NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Tuesday, March 8, 2011

ATI, NI SAWA KUIHASI MIJIBABA INAYOBAKA NA KULAWITI VITOTO VIDOGO???

 • Japo baadhi ya majimbo hapa Marekani (mf. Texas na Lousiana); na baadhi ya nchi (mf. Poland) zimeidhinisha kuhasi kama adhabu mojawapo kwa watu hasa, wataalamu wengi wanasema kwamba kuwahasi siyo utatuzi wa tatizo hili kwani "tiba" hii haigusi hasa kiini cha tatizo lenyewe ambalo ni la kisaikolojia zaidi.
 • Mimi nadhani kwamba kwa nyumbani visa vingi vya ubakaji na ulawiti wa watoto wadogo vinahusishwa na imani za kishirikina, jambo ambalo linatatanisha zaidi kuhusu utatuzi wake. Ati, tuwafanye nini watu wanaobaka na kulawiti watoto wadogo?

8 comments:

 1. tawaelimishi kiroho wajitambue ili waweze kuzitawala hisia zao vyema

  ReplyDelete
 2. Wewe kama mzazi swali la kujiuliza je kama mtu kama huyo kamfanyia mtoto wako hivyoungechukua hatua gani? Na imani za dini zinasemaje, kwani ninawasiwasi kuwa sheria za kidunia zimeshindwa!

  ReplyDelete
 3. LOL. Kumbe hata walawiti nao wana ARI MPYA, KASI MPYA NA NGUVU MPYA??? Nice

  Adhabu sahihi kwa hawa watu ni kuwaweka katika kisiwa chao peke yao mbali kabisa na watu wengine. Wakae huko wabakane wao kwa wao mpaka wote wafe. Nawachukia sana watu hawa.

  ReplyDelete
 4. Haki ya Mungu Imetulia yaani atatoka na ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya. Du!!!!

  ReplyDelete
 5. @Kamala - wanaweza kubadilika kwa mafunzo tu? Wakati wa Septemba 11 kuna watu walitoa pendekezo kama hili. Kwamba magaidi wapewe "therapy" ili hatimaye waweze kubadilika.

  @Mfunguo - unaunga mkono kuhasiwa au unapinga?

  @emu-three - watu ambao watoto wao walifanyiwa hivi walipohojiwa wapo waliokuwa na hasira na kudai kwamba adhabu sahihi ni kwa watu hawa kunyongwa. Wapo ambao walisema kwamba walikuwa wameshawasamehe na walikuwa wamemwachia Mungu. Wachache waliunga mkono kuhasiwa!

  @anony - una uhakika gani kwamba hawa jamaa hawatatengeneza mitumbwi na kwenda sehemu zingine "kubangaiza"?

  @ Lutonja - kama Mwanasaikolojia, hili suala unalionaje? Unapendekeza nini?

  ReplyDelete
 6. Mi nashauri KUHASIWA ni adhabu inayomtosha mbaki kwani kamwe hatorudia kitendo hicho na ataishi kwa kusononeka mpaka mwisho wa maisha yake. Lakini pia nakuwa na wasiwasi kwamba yanaweza yakatengenezwa majitu mengine ya ajabu kwani baada ya kuhasiwa yanaweza sasa kubuni njia nyingine ya kufanya uhalifu kama kuwa na chuki kali ambaya inaweza kupelekea mauaji kwa wengine.

  Au kama ingewezekana na yenyewe ya bakwe ili yaone ni jinsi gani aliyebakwa huwa anapata maumivu gani ya kimwili na kiakili. Na kubwaka huku si kwamba abakwe na mwanamume isipokuwa kumuingilia kwa vifaa ambavyo vitamuumiza mpaka akome. Nawachukia sana wabakaji kwa njia yoyote ile maana hawana tofauti na wauwaji na wengi pia huishia kuua.

  Kabla ya kutoa hukumu ni vyema yakaoulizwa ni kwanini yalibaka kisha nayo yaingiziwe kama ni mti au kitu chochote ambacho yatakifanya yasikie maumivu ambayo yanawasababishia wenzao.

  Ikiwa wezi wa TSh 1000 hishia kuchomwa (japokuwa adhabu hii imeshindwa kutolewa kwa akina vijisenti, Mramba na wezi wengine) basi na suala la ubakaji tukikataka tunaweza kutoa adhabu kali.

  SWALI:
  UNASHITAKIWA MIAKA KUMI au UNAHUKUMIWA MIAKA KUMI?

  ReplyDelete
 7. Anony - wataalamu wa Saikolojia wanadai kwamba kuwahasi hakusaidii sana kwani tatizo la watu hawa siyo ngono peke yake. Hata kama ukiua kabisa uwezo wao wa kufanya ngono na vitoto vidogo, bado tamaa yao itakuwepo na lazima watakuwa na njia zingine za "kujifurahisha" na vitoto vidogo.

  Wabakaji na walawiti wa vitoto hivi wameonyesha kwamba hupata faraja na ridhiko la ajabu kingono kutoka kwa watoto - kitu ambacho hawakipati wakingonoka na wanawake. Kwa mijitu hii, ili kukidhi tamaa zao ni lazima wapate watoto wadogo na si vinginevyo!

  Kuhusu swali lako, nadhani mchora katuni alikosea. Inapaswa kuwa unahukumiwa miaka kumi...

  Tunaishi katika dunia ya ajabu sana na matendo kama haya yanatosha kukukumbusha kwamba binadamu siye ni wanyama tu na si vinginevyo. Ati, ulishawahi kumwona ng'ombe akingonoka na ndama? Tafakari !!!!

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU