NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Tuesday, February 1, 2011

UANASIASA: KAZI INAYOPENDWA SANA JAPO HAINA "SHUKRANI" !!!

  • Hata Plato aliilalamikia kazi hii huku akidai kwamba ni kazi ngumu na isiyofaa kwa kila mtu. Kama alivyonukuliwa na Mwalimu Nyerere, Myunani huyu wa kale anayetambuliwa na wengi kama baba wa Falsafa "alipendekeza kuwa mafilosofa ndio wanaofaa kuwa watawala wa nchi, maana wana sifa mbili muhimu: kwanza wana uwezo wa kutawala, na pili hawapendi kutawala. Kwa hiyo Jamhuri ya Plato itakuwa na sheria ya kuwalazimisha mafilosofa kutawala kwa zamu; na mtu zamu yake ya kutawala ikiisha, atafurahi sana kurudia shughuli zake za falsafa ambazo ndizo hasa anazozipenda." (Uongozi wetu na Hatima ya Tanzania, uk. 8)
  • Kimsingi duniani kote uanasiasa ni kazi isiyo na shukrani (tazama picha hapa chini), na mimi nadhani kwamba pengine hii ndiyo kazi ngumu kuliko zote hasa kwa watu wanaopenda faragha, uadilifu, maisha yasiyo na mikikimikiki na wenye lengo la kweli la kuleta mabadiliko chanya katika watu wanaowaongoza au kuwawakilisha.
  • Pamoja na "ubaya" na matatizo yote yanayoambatana na kazi hii, inashangaza kidogo kuona kwamba pengine ndiyo kazi inayokimbiliwa sana na wasomi na wanajamii wengi huku kila mmoja akiahidi kwamba anafanya hivyo kwa maslahi ya wanajamii. Sote tunajua kwamba huu ni uwongo, na wengi wao wanafanya hivi ili kushibisha matumbo yao tu. 
  • Kinachofurahisha kwa sasa ni kuona kwamba kote Afrika watawaliwa wameanza kuamka na sasa wanahoji baadhi ya matendo ya watawala wao na kuyapinga waziwazi. Hawataki tena kuDowanishwa na kuendelea kusikinishwa na wanasiasa wao ambao, kwa kutumia maneno ya Mwalimu Nyerere, "wanapenda sana kutawala, hata kama hawana uwezo wa kutawala". Na hili ni jambo jema!!!
  •  Bofya HAPA ili kutazama picha zaidi juu ya "vijembe" mbalimbali dhidi ya wanasiasa!

No comments:

Post a Comment

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU