NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Thursday, February 17, 2011

RAIS WA JAMHURI AZUNGUMZIA MIRIPUKO YA MABOMU GONGO LA MBOTO (VIDEO)Video kwa hisani ya Abdallah Mrisho wa Global Publishers.

Kwa picha na habari kutoka vyanzo mbalimbali kuhusu tukio hili la kusikitisha tembelea HAPA HAPA, HAPA (kuna maoni 99 tayari) na HAPA. Hotuba kamili ya rais katika maandishi inapatikana HAPA.

Kwa waathirika wote, poleni sana kwa msiba huu. Hebu Muumba na Akawatie nguvu katika saa yenu hii ya giza. 

Mungu Ibariki Tanzania !!!

8 comments:

 1. Poleni sana ndugu wote mliopatwa na mkasa huu, kwani inaonyesha kabisa kwamba kwasasa jiji la Dar es Salaam si salama kabisa kuishi, kwa jinsi inavyoonyesha nadhani haya madude yaliwekwa zamani tangu nyerere alivyokuwa kijana. kwasababu hatujui kuwa ni gala gani lingine litakalofuatia kulipuka, Ilianza Mbagala tukaambiwa haitatokea tena lakini baadae mabomu mengine yaliendelea kupasuka na kuua watu, sasa hivi Gongo la mboto, hatujui baada ya Gongo la mboto labda ni lugalo, Lugalo nako si kuna kambi ya Jeshi siajabu yapo yaliyokwisha iva yanasubiri muda wa kuua watu, Upanga , Changanyikeni , makuburi , Kunduchi, na sehemu zingine zote za Tanzania ambazo zipo karibu na kambi za jeshi maana yake wakae mkao wa kula, muda na siku haijulikani, ni lazima tufikirie hivi maana sasa inatisha
  kweli inasikitisha sana,tunakuwa wakimbizi ktk nchi yetu wenyewe. Yawezekana ni bahati mbaya lakini je kwani hii ni mara ya kwanza kutokea? na kama ni kuhamisha wananchi waliokaribu na kambi za jeshi mbona ni wengi sana, Tanzania nzima nyumba nyingi za raia zipo karibu sana na jeshi, je wote hao watapelekwa wapi, mbaya zaidi ni kwamba hii midude ikilipuka inaruka mbali zaidi si pale tu kwenye eneo husika. Mfano pale upanga ;hatuombei itokee; pale mambo yakiiva inamaana hadi ikulu adhari zitafika, Hivyo basi mi nadhani hili ni janga kubwa sana kwa watanzania wote, na kama lisipotafutiwa ufumbuzi wa haraka, basi tusubirie chain hii iendelee kufanya maafa mengine, maana Jiji la Dar limezungukwa na kambi za jeshi.
  Mungu Ibariki Tanzania.

  ReplyDelete
 2. Ama kweli hii ni kasheshe.

  ReplyDelete
 3. Kweli hatuna rais bali bomu. Lugha anayotumia na sura anayoonyesha vinamsuta. Busara imekwenda wapi?
  Mbagala haikutoa somo na hakika hakutatokea somo hadi watu waende Tahrir.

  ReplyDelete
 4. Hakuna mabomu ni redio mbao, huku watu wanakufa. Hivi kuna redio mbao ktk uhai wa mtu.

  ReplyDelete
 5. Waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa pamoja na mkuu wa majeshi wanayo kila sababu ya kuwajibika na matukioo haya ya kujirudia. Kauli ya raisi ya REDIO mbao ni ya kujilinda (defensive mechanism) na ni ya kiswahili mno.

  Nimategemeo yangu kuwa baada ya msiba huu wa kitaifa, watanzania na hasa wana-Dar es salaam watatumbua umuhimu wa maandano ya kushinikiza kujiuzulu kwa viongozi husika katika wizara ya ulinzi.

  ReplyDelete
 6. Mnafikiri ni nani wa kujiuzuru hapo, wakati wahusika ni watoto wa maraisi. Ukiwa masikini huna haki

  ReplyDelete
 7. Inasemekana hakukuwa na mwanajeshi yoyote aliyejeruhiwa, je walijua kuwa mabomu yatalipuka? maana saambili usiku ni mapema sana,inamaana waligundua mapema wakakimbia au?kama kweli walijua kwanini wasiwatangazie wananchi wakimbie badala yake wameokoa roho zao na familia zao tu, hakika jambo hili mashwali ni mengi kuliko majibu.

  ReplyDelete
 8. Tukio kama hili KAMWE halipaswi kujirudia tena, period! Na ni lazima jeshi lifanye kila liwezalo kuhakikisha kwamba halijirudii tena kabisa kabisa!!!

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU