NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Friday, February 11, 2011

FIKRA YA IJUMAA: TUZUNGUMZIE VYUO VIKUU "VYA KATA"

 • Hivi karibuni kumekuwa na mfumko mkubwa wa uanzishwaji wa vyuo vikuu katika sehemu mbalimbali nchini mwetu. Hili ni jambo jema sana kwani linaonyesha kwamba tunapiga hatua katika nyanja ya elimu ya juu. Naliunga mkono kwa asilimia 100!
 • Wasiwasi wangu, hata hivyo, ni ubora wa elimu inayotolewa katika vyuo vikuu hivi vinavyochipuka kila leo. Ni kweli vina walimu wa kutosha wenye sifa (PhDs)? Vipi kuhusu mahitaji na miundo mbinu mingine muhimu? Elimu inayotolewa katika vyuo hivi ni ya kiwango cha kimataifa? Nauliza haya maswali kwa sababu juzi juzi hapa nilikuwa naongea na mwanafunzi mmoja ambaye amekuja kufanya shahada ya uzamili (Masters) katika chuo kikuu kimojawapo hapa Marekani na ametokea katika mojawapo ya vyuo hivi vipya ambako alifaulu vizuri sana katika masomo yake ya shahada ya kwanza. Basi alikuwa anaomba ushauri kuhusu nini la kufanya kwani masomo yalikuwa yamemwelemea vibaya sana na amegundua kwamba kumbe kule nyumbani hakufundishwa cho chote cha maana.  
  • Kuna bodi au kamati inayojaribu kuangalia ubora wa elimu inayotolewa katika vyuo vikuu hivi? Isije basi ikawa tunafungua vyuo vikuu kwa mtindo ule ule tunaoutumia katika kufungua na kuendesha shule za kata. Sitaki tuwe na vyuo vikuu "vya kata" kwani madhara yake ni makubwa kwa jamii. Natumaini kwamba hata wewe hutapenda kufanyiwa upasuaji na daktari aliyepata shahada yake ya utabibu kutoka katika chuo kikuu "cha kata"!!!
  Picha (na soma makala kuhusu vyuo vikuu visivyo na sifa) 

   1 comment:

   1. Mkuu, Matondo

    Mimi na kataa katakata yale mawazo ya kusema elimu ni sehemu huru inayejitegemea bila mzazi kuhusika.


    Badala yake na amini kwamba elimu ni sehemu moja au IKO CHINI wa mwamvuli wa kulea mtoto.


    Kwahiyo, sisi wazazi wa wale wanafunzi wanaokwenda vyuoni hivi tuwe kipaumbele kuuliza jinsi mambo yanavoendela huko. Walimu wanafanya kazi kwa niaba yetu, KWISHA!!!


    Kwa hiyo nakushukuru sana Bw Matondo kwatoleo/POST lako hii. Ingawaje haizungumzia mambo ya "kuvutia" kwa wengi... maana yake haigusi mambo ya pesa au mapenzi... lakini inagusia mambo yenye mgongo wa taifa lolote lile: MALEZI NA ELIMU.


    Mungu akubariki, Mkuu!

    ReplyDelete

   JIANDIKISHE HAPA

   Enter your email address:

   Delivered by FeedBurner

   VITAMBULISHO VYETU