NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Tuesday, February 15, 2011

WABUNGE WAZOA MILIONI 90 KILA MMOJA. NI ZA KUNUNULIA MAGARI !!!

 • Hivi mbunge ukimaliza muda wako, hilo shangingi lako unakwenda nalo au unalirudisha? Kwa wabunge waliorudi, mbona wasiendelee kutumia mashangingi yao ya zamani hasa ukizingatia kwamba Toyota Land Cruisers ni magari yanayodumu kwa muda mrefu sana? Mimi sizijui taratibu za hawa "waheshimiwa" na samahani kama haya ni maswali "ya kitoto" Inashangaza kidogo kuona kwamba kila tukibadilisha wabunge ni lazima tuingie hizi gharama za kununua mashangingi mapya.
Hizi ni za 2009
 ************************

Wabunge wazoa Sh. 90 Mil kila mmoja
Tuesday, 15 February 2011 07:35 

JUMLA ya Sh. 3.24 bilioni zimelipwa kwa wabunge ili kuwawezesha kununua magari binafsi kwa ajili ya shughuli za kibunge, imeelezwa.

Kwa mujibu wa habari hizo kila mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amelipwa Sh. 90milioni  kwa ajili ya kujinunulia gari.

Aidha, wabunge hao wapatao 360 wamekatiwa bima ya afya inayotarajiwa kuanza kutumika kabla ya mwezi Juni mwaka huu. Na wameomba kutibiwa hospitali za binafsi!

 Halafu Chadema nao wakaingia....

"Ndugu zangu hali ni mbaya, siku moja tutafanya maandamano bungeni, sio kutoka nje ya ukumbi. Inashangaza, tumepewa Sh90 milioni za magari kwa wabunge wote, huku bungeni tunajadili bajaji kuwa 'ambulance' (gari ya kubebea wagonjwa),'" alisema mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema.


"..Wabunge tumeomba 'insurance' (Bima) kila mmoja amepewa na kabla ya Juni naamini zitaanza kutumika, tumeomba kutibiwa 'private hospital' (hospitali binafsi). Hii inaonyesha hospitali za serikali zilivyo mbaya na hao wenye uwezo wanazikimbia," alisema Lema.
 Isome habari kamili HAPA.

6 comments:

 1. Hawa Chadema - mbali na ukabila, udini na upumbavu mwingine na unafiki kweli wanashangaza. Sasa kama kweli wana uchungu mbona wasikatae hizi milioni 90 za bure na Watanzania tukawaelewa. Huu ni unafiki wa hali ya juu. It is only a matter of time kabla watanzania hawajawaelewa hasa who they are. Hypocrites !!!

  ReplyDelete
 2. Kwa jinsi tunavyowategemea wabunge kuweza kutembelea sehemu mbali mbali za jimbo lao, kuwepo kwenye mikutano, kushiriki shughuli huko na huko, ni lazima wawe na magari. Tunaweza kujadiliana ni magari ya aina gani, lakini ni wazi kuwa tutawaona hawafai iwapo hawaonekani kwenye maeneo wanakohitajika kwa muda unaotakiwa. Ingawa wakati huu niko ughaibuni, mimi ni raia wa jimbo la Ubungo, na ninatembelea dala dala au bajaji. Sielewi mbunge wangu atawezaje kufanya kazi vizuri katika jimbo la ubungo iwapo atategemea dala dala au bajaji.

  Afadhani hapo Ubungo kuna hizi dala dala na bajaji. Je majimbo ya huko vijijini. Mbunge ataweza kweli kutimiza majukumu yake bila gari?

  ReplyDelete
 3. Angalizo zuri Profesa Mbele. Ni kweli wanahitaji magari tena ya kweli kweli hasa ukizingatia hali ya barabara zetu hasa zile za vijijini. Na kusema kweli sina ugomvi na mashangingi. Wasiwasi wangu ni huu utaratibu wa kuwa tunanunua mashangingi mapya 360 kwa gharama ya 90,000,000 kila baada ya miaka mitano. Kama haya ni magari ya kiofisi, haiwezekani yakaendelea kutumiwa hata baada ya hicho kipindi cha miaka mitano - angalau kwa wabunge wanaorudi bungeni? Na kwa vile wanapewa pia posho ya matunzo ya magari haya naamini baada ya miaka mitano yanakuwa bado katika hali nzuri sana. Kama nilivyosema hapo juu, sizielewi taratibu. Pengine ukishanunuliwa hii shangingi basi ni la kwako na baada miaka mitano tena ni lazima upate jingine.

  Kwa anony. wa kwanza. Nawe umesema ninalokukera na umesikika. Ungetegemea Chadema wafanye nini kuhusiana na jambo hili? Wagome kuchukua hizo milioni 90 au? Toa mapendekezo yako sahili mbali na kuhemka tu kama ulivyofanya hapo juu.

  Pengine kutatizwa kwangu kumetokana na kutoelewa baadhi ya mambo katika habari hii mf:

  "..magari binafsi kwa ajili ya shughuli za kibunge" ni magari ya ofisini au? Je, hii ni tofauti na mashangingi yao ya ofisini? Ina maana unapewa hizi 90,000,000 na unanunua gari unalotaka mwenyewe ama? Nilifikiri kwamba serikali ndiyo ilikuwa inaagiza haya magari na kuwagawia wabunge! Mnaofahamu kuhusu taratibu hizi mtujulishe jamani.

  ReplyDelete
 4. Wewe any.wa kwanza, mi nadhani wewe umelewa bila kutumia kilevi, ni bora kama huna comment ukae kimya kuliko kuropoka mambo ambayo huna uhakika nayo.

  ReplyDelete
 5. True anony. wa kwanza. I salute you kwa kuliona hili. Chadema ni chama cha mazuzu na malimbukeni tu!!!!

  ReplyDelete
 6. Nyie anony. acheni chuki zenu na Chadema. Inashangaza mnawashambulia wabunge wa chadema tu pekee yao. Binafsi naunga mkono mawazo ya Profesa Mbele na Matondo.

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU