NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Friday, February 11, 2011

HIVI VIATU MBONA KASHESHE? INAONEKANA WENGINE WAMEAMUA KUVIBEBA KABISA !!!

Mwenye katuni ni Said Michael

13 comments:

 1. U wiiii, mbavu zangu mieeee! kwi kwi kwi kwi kwi kwiiiiiiiiiiiiiii!

  ReplyDelete
 2. huo ni ujinga tu. Uhuru wa vyombo vya habari unatumika vibaya, hapo una maana gani? Kwani nyerere hakuwa na makosa ktk utawala wake? Unajua sababu ya kujiuzulu kwake? Nchi ilishamshinda hii na hakujiuzulu kwa mapezi yake ila baada ya kuona ipo siku atakuja kuuwawa.

  ReplyDelete
 3. Kaazi kweli kweli, Mh.

  ReplyDelete
 4. Uadilifu wa Nyerere unajulikana ndani na nje ya Tz.Mapungufu yake yanajulikana pia.

  ReplyDelete
 5. Anony. wa pili. Mimi nadhani Tanzania ni nchi mojawapo ambayo ina uhuru mkubwa sana wa vyombo vya habari barani Afrika hasa ukizingatia kwamba muda si mrefu tu uliopita tulikuwa na magazeti mawili (ya serikali na chama) na redio moja ya taifa. Leo hii mtu unaweza kusema karibu kila kitu unachotaka. Ndiyo maana watu wanaweza kuchora katuni kama hizi bila wasiwasi wo wote - jambo ambalo wakati wa Nyerere lisingewezekana. Tumepiga hatua kubwa sana.

  Kuhusu uhuru wa vyombo vya habari kutumiwa vibaya katika katuni hii sina uhakika. Kwa namna moja au nyingine viongozi wetu wote ni lazima watapita katika chekecho la Historia na historia ndiyo itaamua yupi aliifanyia mema nchi yake, yupi alijaribu, yupi aliboronga, yupi alifanikiwa n.k. Nionavyo mimi hakuna kiongozi ambaye atakuwa na mafanikio tu bila kuwa na matatizo au matatizo tuu bila kuwa na mafanikio.

  Nyerere anasifiwa sana ingawa kusema kweli siasa zake nyingi na sera zake nyingi ndizo zinazotawala mpaka sasa. Yeye ndiye mwanzilishi wa kila kitu; na kwa mantiki hii hawezi kukwepa lawama. Kwa maoni yangu, kitu kimojawapo ambacho kinamfanya aendelee kupendwa ni ule ukweli kwamba hakuwa mnafiki na kwamba alikuwa anaamini kabisa katika kile ambacho alikuwa anakihubiri mf.ukombozi wa bara zima la Afrika, siasa zake za ujamaa n.k. Watanzania wanavutiwa sana na ukweli kwamba hakujaribu kujitajirisha yeye na familia yake mbali na ukweli kwamba alikaa madarakani kwa muda wa zaidi ya miaka 20! Ukweli huu unamfanya asameheke kirahisi pamoja na ukweli kwamba ni kweli alipoondoka uchumi ulikuwa umevurugika na alikuwa haambiliki (Zidumu Fikra Sahihi...!!!)

  Tanzania 2 alipewa nchi yenye uchumi uliovurugika na isiyo na nidhamu. Alijaribu kiasi chake na alitawala kulingana na mazingira ya wakati ule. Pengine mazingira aliyoyakuta ndiyo yalimfanya afanye aliyoyafanya mpaka Watanzania wakambatiza jina la Mzee Rukhsa. Inavyoonekana tayari Historia iko tayari kumsamehe na nadhani anaangaliwa vizuri na Watanzania walio wengi kwa wakati huu.

  Kwa maoni yangu rais aliyefanya kazi nzuri zaidi ya kuleta nidhamu serikalini ni Tanzania 3. Huyu alirithi nchi iliyokuwa imevurugika kabisa, rushwa za waziwazi, misamaha ya kodi ilikuwa imetawala na ukusanyaji wa mapato ulikuwa karibia ziro. Alikuwa mkali na muda si mrefu mambo yalianza kunyoka. Yapo makosa aliyotenda na mwenyewe amekiri mf. kutokuwa mwangalifu zaidi katika zoezi zima la ubinafsishaji wa mashirika mbalimbali na baadhi ya mikataba. Ni wazi kwamba aliiacha nchi ikiwa na "afya" nzuri mno ikilinganishwa na alivyoikuta.

  Tanzania 4 alirithi nchi yenye nidhamu na iliyokuwa na msimamo kiuchumi na hata kisiasa. Pengine kati ya marais wote huyu ndiye aliyerithi nchi yenye hali na mwelekeo mzuri zaidi. Yapo mengi mazuri amefanya na pia kuna matatizo mengi ambayo amepambana nayo - na hasa upinzani kutoka kwa "wenzake" kuhusu suala zima la ufisadi. Mimi nadhani pia ni mpole kidogo katika kukemea maovu na hali hii inawachanganya baadhi ya watu kiasi cha kufikia hatua ya kumdhania kwamba pengine naye anahusika katika baadhi ya masuala haya anayoyanyamazia (mf. Dowans). Huyu bado ana muda wa kurekebisha historia yake na ameshaahidi kuchapa kazi kwa bidii.

  Katuni hii inatafakarisha na sidhani kama ni matumizi mabaya ya uhuru wa habari. Ni kielelezo kizuri cha safari yetu kupitia katika jicho la viongozi wetu.

  ReplyDelete
 6. kwani kila kiongozi wa tanzania lazima aongoze kama alivyongoza nyerere? kila kipindi kina kizazi chake na changamoto zake.

  ReplyDelete
 7. Mwaipopo - pointi nzuri. Wakati mwingine ni bora kutupilia mbali viatu ulivyoachiwa (hasa kama ni chakavu au kama vimepitwa na wakati) na kujichongea viatu vyako mwenyewe hasa kama unaamini kwamba vitakufikisha huko unakotaka kwenda - wewe na waongozwaji wako.

  ReplyDelete
 8. Tutaongea yote lakini ukweli unabaki pale pale kuwa pamoja na udhaifu wa binadamu, Nyerere alijua alichofanya.
  Pili matendo na maneno yake viliendana. Kinachogomba ni hawa watawala wa sasa ambao hawana mawazo, hawasomi, hawafanani na wasemayo. Watanzania sasa ni kama yatima. Yatima yoyote atawakumbuka wazazi wake hasa pale anapoangukia kwenye mikono ya walezi wabovu. Atawakumbuka wazazi wake tu hata kama walikuwa hawampi kila kitu kuliko wanaomuahidi uongo na upuuzi mtupu. Tuyaache.
  Kuchonga viatu vipya ni bora kama kweli unachonga viatu na si kuchonga maneno.
  Sera za Nyerere hata kama zilifeli angalau kuna "makaburi" ya aliyotenda kuliko hawa ambao hawana "makaburi" zaidi ya mifupa na mashimo.
  Tuliosoma wakati wa Nyerere tukiangalia wana vyuo wa sasa wanavyodhalilika tunamkumbuka taka usitake.

  ReplyDelete
 9. Nyerere! mwanasias wa aina yake, naona kama alishindwa zaidi ya kushinda ila hiyo picha ni kiboko

  ReplyDelete
 10. Pamoja na kwamba mimi siyo mtaalamu wa kuelewa ujumbe hasa unawakilishwa kwa njia ya vikaragosi. Hivi vikaragosi ndiyo vinanichanganya zaidi. Ningelipenda kama kuna uwezekano kupata ufafanuzi zaidi hasa kutoka kwa Said Michael.
  Nikiangalia inaonekana kama kiatu kinawakilisha nchi, na kama ndivyo hivyo, Nisingependa kumuongelea kiongozi aliyevaa kiatu TZ1 kwa vile inaonekana kiatu kilimuenea ipasavyo!!! na kwa hilo inakuwaje kiongozi wa kiatu TZ3 kimempwaya zaidi ya kiongozi wa kiatu TZ2. Mimi nafikili Kiongozi aliyevaa kiatu TZ2 kingempwaya zaidi ya kiongozi aliyevaa kiatu TZ3. Nchi aliyoiacha kiongozi aliyevaa kiatu TZ3 ilikuwa bora zaidi ya aliyoicha kiongozi aliyevaa kiatu TZ2.
  Pia ninashindwa kuelewa kwa nini wawili wako ndani kunako ashiria mawingu na wawili wako tu nje.

  ReplyDelete
 11. Hii picha kila mmoja anaweza kutafsiri kutokana na atakavyoona, mimi naona hawa waliopo ndani ya minara mirefu yenye mawimbi yaliyokatika, ni viongozi waliokuwa wanathubutu,yaani walijaribu kufikiri zaidi kabla ya kutenda,maana yake ni kwamba walikuwa na maamuzi magumu ambayo yalikuwa yakileta misukosuko kwa kuwa wengi wao waliyakataa lakini yalileta manufaa kwa wananchi.
  Waliokuwa nje ya nyumba waliamua tu bila kufikiria ili mradi wameshauriwa na pia ili mradi wengi wamekubali,bila kujua maamuzi hayo yataleta faida au hasara kwa wanaowaongoza. Kila mtu atasema alichoelewa ila aliyechora ndo mwenye majibu, sisi tunajaribu kuangalia tofauti tulizoziona tangu uongozi 1.Japokuwa hata sisi si wakamilifu.

  ReplyDelete
 12. Ni bora huyo ambae hakuvivaa kabisa, kwasababu ameogopa labda vitakuwa fungus, ana akili sana na anajua kabisa kuwa mtu ni afya,havai mtumba huyo, anakwenda na wakati, Yes!

  ReplyDelete
 13. FUNGUS WA UBONGO NI HATARI ZAIDI MAANA KAAMUA KABISA KUJITWISHA

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU