NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Sunday, February 27, 2011

HATA KAMA MTU HUJUI KUSOMA HUWEZI KUSAINI MKATABA WA AINA HII !!!

Mikataba ya aina hii itatumaliza jamani.
Halafu tunashangaa eti ni kwa nini gharama za umeme 
zinapanda kila siku. Ni kwa nini lakini hatuwezi kuwa siriazi na raslimali zetu?


....WABUNGE WAPIGWA BUTWAA

...Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini waliotembelea mitambo ya kuzalisha umeme ya TANESCO, wameshitushwa na gharama kubwa za uendeshaji wa mtambo wa kuzalisha umeme wa gesi asilia Ubungo, Dar es Salaam.

Hatua hiyo inatokana na kuelezwa kuwa, wananunua gesi kwa kampuni ya Pan Afrika kwa fedha za kigeni, jambo ambalo limekuwa likiongeza gharama kwa watumiaji.

“Gesi inapatikana mkoani Lindi mnanunua kwa dola za Marekani, halafu mnauza umeme kwa shilingi, hamuoni mnawabebesha watumiaji mzigo usio na sababu,” aliuliza mmoja wa wajumbe hao, baada ya kupata maelezo kutoka kwa Meneja Mwandamizi wa Mitambo ya Gesi na Mafuta, Mhandisi Gregory Chegere.

Chegere alisema hayo ni masharti ya mkataba kati ya TANESCO na Pan Afrika, inayosafirisha gesi kutoka Kilwa hadi mtamboni hapo. Alisema mitambo hiyo inazalisha megawati 100, ambazo huingizwa kwenye gridi ya taifa kwa siku.

 
*********************
Kwingineko....

Mkuu wa Dowans kumbe yuko tayari kusamehe baadhi ya kale kadeni tunakodaiwa....

.....Al Adawi yuko tayari kusamehe fidia ya sh. bilioni 94 lakini kiasi cha dola za Marekani milioni 24 ni lazima kilipwe kwa kuwa ni deni halali.

“DOWANS ilizalisha umeme kwa kipindi cha miezi 10, watu wanaposema deni lote lisilipwe si sahihi. Hawajui fedha wanazolipa umeme zinakwenda wapi, tumezalisha tukawapatia umeme, wameuza lakini mpaka sasa hawajatulipa,” alisema.

Chanzo: UHURU

3 comments:

 1. -Baada ya kusoma hii habari katika gazeti la Uhuru sikupata hata nguvu za kucheka badala yake nilipata nguvu za kusikitika sana. Baadaye, picha mbili zilinijia usoni.
  Picha ya kwanza ilinionyesha ni jinsi gani mhusika aliyesaini mkataba; asivyothamini pesa ya nchi yetu au asiye uamini uchumi wa nchi yetu.Kama sivyo, basi haishangazi kuona kama ni mikono ya rushwa iliyosaini huu mkataba.
  Picha ya pili ilinionyesha ni jinsi gani nchi yetu bado ina viongozi wanaokabidhiwa madaraka makubwa zaidi ya uwezo wao wa kifikra au matendo kutokana na miparanganyiko katika mifumo ya uongozi.
  Kwa jinsi alivyokuwa anaielezea Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, hata yeye, Mhandisi Gregory Chegere alikuwa anaona aibu kama msomi kueleza kuwa bidhaa ya inayozalishwa nchini inananunuliwa kwa pesa ya marekani na kuuzwa humu humu nchini kwa pesa ya Tanzania. Ande makoye enaya!!

  ReplyDelete
 2. Ng'wanaMwamapalala - hata mimi nisiyejua cho chote kuhusu uchumi hili lilinishangaza sana. Inakuwa kama vile ni ile mikataba wakati ule machifu na watemi wetu (akina Chifu Mangungo) walikuwa wakisainishwa na akina Carl Peters na wapelelezi wengine kutoka Ulaya.

  Ali mradi tu mtu kapata "ten percent" yake na kujijengea hekalu lake basi hakuna anayejali na wala hakuna anayechukuliwa hatua. Haki ya mama matatizo yetu mengi ni ya kujitakia tu.

  Tungekuwa wapi kama tungesimamia vizuri raslimali zetu na kuhakikisha kwamba tuna mikataba mizuri na yenye kuleta tija kwa taifa?

  http://matondo.blogspot.com/2011/02/serikali-yapoteza-sh-bilioni-24-za.html

  Kwa mtindo huu, safari yetu ya kuelekea huko tuendako (kama kuna mahali tunakwenda) bado ni ndefu sana. Makoye getegete !!!!

  ReplyDelete
 3. Eng. Chegere ni mtu aliebobea kwenye taaluma hii ya uzalishaji umeme kwa miaka mingi. Hawa wana saini mikataba ndio wanaowaangusha watu kama akina Chegere, sasa JK awashughulikie kama anavyofanya kwa akina D. Yona na B. Mramba, hata kama anacheza kiini macho na hata wafunga lakini awaweke mbele tuwajue. Au la basi kuna uwezekano wa nae hayupo mbali nao

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU