NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Monday, February 7, 2011

HEBU LEO TUYAFIKIRIE MANENO HAYA YA MWALIMU NYERERE KWA MAKINI. TUFIKIRIE TU !!!

 ******************
"Waingereza wana msemo: "Nature abhors a vacuum", "hulka huchukia ombwe". Hata siasa huchukia ombwe. Kama uongozi ni mbovu, upo kama haupo, au upo kwa maslahi ya wenyewe, watatokea watu waujaze uwazi uliopo; hauwezi kuachwa wazi hivi hivi. Lakini uongozi mbovu ni kama mzoga, una tabia ya kukaribisha mafisi na mainzi. Tusidhani kuwa hulka ya siasa yetu ni tofauti na hulka ya siasa ya watu wengine; kwamba sisi tunaweza kuvumilia uongozi mbovu na tusivune matunda ya hulka ya uongozi mbovu" 
 
(J.K. Nyerere. Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania, Zimbabwe Publishing House 1993:52)

7 comments:

 1. Sijui kwanini nahisi ni matusi haya!:-(

  ReplyDelete
 2. Mtakatifu - ni nani anayetukanwa hapa? Acha mafumbo basi.

  ReplyDelete
 3. @Mkuu Matondo: Tatizo la tusi ni nani anatafsiri kitu ni tusi!Kwa hiyo labda wala hatukanwi mtu ingawa ni matusi !:-(

  ReplyDelete
 4. Mwalimu Nyerere....alifikiria sana, akaandika uongozi wetu na hatma ya Tanzania. hivi wenyewe hao wanakiisoma kweli?

  ReplyDelete
 5. Mtakatifu - nimekupata. Je, yawezekana kwamba hili "tusi" linatugusa sote - waongozaji na waongozwaji?

  Fadhy - Maneno ya Mwalimu ni kama vile yamesemwa leo. Ningekuwa kada wa chama ningeamrisha kwamba kila mwanachama akisome kitabu hiki cha Mwalimu badala ya hali ya sasa ambapo hata kukipata tu ni mbinde!

  ReplyDelete
 6. Maneno haya ni makali na mazito ambayo kwa kiwango kikubwa yalielekezwa kwa serikari ya awamu ya pili. kitu ambacho kilinishangaza kidogo ni kuona Mwalimu alibadilika na kuwa mlalamikaji kama wananchi wa kawaida wakati yeye ndio aliyetuletea hao watu na akawapigia ''debe'' ili waunde serikali.
  Imeanza kuonekana kama maneno haya pia yameanza kufanya kazi katika serikali ya awamu ya nne. inanitatanisha kuona rais wa awamu ya nne pia anakuwa mlalamikaji katika maswala ambayo tulitegemea yeye kama kiongozi wetu awe ni mfumbuzi. Hii inatulejesha kwenye hoja ya Mwl Nyerere, nani ni kiongozi na nani ni mwongozwaji au Tanzania ya sasa iko kwenye "hulka huchukia ombwe" au labda ninaota ndoto za jioni.

  ReplyDelete
 7. N'wanaMwamapalala - tukumbuke pia kwamba Mwalimu aliyasema haya maneno baada ya kuwa ameshaachia ngazi. Kuna tofauti kidogo kati ya kulalamika wakati umeshaondoka madarakani (hata kama kile unachokilalamikia we ndo ulikianzisha) na kulalamika huku bado ukiwa madarakani. Huu ulalamikaji wa pili nadhani unashangaza kidogo!

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU