NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Friday, February 18, 2011

WITO KWA WACHAGA: KISOMENI KITABU HIKI !!!

 Ganda la mbele
 • Baada ya kuona kuwa Wachaga wamebaki jina tu kwa wengi wao kutoifahamu lugha wala utamaduni wao, leo napenda kuwaletea habari nzuri juu ya kitabu kinachoelezea maisha na utamaduni wa Mchaga kwa undani. Kitabu hiki kiitwacho Maisha ya Mchagga Duniani na Ahera kimeandikwa (kwa Kiswahili) na Mangi Petro Itosi Marealle na kuchapishwa na Mkuki na Nyota Publishers 
Ganda la nyuma
 • Nilikiona maktabani na mara moja nikakiazima na kuanza kukisoma (mimi ni Kyasaka niliyeoa binti wa Kichaga!). Ni kitabu kizuri ambacho kinaelezea mambo ya kina kuhusu maisha ya Mchaga tangu anapozaliwa mpaka anapofariki na baada ya hapo.
Tabaruku


Yaliyomo

 • Hata kuna sura nzima juu ya Uchawi na Jinsi ya Kuroga. Kutokana na kiwango chao cha elimu, sikujua kama Wachaga nao wanaamini sana katika mambo ya ushirikina mpaka nilipoisona sura hii. 
 • Ingependeza sana kama vitabu vingi vyenye kuelezea tamaduni mbalimbali za makabila yetu vingeandikwa kwani tutake tusitake lugha na tamaduni zetu nyingi zinaonekana kutishwa na wimbi la utandawazi na mabadiliko ya maisha ya kisasa.
 • Na kwa wavulana na wasichana wa Kichaga - na kama tabaruku ya kitabu hiki inavyosema - Mambo Makuu Zaidi Yanatarajiwa Kutoka Kwenu !!!
Nyongeza Chekeshi
 • Mbali na "ukweli" kwamba mimi ni Kyasaka, jina langu pia huwa linawatatanisha Wachaga kwani katika Kichaga neno Matondo si neno zuri sana. Napenda tu kuwahakikishia kwamba mimi SIYO Itondo na binti yenu kabisa hajafanya makosa kuolewa na chasaka! Na kwa mnaotegemea kuoa mabinti wa Kichaga, hakikisheni mnasoma HAPA kwanza. 
*******************
Kuhusu Upatikanaji wa kitabu hiki kutoka Mkuki na Nyota Publishers

Kitabu hiki kinapatikana kutoka Tanzania Publishing House Bookshop, Samora Avenue, Dar es salaam. Habari kuhusu kukinunua kutoka mtandaoni zitapatikana hivi karibuni !

12 comments:

 1. Asante sana kwa kutangaza kitabu kama hicho. Kwa kweli, tungekuwa sisi Waafrika tunavisoma kwa makini vitabu vya aina hii (isiwe tu 'kusomwa labda na Wachagga pekee yao kwani ni kitabu kuhusu Wachagga') lakini visomwe na kila Mwafrika anayependa Bara lake, tungekuwa mbali sasa ki utamaduni wetu na maelewano kama Waafrika kwa Waafrika.


  Mimi na amini hata vita vya Waafrika wenyewe kwa wenyewe tungekuwa mbali sana navyo.


  Bahati mbaya elimu tuliyepewa pitia mfumo wa Nchi za Magharibi (WESTERN EDUCATION) mara nyingi inamatokeo ya kutufanya tuwe tunadharau vitabu kama hicho, eti: "Mimi mwananchi, Bwana, Mwanamapinduzi na Mtoto waKitaifa...nayafatafata nini mambo haya ya kikabila na vitabu vyake?"


  Kama Manyanya ningependekeza kwamba Watanzania wote kitabu hicho wasome. Vilevile wasomi wafanye tafsiri yake katika lugha ya Kiingereza, Kireno au Kifransa vilevile ila sote Waafrika Barani tumwelewe Mchagga, Mxhosa, Mzulu, Mkurya, Mswati (Swaziland) au kabila lolote lile Barani ambalo linaweza kwandikiwa kitabu kama hicho.


  Ya mwisho, Mkuu Matondo, nashukuru sana kwa uvumilivu wako juu ya Kiswahili changu dhaifu. Maana yake Ndugu zangu wengi ANONYMOUS hukimbilia zaidi kushambulia ?msamiyati? (VOCABULARY) wa Ndugu
  Manyanya Phiri badala ya kuzungumzia pointi.


  Juu ya hilo suala, tena naomba uvumilivu niwe mpana kidogo, mimi ningefurahi zaidi kusahihishwa lugha. Tena na tangaza sasa, kwa maandishi yangu yoyote yale wasomaji wenzangu wako huru kabisa kufanya ile COPY AND PASTE na wanisahihishe baada ya hapo watume kwa manyanyaphiri@gmail.com

  Nami watakapojaribu kwandikia blogu yangu ya Kizulu, nitafanya hivyohivyo kuwasahihisha kwa uungwana.


  Afrika ni moja!

  ReplyDelete
 2. Yaani Matondo na ujanja wako umeoa mchaga! Pole sana kaka yangu. Mimi nilimuoa na kumuacha hata kabla ya mwaka kuisha baada ya kugundua kuwa wale waliniambia ni kaka na uncles wake tulikuwa tukila chungu kimoja. Hii mila kwa wachaga na wapare huwezi kuiondoa kwenye DNA zao. Ninavyojua malezi ya kisukuma, nakiri kusema kwenye miti hakuna wajenzi. Pole sana kakaangu. Yethu na Maria!

  ReplyDelete
  Replies
  1. you suck you young ass hole kabila lenyu limefanya nini thats why you cant show your face and head made of stupidity

   Delete
  2. Pole pole mdau hapo juu kwani naona huyo Msukuma hapo juu amekutibua kweli kweli...LOL

   Delete
 3. Anonymous wewe unachukia wachaga bure. Kama mke wako alikuwa malaya si kwa sababu ni mchaga bali tabia ya mtu binafsi. Hii mila hata kama ipo ni juu ya mtu binafsi kuifuata au kuachana nayo.
  Wachaga ni watu kama wengine. Je kwenye kabila lako mna mila gani unayoina kuwa siyo?

  ReplyDelete
 4. @2Anonymous: Nami nakubaliana kabisa na mjadala wenu wote wawili ndugu zangu, Anonymous. Huwezi kabisa ukasema eti kwasababu 'nimegombana na huyo Mzungu mmoja kwa hiyo wote Wazungu ni wabaya".

  Mawazo kama hayo ni dalili za ujinga kwasababu na huyo CAIN (jambazi wa kwanza katika historia ya binadamu) hakumchinja mtu wa kabila lingine lahasha! BALI ALIMWUA MDOGO WAKE KABISA, ABEL!!!

  ReplyDelete
 5. Tuache ushabiki wa kipumbavu. Anonymous ametoboa ukweli. Chunguza malezi ya watoto wa kichaga. Ni besha besha na si utu utu. Ukitaka kujua wachaga ni wa hovyo kiasi gani hebu mwambie rafiki yako kuwa unataka kuoa mchaga au mpare. Atakuonea huruma akijua kuwa umekwisha.
  Tusianze kutukanana ujinga bila kufikiri. Wachaga, wahaya, wamanyema, wazaramo na wengine ni mishipa katika maisha ya ndoa. Weldone Anonymous kuanzisha mjadala huu. Najua wengi watapinga kutokana na mapenzi ya wake zao ambao wameishawaoa au kuwa wachaga. Wizi, umalaya, uvivu na uchafu ni sifa kubwa za wachaga na wapare bila kusahau uchoyo na ubahiri. Nitarejea baadaye.

  ReplyDelete
 6. Ni kweli kwenye makabila yetu huwa kuna baadhi ya mila ni balaa, lakini hii haina maana kwamba mf. wakurya wote hupiga wake zao na hawana mapenzi kwa wake zao lakini wapo ndani ya kabila hilo wastaarabu, wachaga nao pamoja na tabia zao chafu (hii ikiwa ni pamoja na kung'ang'ania kuolewa na wazungu ama mtu mwenye uwezo) lakini wapo wenye tabia njema na mapenzi ya dhati kama ambavyo mwenye blogu anavyompotrei mkewe ni wazi ni binti na mama mwema au siyo bwana Matondo unatufanya tuamini kuwa huna hata chembe ya majuto kumuoa mchagga huyo. Hata hivyo mko mbali na maingliano ya kimila. Tukumbuke kila kwenye kabila kasoro hazikosekani japokuwa kuna baadhi ya makabila watu hutamani kama si kuoa huko basi ni kuolewa huko hili lipo tukubali au tukatae. WACHAGGA OYEEEEEEEEEEEEEEE!!!!!!!!!!!!!!!!

  ReplyDelete
 7. Sina shaka Phiri nawe unatetea wakwe zako. Maana wanyasa waliokimbia Malawi kwa kupenda kuoa wachaga hamna mfano!
  Mtaibiwa, kuziniwa na hatimaye kumalizwa kabisa kwa kudhani mmepata wakati mmepatikana.
  Nashikilia msimamo wangu kuwa mwanamke wa kichaga si wa kuoa. Maana ni hatari kwa mtu asiyechagua kiasi cha kufakamiwa hata na kaka yake na mjomba wake. Hawa watu ni pesa. Hata baba yake mdogo akiwa na pesa anachukua tu mradi atoe kitu kidogo.Kwao mwili ni mtaji na kifaa cha kusaka pesa. Kweli mwenye mapenzi haoni na chongo huita kengeza. Wachaga ZIIIIIIIIIII.

  ReplyDelete
 8. Mmmmm! Mimi wala sijitetei wala kutia neno hapa. Nawaachia Wachaga wajitetee wenyewe. Hata Bwana Phiri simtetei. Kazi kweli kweli!

  ReplyDelete
 9. @Anonymousx3
  Bondeni hapa ya Afrika tunalo kabila (sitataja jina) ambalo ukimpenda mwanamama wa kabila lao na kujiandaa kutoa mahali, basi mama-mkwe, enzi za kale lakini, lazima alale nawe kusudi eti akuonje ili ajuwe "je mwanae hatakufa njaa kitandani?" Basi, huo ni ushamba kabisa; na wengi wenye ustaarabu wakabila hilo wamekwisha acha uchafu huo katika utamaduni wao (na mmoja au wawili kutoka kabila hilo ni raisi au wamekwisha kuwa raisi wa Afrika Kusini), kwani mila na desturi za kabila ni kiumbe chenye uhai na kinabadilika jinsi wakati unavyosonga mbele.


  Wengi sana katika hilo kabila la kulala na mama-mkwe walijikuta wanatoroka naye mama maana yake labda waligunduana ni "watamu" kuliko na yule mtoto!!!!!Lakini sisi wasiokuwa wenye kabila hilo Afrika Kusini, hatuwezi kujipatia haki ya kuwatukana wote wenye kabila hilo kutokana na mambo ya kale yenye kabila lao, kwani nasi tunayo ya kwetu (SKELETONS IN THE CUPBOARD).


  Kuhusu Wanyasa, Aiseee, Anonymous-wangapi, SOMA KIDOGO, Ndugu yangu: WANYASA NI TAIFA, SIYO KABILA! Kisiasa za nchi kadhaa (mfano Tanzania, Afrika Kusini) unaweza kusema "Mnyasa ni kabila", lakini kimasomo ya ETHNOLOGY huwezi ukafananisha Mchagga, Msotho au Mpedi na Mnyasa!


  Katika Wanyasa wapo Wachewa, Wangonde, Watonga namakabila mengimengi tu. Sasa ni wepi unayodai wamewoa Wachagga wengi? Sasa kama wamewoa Wachagga kuna ubaya gani hapo? Si wewe Wachagga unawaona takataka tu? Pilipili usizozila zakuwashaje?

  Kuhusu mimi binafsi, siMnyasa tu, bali kabila langu niMtumbuka kabila ambalo ni ndugu nao Watonga(ila nikusaidie wewe @Anonymous-Namba-Ngapi).


  Kitumbuka sijui zaidi ya "Monile! Mulimakola?" kwani mimi mzaliwa Afrika Kusini na mama wa kabila Swati/Swazi, na kabila Swati liko nchini Afrika Kusini (50.5%) na Swaziland (49.5%).

  Watumbuka mizizi yao ya kwanza iko Afrika Magharibi (kama nchi Cameroon) na Afrika Kusini hapo baadaye kutokana na vita vya Waafrika dhidhi ya ukoloni waWaingereza na kukamatwa kwa Waafrika (Mfecane/Difaqane) ili wawe watumwa wa BRITISH SETTLERS Afrika Kusini. Labda utanielewa kwa urahisi ninaposema tofauti katika Wangoni, Watumbuka na Watonga haipo, na kama ipo, kwa Kiingereza tunasema IT IS ACADEMIC BORDERING PURELY ON DIALECTS ELEVATED TO INDEPENDENT-LANGUAGE STATUS BY THE DIVIDE-AND-RULE-MINDED COLONIZER.


  Basi hao Watumbuka, Mkuu Anonymous, ndilo kabila langu mimi. Nina uhakika ni hilohilo kabila ambalo unadai [ni Wanyasa waliyowoa au kuolewa na Wachagga].


  Lakini kwanini usichunguze wangapi haohao Watumbuka waliyowoa wanadada wa kabila lako wewe mwenyewe Anonymous?


  Utakuta kibao!


  Kwasababu sisi Watumbuka, kutokana na chimbuko letu labda, hatuna ukabila kabisa.


  Baba yangu mzazi alikuwa ananishauri ningali mtoto:

  "Mwanangu, ni aibu kubwa mwanaume UNAZALIWA HAPA, UNASOMEA SHULE HAPOHAPO, UNAFANYIA KAZI PAPOHAPO ULIPOZALIWA, UNAMWOA MWANAMKE KUTOKA HAPOHAPO ULIPOZALIWA; NA UNAFIA HUKO HUKO ULIPOZALIWA: HAIDHURU POTELEA MBALI". Wazulu nao wanamuunga mkono Baba wanaposema [ITUNA LENDODA LISECELENI KWENTABA= ["kaburi la mwanaume halisi mbali sana na nyumbani kwao tena kwenye milima kabisa"]


  Kumaliza (kwasababu umedai labda nami nimemwoa Mchagga, tena ningekiri kwa kujigamba ingekuwa hivyo kwani Wachagga na Wapare wanazo sura nzuri sana), mimi ninawake wawili. Wakwanza ni Mhehe wa Iringa (najuwa utasema "ni mlambwa na kwanini Bwana Phiri umemwoa?")

  Mke wangu wapili niMswati kutoka Mbabane Swaziland (nao Waswati wanasifa zao mbaya na nzuri). Moja ya sifa zao ni kupendeza kwa wanadada wa nchi hiyo, mke wangu wapili yeye lakini anayo sura mbaya, kumradhi, kama unavyoweza wewe mwenyewe kushuhudia ukitembelea website ifwatao: http://www.youtube.com/watch?v=h5p1V_E-MkQ.


  Mkuu Anonymous, ukitaka mke aliyekamilika na mwenye kabila liliyokamilika, nakushauri wende mbinguni umtafute malaika! Maana yake maneno yako siyo utani kabisa na ingekuwa utani ungejitambulisha kusudi nasi tukwelewe nakweli wewe ni mtani wa Wachagga!

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU