NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Wednesday, February 9, 2011

MWANAMKE AFARIKI DUNIA BAADA YA KUDUNGWA SINDANO ZA KUNENEPESHA MAKALIO!

 • Inavyoonekana vuguvugu la kuongeza makalio kwa mabinti haliko kwetu pekee ambako dawa za Kichina ndizo zinasifika kwa kazi hiyo, (japo sina uhakika kama ni kweli). Hapa Marekani mabinti huamua kufanya operesheni kabisa au kudungwa sindano makalioni. 
 • Sasa mwanamke mmoja kule Philadelphia amefariki dunia baada ya kupigwa sindano za kunenepesha makalio yake. Inasemekana kwamba yeye na wenzake wawili walikuwa wamesafiri kutoka London Uingereza kuja kudungwa sindano hizo. Mwenzake alidungwa sindano za kuongeza mahips na yeye hakupata madhara yo yote. Wadungaji wa sindano hizo sasa wanasakwa na polisi.
 • Dada zetu kuweni waangalifu na haya mambo. Na kama kweli kuna hizi dawa za Kichina, mnajua madhara yake (ya muda mrefu) ni nini? Jihadharini.

  ********************

  Binti huyu mwenye miaka 20 aliyefariki amejulikana kuwa ni Claudia Aderotimi na aliamini kwamba akiwa na matako makubwa basi angeweza kuigiza katika video nyingi za muziki wa kufokafoka. Habazi zake zaidi zinapatikana HAPA.

   Picha ya mwisho aliyopigwa marehemu kabla ya kudungwa sindano hizo. Ni huyo wa pili kutoka kushoto.

6 comments:

 1. mmmhhh ameendea kifo,Wanawake wenzangu sijui nani aliwaambia uzuri ni makali!.
  Ahsamte kaka Matondo.

  ReplyDelete
 2. Binadamu haturidhiki wenye makubwa wanataka kuyapunguza,wenye madogo na wastani wanataka kuyaongeza yaani mi hata sielewi sijui kwanini watu hatushukuru tulichopewa badala yake tunamkosoa muumba wetu,tena huyo dada alikuwa na miaka 20 tu niliona kwenye news,Kuna mwingine yeye yeye alitaka marekebisho ya sura matokea yake mambo yamekwenda vibaya uso umekwenda upande kabisa!

  ReplyDelete
 3. Jamani nawashauri wanawake wenzangu turidhike na tulivo umbwa. kabla hujafanya chochote jiulize mala mbili.
  Ni wangapi wangependa kuwa kama ulivo wewe? unawazidi wengi kwa uzuri, akili na mafanikio pia. Furahia ulichonacho, kuliko kujiumiza kwa ulichokosa.

  ReplyDelete
 4. takokakosa nakafa

  ReplyDelete
 5. jamani hao wanaofanya ivo itakua watumiaji tigo

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU