NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Saturday, February 19, 2011

MUNGU ATUSAIDIE KUJIFUNZA ILI TUKIO KAMA HILI LISIJIRUDIE TENA !!!


Au Tutafute mechi za kirafiki za kivita ???


4 comments:

 1. Mwe! Labda Atume Malaika wake sasa waje "washughulikie" na "kudhibiti" hivyo vyanzo vya "matatizo" kama "hili la Gongo la Mboto!"
  Kwani hili ni la kwanza? Mbona basi hata tumeshindwa kujifunza "kutokana na makosa" ya tukio lililopita juzi tu...hata wahanga wa Mbagala wengine hawajalipwa?? Ama "tunaponea hapohapo" kwenye matukio kama haya?? Si unakumbuka kwenye tukio la Mbagala watu walitoka hadi Chalinze kwenda kudai fidia..kisa..."wameathiriwa na mabomu yaliyoripuka Mbagala!" Na utashangaa hawa ndio namba moja "kufidiwa", ilhali wale wahanga hasa hadi sasa bado hawajapewa kituy...zaidi tu ya vibaba vya maharage na unga??? Pengine "kuna mavuno" kwa baadhi ya watu?? Pengine...
  Ni akili gani tena tunataka tupewe!!!!
  Ni mawazo tu...Ila INAUMA SANA JAMANI!!

  ReplyDelete
 2. Sijui kama hata tunajifunza kutokana na makosa...
  Wasiwasi wangu ni kwamba Dar kuna kambi za jeshi kibao, na inasemekana zote ziko full loaded hayo "masiraha!" Nina mashaka kuwa kuna siku Dar nzima italipuka...! Mi kwakweli hili linaniuma sana jamani...
  Sasa sijui tufanye maombi ya kufunga?? Tumfungie nani?? Huu ni uzembe..na siyo "jambo lililo nje ya uwezo wa nchi yeu!" Ama pia ukaombe misaada kwa wenzetu watusaidie ku...ah! Hadi napata kigugumizi mie!! Inauma sana! Yale tusiyoweza tunaomba misaada...hata haya tunayoweza tumekaa tu! Uzembe..uzembe..uzembe! Watu kila siku wanapanga tu namna ya "kuchakachua" kodi za walala hoi, tazama wanavyojipa mabilioni ya kodi za "wasio nacho!" Muogopeni Mungu jamani...na mbona hamtaondoka hata na senti??? Hivi nyie mwadhani "Uzima wenu umo katika wingi wa mali mnazojirundikia...tena kwa dhuluma?" Acheni ubinafsi, hebu kaeni mtafute suluhu ya mambo, angalau kama haya ya mabomu ambayo pengine nayo sasa yawe "janga la kitaifa??" Ona raia maskini walivyobomolewa vijumba vyao! Mtu kajikusanya miaka kibao, akajinyima na kuinyima familia yake, withina second, kajumba kake kanayeyuka kama donge la barafy juani! Acha hao waliokufa na wengine kuumia...acha mali zingine zilizoharibiak..! It will NEVER be OK kwa raia kama hao...! Nyie mnachakachua tu kodi zao huko!!!! Tubuni!! Ah! Inaudhi sana.....!!! Ni mawazo tu....!

  ReplyDelete
 3. Kama ni kweli ``HISTORY is a TECHER´´ basi mambo yatajirudia tu tena kwa kuwa labda moja ya funzo ni kuwa watu husahau kirahisi .:-(

  ReplyDelete
 4. Kama kweli JWTZ na viongozi wetu wako siriazi nashawishika kuamini kwamba watafanya kila wawezalo kuhakikisha kwamba jambo kama hili halijirudii tena period!

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU