NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Friday, February 4, 2011

"VIONGOZI WETU, NYINYI MLISOMA KATIKA MAZINGIRA KAMA HAYA ?" WASOMI WA MLIMANI WANAULIZA.

Ni swali linaloulizwa na waandamanaji hawa wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam leo walipojaribu kuandamana kwenda kumwona "Mtoto wa Mkulima" kuwasilisha madai yao ya kuongezewa posho ya kujikimu kutoka 5,000 mpaka 10,000 kwa siku. 


Maandamano ya vijana hawa hata hivyo hayakufika popote kwani walipofika Savei walikutana uso kwa uso na walinzi wa mfumo.

Migomo hii ya kila siku katika vyuo vyetu inaakisi nini kuhusu mfumo wetu wa elimu na "wasomi" wetu hawa? Hatuwezi kweli kutafuta suluhisho la kudumu kuhusu migomo hii ya kila leo miaka nenda miaka rudi katika vyuo vyetu? Kwa picha zaidi, tembelea HAPA.

Kwa habari zaidi soma makala ya gazeti la mwananchi HAPA.

5 comments:

 1. Jamani mimi nakwazika sana na hizo nguvu za jeshi,kwani wakiwaacha na kuwalinda ili wafikishe ujumbe wao itakuwaje?Mwananchi hana uhuru wowote katika nchi yake?au wanahamu ya kutumia hivyo vifaa hawana pakuvitumia?jeshi badala ya kutulinda sasa linatuumiza,kweli tutafika hivi jamani?MUNGU IBARIKI AFRIKA,MUNGU IBARIKI TANZANI!!!!.

  ReplyDelete
 2. Acheni kutusumbua wakati tuko bize tunapanga kujengea nyumba WABUNGE!


  Sasa nyie niniiii! Usumbufu tu !:-(

  ReplyDelete
 3. 'Hawa watoto bwana, sisi tunakuna kichwa jinsi ya kurudisha madeni ya kampeni, kubadilisha magari, haya yamepitwa na wakati, na...ile nyumba ndogo inadai nyumba ya kisasa, na...ooh, wapigeni mabomu watulie darasani, watu badala ya kusoma mnasumbua watu....'

  ReplyDelete
 4. Nchi masiniki kama vile haina viongozi. Priority zao ziko kwenye ufisadi. Sasa wanataka kujenga majumba ya wabunge kule Dodoma. Hii itakula mabilioni ya shilingi na cha ajabu ni kwamba hata hao wabunge wenyewe hawatakaa huko Dodoma. Ni watu hawa hawa ambao wamekazania kuilipa Dowans wakati mfumo wa elimu ukiteketea.

  Wengi walikopa mabilioni kukodisha helikopita za kufanyia kampeni na sasa inabidi wazirudishe. Mashangingi mapya ya milioni 400 wameshagawana duh. Nchi hii inakwenda wapi lakini?

  I swear hakuna mtoto wa Lowassa katika kundi hili linalopigwa mabomu. Watoto wao wako wanasoma kwenye vyuo vya kimataifa nje ya nchi. Inavyoonekana wanataka kujenga permanent class of walala hoi. Hii ni hatari sana na siku moja itawatokea puani kwani ipo siku hawa masikini wataamka tu!

  Hakuna wakati ambapo kumekuwa na VACUUM (OMBWE) ya uongozi katika nchi yetu kama wakati huu. Hata wakati wa Mzee Rukhsa kumbe kulikuwa na unafuu!!! Mungu Atusaidia jamani.

  Na wewe mwenye blogu usibanie comment hii. Sijatukana mtu. Ni raia tu ninayetoa maoni yangu kuhusu na mwendo wa kutisha wa nchi yangu, nchi ambayo haina mwelekeo kabisa...Nina huzuni na uchungu sana na niko tayari kufanya lolote ili kurekebisha hali hii.

  ReplyDelete
 5. hahhaahhha ooohhhhhh Nana wewe mwenye blogu usibanie hii comment!!!!!!!!!!pole mwanakwetu umewaza kwa sauti na kupunguza uchungu wako moyoni!

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU