NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Monday, February 21, 2011

ZAWADI ZANGU ZA VALENTINE DAY !!!

Zawadi hizi bora kabisa ni kutoka kwa mabinti 
Minza (aka Zofa - darasa la kwanza) na Kija (darasa la 4). 
Kwangu mimi, hakuna zawadi nzuri kushinda hizi !!!

7 comments:

 1. ni zawadi nzuri na kumbukumbu nzuri sana nakushauri uzitunze na ukiweza fanya kama picha vile sijui kama umenielewa?

  ReplyDelete
 2. Dah! hongera sana kwa kupata watoto wa namna hiyo, kwa kweli ukiwa kama mzazi halafu mwanao awe anakukumbuka hivi hutia raha sana...

  Hongereni mashangazi zangu.

  ReplyDelete
 3. Hongera sana Kaka, kizuri sana ni kwamba malaika hawa tayari wanajua unachokifanya kwao. Mungu awabariki sana na azidi kuwalinda.
  Mdau Japan

  ReplyDelete
 4. Ni jambo la kujivunia kwa watoto kuonesha upendo kwa mzazi,yote ni matokeo ya malezi stahili toka kwa mzazi. Hongera kwa mabinti na familia nzima ya Matondo. Tutajitahidi kuiga mwenendo huu mzuri wa malezi.

  ReplyDelete
 5. Asanteni. Kama wazazi, ni wajibu wetu kufanya kila tuwezalo ili kuwawezesha malaika hawa wa Mungu kuwa na utoto wenye neema na kuwapatia urithi wa maana yaani elimu bora. Na huku ughaibuni hii ni kazi ya kila siku, kila saa na kila dakika.

  Da Yasinta - asante kwa ushauri. Nimekuelewa.

  Da Mija - ndiyo mashangazi zako wanakua tena kwa haraka. Pengine siku moja wataweza kuonana na akina Manjula.

  Mdau wa Japan - asante pia na tunatumaini kwamba Mungu Ameisikia sala yako.

  Matiya - "madume" yako yanasemaje? Peleka salamu.

  ReplyDelete
 6. Kwakweli inafurahisha.

  Mimi nina kumbukumbu kutoka kwa marehemu baba yangu mpendwa, mimi pamoja na ndugu zangu tukiwa tungali wadogo sana alisafiri nje ya nchi, lakini wakati huo tukiwa hata kusoma hatujui kila wakati alikuwa akituandikia postcard (miaka 40 iliyopita) ambazo tulikuja kuzisoma baada ya kuwa wakubwa na kujua kusoma kila mmoja wetu katunza za kwakwe, kwakweli hizo ni kumbukumbu tosha kwani alitupenda kwa dhati nasi pia tulimpenda. Yafurahisha sana kuona mzazi akiwapenda wanawe (hasa mzazi wa kiume). Ni kumbukumbu nzuri sana hifadhi.

  ReplyDelete
 7. Matondo salamu zako zimewafikia. Madume yangu pamoja na ka-dada kao hako kamoja wanafanya vizuri. Wawili ambao wapo primary so far wanamekuwa leaders kwenye mitihani yao. Ninaimani hawataniangusha mbele ya safari.

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU