NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Thursday, February 3, 2011

NAKUBALI. HUU SI UUNGWANA KABISA !!!

4 comments:

 1. sambamba na hilo kufakamia ugimbi baa kila uchao ilhali nyumbani hawajui hata soda inafananaje miaka nenda rudi!...Si uungwana hata kidogo!

  ReplyDelete
 2. Kwakweli hata mimi huwa inaniwia vigumu kuona watu (hasa wanaume)asubuhi anaingia hoteli au sehemu yoyote inayotoa huduma ya chakula na kujiagizia supu/mtori na chapati mbili pamoja na soda kisha na chupa ya maji. Lakini ukimuuliza ameacha nini nyumbani hana jibu zaidi ya kwamba yeye ndo mtafutaji lakini amesahau kwamba anatafuta kwaajili ya hao aliowaacha nyumbani.

  Siku hizi katika kaya nyingi kichwa cha familia ni mama akina baba wamekuwa ni mikia tena ya mbwa mwoga aliyechoka ambaye ameficha mkia wake, hawajui familia inakula nini, matibabu ni nani anayeshughulikia, nani anasomesha watoto lakini bila aibu hujumuika mezani na kula chakula ambacho wala hajui mama amekipata vipi kama ni kuhongwa na wanaume wengine au ni kwa kuhangaika yote kwake ni sawa tu.

  Anapotoka kwenye shughulli basi apite baa huko atakula mboga (atachoma makuku, mbuzi, kiti moto)na kunywa ugimbi bila kujali kwamba familia yake inaangamia. Mwanamke ukiwa unasubiri eti kuna kichwa cha familia umeliwa, siku hizi dunia imebadilika sana. Akinamama amkeni vinginivyo watoto wenu watakujakuadhirika wasijue la kufanya.

  ReplyDelete
 3. @ Mfalme: Mzee wa Uungwana, niliiweka hii nikijua kwamba utaiangalia tu kwani imegusa kwenye uungwana unaoupigania kila siku

  @ Ng'wanambiti na anony: Hilo la ugimbi ni tatizo la kijamii na kama alivyosema anony. familia nyingi bila kuwa na mwanamke makini hazingekuweko. Wanaume hawaonekani majumbani. Wako kwenye makontena wakinywa bia na kuchoma kuku na washikaji zao. Asante sana anony. kwa maoni yako ya kina. Ni kweli dunia imebadilika.

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU