NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Sunday, February 6, 2011

HUYU MWIZI KACHEMSHA VIBAYA SANA !!!


Ni kule Maryland nchini Marekani. Jamaa kavunja na kuingia ndani ya nyumba ili "kuchaji" simu yake. Simu hiyo haikuwa na chaja kwa sababu katika mtaa wake hakukuwa na umeme kutokana na barafu nyingi iliyokuwa imeanguka katika eneo hilo. Basi baada ya kuichomeka simu yake kwenye umeme ili ipate chaja, wenye nyumba wakarejea. Huyoo akakurupuka na kuiacha simu. Polisi wakaitwa na walipopiga baadhi ya namba zilizokuwa kwenye simu hiyo,  jamaa akakamatwa kwa ulaini tu. 

Baadaye imegundulika kwamba kumbe jamaa ni mwizi sugu ambaye ameshawaliza watu kibao katika maeneo hayo na polisi walipokwenda kupiga sachi nyumbani kwake waligundua vitu vingi tu vya wizi. Jamaa bado yuko jela na dhamana yake imeamriwa iwe 1,100,000. Tangu hapo siku za mwizi ni arobaini ati! Kisa cha huyu mwizi kinapatikana HAPA.

No comments:

Post a Comment

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU