali muhimu. Sio rahisi uone gazeti la Tanzania linajadili vitabu muhimu. Unaona wazi kabisa watu mitaani Tanzania hawavithamini vitabu.

   ReplyDelete
  7. Ndugu Mbele usemayo ni kweli kabisa. Hata ukiangalia kiswahili ambacho asili yake ni Tanzania, kinatangazwa kupitia kiswahili kibaya cha Kenya na angalau kizuri cha Mombasa. Watu wengie wanajua kiswahili ni lugha ya Kenya na si ya Tanzania kwa asili.
   Sisi tumewekeza kwenye upuuzi kiasi cha kuanza kuibiwa hata akili yetu tuliyoilaza. Inauma sana kuona kiswahili kikidhaniwa kina asili Kenya wakati Kenya kwenyewe kinadharauliwa. Kimeanza kupata soko na heshima kule baada ya kugundua kuwa kumbe kinauzika na wanaopaswa kukiuza yaani watanzania wamelala. Unaweza kuandika msahafu hapa.

   ReplyDelete
  8. Tukumbuke pia kwamba hizo pesa zitabadilishwa na wawekezaji wa nje na mwisho zitaihama Tanzania!

   ReplyDelete

  JIANDIKISHE HAPA

  Enter your email address:

  Delivered by FeedBurner

  VITAMBULISHO VYETU