NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Monday, February 14, 2011

VALENTINE DAY, MASHINDANO YA UREMBO, NOECLEXIS NA DHANA YA UZURI.

Angalizo: Hii ilitoka mwaka jana. Nimeongezea na kupunguza vitu vichache ili kuashiria mabadiliko ambayo yamekwishatokea tangu wakati huo. Maswali ya msingi, hata hivyo, bado ni yale yale. Tuwemo!
********************


 • Leo hii dunia inasherehekea sikukuu ya "kipagani" ya Valentine Day. Kwetu sisi Afrika nadhani siku hii bado ina ugeni fulani. Kwa mfano, wakati nikisoma pale mlimani miaka michache tu iliyopita,, sikumbuki kuona watu wakihangaika kusherehekea hii Valentine Day. Mambo yamebadilika kwa kasi mno na siku hii sasa ni muhimu kwa wapendanao kusherehekea kwa kwenda pwani, kwenye kumbi za starehe na kwingineko. Mwaka jana, kwa mfano, blogu kadhaa ziliwaonya na kuwakumbusha washerehekeaji wa sikukuu hii juu ya hatari ya kuambukizana gonjwa la UKIMWI. Hii imegeuka na kuwa siku ya kungonoka! (Tazama maoni ya wadau HAPA)
 • Siku hii ya wapendanao na mashindano ya urembo tunayoyashuhudia kila leo (vyote ni matokeo ya utandawazi) vimenikumbusha swali gumu ambalo limewasumbua wanafalsafa tangu enzi na enzi: Uzuri ni nini? Hili ni swali linalohusu kila kitu hapa duniani lakini leo nitatumia mifano ya washiriki wa mashindano ya urembo yaani mabinti.
 • Ni kweli kuna wazuri/warembo au pengine uzuri/urembo umo katika fikra za mtazamaji tu? Inakuwaje leo tunalazimishana kuwa na mrembo mmoja tu tena mwenye sifa zile zile za Kimagharibi- tineja, mkondefu, mrefu, mwenye miguu mchongoko na tumbo tambarare, mwenye madaha, nyanya msumari kifuani na ikiwezekana "aliyepigwa pasi"? Hebu chunguza picha hizi kwa makini halafu ufikiri tena dhana hii ya uzuri/urembo:
(1) Tunalazimishana kuamini kwamba eti mrembo ni lazima awe hivi:

 
(2) Huu ni uwongo kwa sababu katika jamii zingine za Kiafrika mrembo alitakiwa/anatakiwa awe hivi:(3) Na katika jamii zingine mrembo alitakiwa/anatakiwa apambike hivi:

(4) Kwa wengine, mrembo ni lazima awe amenona kama hivi. Na kwa mwanamke wa Kiafrika, kunona hivi lilikuwa ni jambo jema!


(5) Au awe na umbo namba 8 kama hili:


(7) Wengine huwa hawajali umbo ali mradi kuwe na "kitu" wakipendacho!


(8) NOECLEXIS - Waswahili walipatia waliposema kwamba "mwanamke tabia"! Msikilize Dudubaya hapa chini akitetea Noeclexis!(9) Swali: mbona tunalazimishana kwamba eti mrembo ni lazima awe hivi?


 • Na kama kila mtu ana dhana yake ya uzuri kama tulivyoona hapo juu, inawezekanaje tuwe na mzuri mmoja tu anayewakilisha dhana zote hizi? Ati, uzuri hasa ni nini? 
 • Kwangu mimi, mwanamke mzuri, mwandani mwema, rafiki wa kweli, shujaa wa moyo wangu, malkia wa dunia, Eva wangu na mshindi mwema ni HUYU (Tazama pia HAPA). Nina sababu nyingi; na nyingi hazihusishi umbile wala uzuri wa nje. Valentine njema wadau mnaposherehekea "uzuri" uliotamalaki katika kila kitu hapa duniani! Na vita vya UKIMWI ni lazima viendelee ati!

  4 comments:

  1. Ndiyo maana si vizuri kuwacheka wapendanao kwani hujui kwa nini wamependana. Kila mtu anapenda vitu tofauti and it does not make any sense eti kuwa mrembo you have to be slim and skiny kama wazungu wanavotaka.

   Na watoto wetu wanajikondesha sana ili waonekana warembo. Upuuzi mtupu and you can be beautiful katika umbo lolote ali mradi tu uwe healthy.

   Tuacheni kuiga mambo kupita kiasi. Tunaonekana wapumbavu.

   ReplyDelete
  2. Lazima tuwe modern bwana. The beautiful woman siku hizi must be skiny. Unene na hayo matako makubwa yalishapitwa na wakati. After all it is not healthy kuwa mnene namna hiyo.

   Love the vimobitel and always will.

   ReplyDelete
  3. Tatizo ni kwamba wanaume ndo wanapenda vimobitel nasi wanawake inabidi tufanye kile ambacho wanaume wanapenda. Nakumbuka miaka ya nyumba nilikuwa na rafiki ambaye yeye alipenda kuwa na mwanamke mnene nami ilibidi kujithidi na kula ili niweze kuwa kama anavyotaka, kwa hilo alinipenda mno.

   Wembamba tu bila mpangilio si mzuri wenzetu, wanauita skinny, kinatochatakiwa ni kuwa slim. Kwa upande wangu japokuwa mimi ni mwanamke namba tano hapo juu ndo ideal kwa mwanamke kwa mtizamo wangu mimi, Makalio, hips zikizidi zinachusha hakuna ulingano na miguu, miguu inakuwa imebeba limwili likubwa kupita maelezo. Lakini mara nyingine wengine huwa ni kama ugonjwa nyama (tumours) kuota kwa wingi bila mpangilio.
   Ila kikingine kinachosumbua ni matumbo kwetu akina mama mara baada ya kujifungua maumbo hubadilika na usipokuwa makini basi hata hutaeleweka kiuno kiko wapi au mara nyingine hueleweki kama unakwenda mbele ama unarudi nyuma. Mazoezi na taratibu za ulaji ni muhimu

   ReplyDelete

  JIANDIKISHE HAPA

  Enter your email address:

  Delivered by FeedBurner

  VITAMBULISHO VYETU