NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Monday, February 28, 2011

KABINTI KANGU KA MWISHO KAMEFIKISHA MIAKA MITATU

Kanaitwa Johari na ndiko kamalaika ka mwisho (gawalaga) katika familia yetu. 
Na sasa Mungu Amekajalia kufikisha miaka mitatu.
Tunakatakia kila la heri.
Hebu Mungu na Akajalie maisha marefu, yenye furaha, amani na ridhiko.

Keki ni lazima ziwe na Dora the Explorer!

Shamrashamra nyumbani na Chuck E. Cheese's

15 comments:

 1. Hongera kwa binti yetu Johari kwa kutumiza miaka mitatu.

  ReplyDelete
 2. Haaa, Hongera sana Johari, Tunakuombea kwa Mungu akupe ulinzi utokao kwake.

  Umependeza kweli Johari. !Happy Birthday!

  ReplyDelete
 3. Matiya na Anony - asanteni.


  Kamala - Unaonaje tukigeuza kibao na kusema kwamba Mwombeki awe ndo kifaa cha Johari? Au mfumo dume utakuwa umepinduliwa?

  Mwombeki mwenyewe anayetafutiwa "kifaa" bado anavaa nepi! Au ni yale yale ya mtoto wa nyoka ni nyoka?

  ReplyDelete
 4. Hongera sana na kila la heri.

  ReplyDelete
 5. Hongera sana Kifaa Johari, Mungu akuzidishie mamiaka tele.

  Kaka Matondo ina maana huongezi mwingine? naona umetumia sana hili neno la kabinti ka mwisho..

  ReplyDelete
 6. Da Mija. Nimeshatosha na haka ndiko ka mwisho. Ukisikia kengine basi jua kuwa ni ka kubambikiwa tu!!!

  http://matondo.blogspot.com/2009/12/watoto-wa-kubambikiwa-nani-wa-kulaumiwa.html

  ReplyDelete
 7. Hongera da Johari!!Mungu akubariki katika maisha yako!!

  ReplyDelete
 8. nadhani nimechelewa keki ila hoja haichelewi...swali la Da Mija halijajibiwa vema....lol!

  Hongera Johari

  ReplyDelete
 9. Hongera sana Profesa Matondo. Kabinti kenu ni kazuri sana. Mungu amlinde na awalende familia yenu yote.

  ReplyDelete
 10. Hongera mwanangu Joharia, Mwenyezi Mungu azidi kukulinda na kukuongoza katika maisha yako ya hapa duniani. Damu ya Yesu ikufunike muda wote. Nakutakia maisha marefu yenye Amani, Upendo na furaha tele. Aaaaaaahhhhh shemeji hakuna kubambikiwa hapo wakilema sio zetu hizo we are very innocent. Lol

  Ma mdogo Lucy

  ReplyDelete
 11. @Ng'wanambiti - Asante. Swali la Da Mija limejibiwa sawasawa na kwa ufasaha kabisa.

  @Da Mija - unamuunga mkono Chacha kwa lipi? Kubambikiwa ama? Nshatosha miye na kazi niliyotumwa na Mungu ya kuutawala na kuujaza ulimwengu nshaitimiza !

  Shemeji mpendwa Lucy - Asante kwa sala zako. Bila shaka Mungu wetu mwenye neema amezisikia. Natumaini pia kwamba Mungu Anaendelea kuwabariki nyote.

  Ulisoma lakini jinsi Wachaga mlivyoshambuliwa hapa:

  http://matondo.blogspot.com/2011/02/wito-kwa-wachaga-kisomeni-kitabu-hiki.html

  Najua wa-Kilema mko innocent. Hizo takwimu za kubambikizana watoto ndizo zinatisha.

  Asante sana shemeji yangu mwema !!!

  ReplyDelete
 12. Shemeji umenifurahisha sana leo itabidi nikitafute hicho kitabu. hao wanaotushambulia wacha wajifurahishe tu, namuonea huruma huyo aliyeacha mke kwa udanganyifu, labda angeangalia walikutana kwenye mazingira gani. You know your wife better, alikuwa role model wangu wakati nipo mdogo, ila sijaona characteristics za wakilema sijui tumesahaulika au vp?

  Lucy

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU