NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Tuesday, February 8, 2011

WALIMU SASA KUAJIRIWA MOJA KWA MOJA - SERIKALI


Walimu sasa kuajiriwa moja kwa moja
8/2/2011
Na Stella Aron, jijini

SERIKALI imesema kuanzia sasa walimu nchini wataajiriwa na kupangiwa moja kwa moja vituo vya kazi bila kufanya usaili ama kucheleweshwa.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwenye vyombo vya habari na kusainiwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Phillemon Luhanjo, kuwa walimu hao wataajiriwa endapo watakuwa wameshinda mitihani yao.

Taarifa hiyo inasema Serikali imeamua kufanya hivyo kwa kuzingatia uhaba wa walimu kama ulivyo uhaba wa madaktari nchini na kwa nia ya kupanua na kuboresha kiwango cha huduma ya elimu.

Imesema uamuzi wa Serikali ulifikiwa katika kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika Februari 3, mwaka huu jijini chini ya uenyekiti wa Rais Jakaya Kikwete.

Katika kutekeleza uamuzi huo, Serikali imeamuliwa kuwa walimu watapangiwa vituo vya kazi katika miezi ya mwisho ya mafunzo yao ili kuwawezesha kuripoti moja kwa kwenye vituo vyao vya kazi baada ya kumaliza masomo na mafunzo yao.

Amesema mara baada ya walimu hao kumaliza wataajiriwa na kupangiwa moja kwa moja vituo vya kazi bila kufanya usaili ama kucheleweshwa na michakato na taratibu nyingine za kirasimu.

CHANZO: Dar Leo

1 comment:

  1. Zamani ndivyo ilivyokuwa lakini baada ya wanasiasa kuivamia kada ya elimu mambo yakaenda kombo.

    ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU