NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Wednesday, February 23, 2011

NINI KINAENDELEA HAPA ???

Anaonekana anafuatilia gazeti kwa makini sana...


Picha ni kutoka kwa SENGO

11 comments:

 1. anasoma hilo gazeti au ana gazeti jingine ndani yake? kama kweli anasoma basi ni mtindo mpya:-)

  ReplyDelete
 2. Ni kawaida kwa tu kujifanya kwamba wanajua Kiingereza ili waonekane kwamba ni wasomi hata kama hata Kiswahili hawajui.

  Sitashangaa kama huyu jamaa kweli yuko siriazi anasoma hili gazeti la Kiingereza!

  ReplyDelete
 3. Mimi nadhani kafanya makusudi tu,kwasababu kama hajui kusoma kingereza hata picha hajui kuwa kichwa cha mtu kinakaa juu au chini,labda uniambie kama ni kipofu maana kama haoni kabisa ni ngumu kusimamisha mti uliochorwa ukawa mizizi chini,badala yake ataweka mizizi juu.

  ReplyDelete
 4. tukiwaambia kingereza kigumu mnabisha!!!

  ReplyDelete
 5. Yawezekana ni kweli anasoma hili gazeti la ki-Ingereza, tena vizuri tu. Magazeti yanakuwa na vipande kadhaa. Yawezekana amebadili hiki kipande cha nje kwa kukiweka juu chini, lakini huko ndani anakosoma anakuwa ameshika vizuri tu.

  Tena huenda kafanya hivyo ili kuangalia wapita njia watafanya nini au watasema nini. Yuko kwenye utafiti huyu jamaa. Anajua watu watamshangaa, na yeye anawashangaa kwa kumshangaa. Anawaangalia wanaomdhania yeye ni mbumbumbu, kumbe anawasanifu tu :-)

  ReplyDelete
 6. Mie naona kafanya makusudi hasa ikizingatiwa habari ya mbele yaani miaka 34. Si ajabu ni mwanafalsafa anayetabiri CCM kuanguka chali au anayetaka kuonyesha kero na dharau zake kwa CCM. Kumbuka Plato alipowasha kibatari kushindana na mwanga wa jua (phos) mchana vipofu walimshangaa na kumcheka hata kumwita mwendawazimu wasijue wao ndiyo!
  Kimsingi hapa kuna somo kubwa tu hata kama mhusika hakulenga huko.

  ReplyDelete
 7. Kaka Mhango yawezekana mawazo yako yakawa na ukweli ndani yake, MIAKA 34 YA UHURU CHINI YA CCM. Hilo ni jibu, kila mtu anajua mambo yalivyo sasa ndani ya kijani na njano kuwa yapo kama hilo gazeti lilivyoshikwa.

  ReplyDelete
 8. Nilipoiona picha hii nilivutiwa nayo lakini ni lazima nikiri kwamba sikuweza kuwaza kwa undani kama walivyofanya Profesa Mbele, Mwalimu Mhango na Anony. wa pili. Wao wamezama kifalsafa zaidi na kuiangalia picha kwa undani mno.

  Na hii ndiyo faida mojawapo kubwa ya kublogu - kujielimisha na kupanua mawazo na uwezo wa kufikiri. Japo lengo langu hasa lilikuwa ni kuibua mjadala kuhusu hii lugha ya Kiingereza ambayo kusema kweli imeshatushinda pamoja na kuwekeana amri za "Speak English" mashuleni na kutandikana viboko kwa miaka mingi, uchambuzi mpya uliotolewa hapa unafikirisha zaidi. Asanteni sana.

  Mwalimu Mhango: Aliyewasha taa mchana kweupe na kuanza kuwaghasi wakazi wa Athens kwa kuwaambia eti alikuwa anamtafuta mtu mwaminifu alikuwa ni Socrates, Plato au Diogenes?

  ReplyDelete
 9. Bwana Matondo samahani.Nilikosea. Aliyewasha taa mchana ni Diogenes the Cynic au Diogenes of Sinope.Alifanya hivyo akimtafuta mtu mkweli na muadilifu. Kama angekuwapo Tanzania leo msingeshangaa kuona anazunguka Dar akiwa na kibatari kuonyesha mgao na ujambazi wa Dowans.
  Nadhani angejaribu kutafuta duka llinalouza giza baada ya TANESCO kukana kuuza kiza.
  Pia usingeshangaa kumkuta akiomboleza kifo cha watawala walio hai. Angeulizwa kwanini anaombolezea walio hai. Angejibu kipayukaji na kusema. Wafu hawawajui wafu. Kama angebanwa sana angeuliza: aliye hai ni nani wakati wote mnaomboleza msijue. Huenda mngemuona maeneo ya Gongo la Mboto akifanya sherehe. Wengi wangeshangaa na kumuona mwanga wasijue waliodhaniwa kufa G'Mboto wametoa changamoto la kufichua uoza uliojificha nyuma ya madaraka. Wamewaumbua wale wale wanaojiona na kujihisi kuwa hai wakati ni marehemu! Jibu la mwisho lingekuwa: kama mwadhani mko hai mbona mwatenzwa kimaitiiti? Tuyaache. Yanahitaji waliojaliwa kuona visivyoonekana. By the way,nasikitika kutangaza msiba wa African Union jibwa lisilo na meno lililoshindwa kutoa hata pole kwa walibya. Je tatizo ni ile hali ya kuwa wanachama karibu wote kama si mafisadi ni madikteta, wababaishaji na wezi wa kura kama Gadaffi? Tuyaache.

  ReplyDelete
 10. he he he, hiyo ndo Tanzania bwana,si mnaona mambo yanavyokwenda,kama msoma gazeti kabisa. Matondo wewe ulituambia humjui mtu aliyekuja kukuwekea umeme nyumbani mwako,baada ya kuambiwa wewe ndiye mwenyewe, sasa kichwa chini miguu juu gafla anatokea mwanaume mwenzio anaingia nyumbani mwako wewe unatoka na mtu huyo anaiambia familia yako eti yeye ndiye aliyeweka huo umeme nyumbani humo, Mh! makubwa haya F.waacheni tu wanafamilia wageuze magazeti maana ndo fashion siku hizi.

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU