NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Tuesday, February 22, 2011

PROFESA MBELE KANIACHA HOI

 • Kama vile alivyoachwa hoi na mwanafunzi wake mwenye moyo wa shukrani, Profesa Mbele pia ameniacha hoi kwa wema, ukarimu na moyo wake wa kujali. Kama wiki mbili hivi zilizopita nilikuta bahasha kubwa ofisini. Muhuri wa posta ulionyesha kuwa ilikuwa imetoka Minnessota na mtumaji alikuwa ameingia gharama ya karibu dola nane kununulia stempu.
 • Nilipoifungua bahasha ile nilishangaa sana kukuta kwamba ilikuwa imetoka kwa Profesa Mbele na ndanimwe mlikuwa na nakala ya kile kitabu chake mashuhuri cha Africans and Americans: Embracing Cultural Differences -tena ikiwa imesainiwa kabisa! Kwa mwanataaluma makini na anayependa vitabu na kujiongezea maarifa kila kuchapo kama Profesa Mbele, hii ni zawadi ya muhimu sana!!!
  • Nimeamua kukisoma kitabu kwa uangalifu sana ili nigundue sababu inayokifanya kipendwe sana na watu wanaopenda kujifunza utangamano wa kitamaduni. Nikishafanya hivyo, nitaandika maoni mafupi hapa kukihusu.
  • Kwa moyo wangu wote, napenda kutoa shukrani za dhati kwa Profesa Mbele kwa wema wake huu. Kwa hakika azima na shauku yake isiyoisha ya kutuhamasisha kusoma vitabu si bure. Kama vile ambavyo nimeshawahi kusema HAPA, mawazo na falsafa zake  kombozi siku moja zitawapambazukia waTanzania na mchango wake chanya usiotetereka katika ukombozi wa jamii yetu utajulikana na kuheshimiwa!
  Kitabu hiki mashuhuri kinapatikana mtandaoni HAPA.
  Kule Tanzania kinapatikana sehemu mbalimbali (bofya HAPA)

  5 comments:

  1. Jamaa nguli huyu!

   Nazimia mambo zake sana tu!

   ReplyDelete
  2. Hongera Prof.Mbele, tunaomba pia uendeleze mkakati wa kuwahamasisha watanzania tupende kujisomea, hili litafanikiwa tu endapo wahamasishwaji hao watakua watoto ili wakue na utamaduni huo. Nilipata shida sana nilipokuja hapa Tokyo miaka mitatu iliyopita, nilikuwa nashangaa ninapoingia kwenye treni nakuta wazee,vijana na watu wote wameinamia vitabu wanasoma, mimi nilijiunga na wale walikuwa wamechoka kwa kazi nyingi wanazofanya ofisini kwao hawa ni wachache wale wanaosinzia. Niliendelea hivyo baadae nikajiuliza maswali hivi hawa watu wanasoma nini kilasiku wamekodolea macho vitabu vyao,hata kama mtu kasimama anaendelea tu kusoma. Kweli nimeamua kujifunza na mimi sasa naweza kujisomea bila kupoteza muda wowote,kumbe inawezekana kubadilika. Nimegundua tunaachwa nyuma kwasababu hatutaki kujisomea, nyumbani ukimuona mtu anajisomea labda gzt la udaku au ni mwanafunzi yupo karibu na mitihani,au wachache wa group lenu. Prof.Mbele, Kaka Matondo na wengine wenye muelekeo kama wenu tusaidieni kubadilisha kizazi chetu kipende kujisomea,hakika tumeachwa mbali.
   Inaelekea Kitabu hicho ni kizuri, Mungu akinijalia nitakitafuta na kukisoma.

   ReplyDelete
  3. Mtakatifu - kweli tupu!

   Kamala - nadhani Profesa ameshaiona anuani yako (666 Bukoba). Asante kwa kurudi tena katika kublogu baada ya kututisha eti ulikuwa unafunga kijiwe!

   Anony - Asante sana kwa maoni yako ya kina kuhusu hili suala la kujisomea. Polepole tu tutabadilika hasa tukishatambua ni nini hasa kinachotufanya tuwe wazembe wa kujisomea. Kumbuka kwamba hata katika vyuo vikuu watoto wetu wanapenda zaidi "madesa" na vitabu vya miongozo kama vile vya Nyambari Nyangwine.

   Kitabu hicho kinapatikana mtandaoni na kwa vile uko Japan, bila shaka unaweza kukiagiza. Unaweza pia kuwasiliana na Profesa Mbele kupitia: africonexion@gmail.com

   ReplyDelete
  4. Pongezi kwa Profesa Mbele, waswahili walisema kutoa ni moyo wala si utajiri, japo hali na mfumo wa maisha ya sasa hivi unafanya watu kuwa wagumu kutoa bure. Zamani ukienda kumsalimia jirani unarudi nyumbani na zawadi ya kuku lakini hali haiko hivyo tena.

   Pili,ni changamoto na mtihani kwa mtu kuzawadiwa kitabu, lakini sina shaka na aliyezawadiwa kwani ni mwelimishaji mkuu na nadhani Profesa Mbele alifanya makusudi kutimiza hiyo azma.

   ReplyDelete

  JIANDIKISHE HAPA

  Enter your email address:

  Delivered by FeedBurner

  VITAMBULISHO VYETU