NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Friday, February 11, 2011

PESA ZA RADA HAKUNA - SERIKALI


Hivi kale ka-rada ketu ka bei mbaya vipi? 
Hakatutoshi, kemaharibika, hatujui kukatumia au kana matumizi mengine? Au kwa vile ni ka jeshi basi hakafai kwa matumizi ya raia kama kututabiria hali ya hewa?

*****************

Fedha za rada hakuna
 Na Halima Mlacha
(10/2/2011)

SERIKALI imekiri kuwa haina fedha za kutosha kwa ajili ya kununulia rada zinazohitajika nchini kwa ajili ya utabiri wa hali ya hewa.

Hayo yamesemwa bungeni na Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk. Athumani Mfutakamba wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalumu, Mkiwa Kimwaga aliyetaka kujua hatua ambayo serikali inachukua dhidi ya ununuzi wa rada moja wakati zinahitajika saba.

Akijibu swali hilo, alikiri kuwa ni kweli kwa mujibu wa mahitaji ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ili ifanye kazi zake kwa ufasaha zaidi inahjitaji rada saba.

Hata hivyo, alisema kutokana na ufinyu wa bajeti ya Serikali imeweza kufunga rada moja Dar es Salaam na sasa iko kwenye mchakato wa kufunga rada ya pili mkoani Mwanza ili kuiongezea nguvu ya kwanza.

“Hata hivyo, tunajitahidi kuzungumza na wahisani kuona kama watatusaidia katika hili lakini
uwezo wa kufunga rada saba zinazohitajika hatuna ila tunajitahidi,” alisema Dk. Mfutakamba.

Alisema ili mamlaka hiyo kupata wataalamu waliobobea, Serikali itaendelea kuwajengea uwezo katika kutoa utabiri wa hali ya hewa na kwa tahadhari zaidi.

Pamoja na hayo, Serikali itaimarisha Chuo cha Hali ya Hewa kilichopo Kigoma, kinachotoa elimu katika fani ya hali ya hewa kwa kukiongezea fedha na kuboresha miundombinu ya chuo hicho.
Chanzo: Habari Leo

No comments:

Post a Comment

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU