NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Thursday, February 3, 2011

SAFARI ZAIDI YA MILIONI 10. ABIRIA ZAIDI YA MILIONI 700 WAMESAFIRISHWA. HAKUNA HATA ABIRIA MMOJA ALIYEPOTEZA MAISHA !!!

Picha hii iko HAPA.
 • Ni mwaka uliopita (2010). Nchi ni Marekani. Ni usafiri wa anga. Hali ilikuwa ni ile ile kwa miaka ya 2006, 2007 na 2008.
 • Kwa watu wanaoogopa kusafiri kwa ndege (kama mimi hapo zamani kidogo) hizi ni habari njema kwani ni uthibitisho kwamba pengine usafiri wa ndege, japo unaogopwa sana, ndiyo salama kuliko usafiri mwingine wo wote. Wewe unasemaje? Unaogopa kusafiri kwa ndege? Vipi, ukipanda Precision au Air Tanzania?  Moyo unakuenda mbio? Mungu Akubariki katika safari yako (ya anga!).
Hata hivyo tazama HAPA...

  6 comments:

  1. Yaani hata hapa nilipo niko hoi kwa 'phobia' ya kukwea pipa!

   Aksante kwa kunifariji japo ni ngumu!

   ReplyDelete
  2. Sijui kwanini mimi sijawahi kuogopa sana ndege!


   Ila kuendesha gari mahali kama Dar-es Salam , hilo ni swala jingine kwa maana kila wakati nahisi ntagongwa au kugonga!:-(

   ReplyDelete
  3. Nimesikia hivyo kuwa usafiri salama ni wa ndege, halafu meli na inafuatia treni, na usafiri hatari ni wa magari..!

   ReplyDelete
  4. Kweli kaka, usafiri wa ndege ni salama salama sana. Kwakweli sina jinsi tu ila gari naogopa sana hasa ukiangalia huku kwenye highways magari yanavyokwenda kasi na kubadili lanes kama mchezo vile. Pindi kikitokea kigugumizi basi huwa balaa tupu. Mungu na atujalie na kutulinda!!

   ReplyDelete
  5. kuna wengine uoga wa kukwea 'pipa' unaisha tu wakati wa 'touch down'. hongera zao waliufanya usafiri huu uwe madhubuti na salama.

   ReplyDelete
  6. Ng'wanambiti - hata watu wa utambuzi kama wewe mnaogopa kifo? Nilikuwa nafikiri nyie hata kama ndege inaporomoka basi ndiyo mnaanza ku-meditate!

   Mtakatifu - kuendesha Dar ni kimbembe. Nilishajaribu nikakoswakoswa pale mataa ya Morocco. We acha tu. Nakubali kabisa kwamba kuendesha Dar ni shughuli pevu na si mchezo. Inahitaji uzoefu. Ni lazima ujifunze kupiga honi, kufoka + kumwaga matusi na kuwa ngangari hasa bila kusahau kitu kidogo cha wenyewe wenye barabara!

   Emu-three: Data hizi ni uthibitisho wa kauli yako. Magari ndiyo yanaongoza kwa kuua watu.

   Mfalme: Nenda California ukaone mambo. Jamaa kule hawana subira kabisa na mambo yanayofanyika kwenye ma-free way huko kama umezoea kuendesha katika sehemu kama hapa Florida ambako inasemekana kuna wazee wengi na wana tabia ya kwenda pole pole, California itakuwa kazi.

   Mwaipopo: Huu ni mmojawapo wa ugunduzi wa kushangaza sana. Ukipanda Boeing 747 iliyosheheni sawasawa halafu ikatulia angani kwa masaa zaidi ya kumi na kutua salama basi ni lazima ushangae jamaa waliyoitengeneza.

   Asanteni nyote!

   ReplyDelete

  JIANDIKISHE HAPA

  Enter your email address:

  Delivered by FeedBurner

  VITAMBULISHO VYETU