NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Monday, March 14, 2011

CCM YAMTABIRIA SLAA URAIS - BAADA YA MIAKA 50 !!!

John Guninita - M'kiti wa CCM Dar


*Yadai CHADEMA ilichangia mauaji Arusha
Na Anneth Kagenda,Temeke

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimemtaka Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbroad Slaa, aendelee kufanya mazoezi ya kuingia Ikulu kwani huenda baada ya miaka 50 ijayo atanyakua nafasi hiyo. Pia kimeitaka Serikali kuacha kumtafuta mchawi katika tukio la mauaji lililotokana na maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), mkoani Arusha na badala yake iwakamate viongozi wa juu wa chama hicho akidai kuwa wamekuwa wachochezi wakuu wa kuvuruga amani nchini.

Hayo yalisemwa jana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Temeke Mwembe Yanga wakati akijibu hoja mbalimbali zinazohusu chama hicho.

Amesema Dk. Slaa aendelee kuhangaika kutafuta urais labda huenda ipo siku Mungu atamuona na kumbarikia urais.

Amesema kama wao walijiona ni ‘ngangari’ kwanini hawakuingia kituoni kuchukua silaha na badala yake waliwashinikiza wananchi.

“Naunga mkono kauli ya waziri Mizengo Pinda bungeni kwamba CHADEMA ndio waliosababisha vurugu na vifo vya watu na hii ni kutokana na kukosa hoja ya kuing'oa CCM madarakani na badala yake wanatangaza udini makanisani eti mchague Wakristo ndio wenye hoja za msingi,” amesema Gugunita.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Ramadhan Madabida, amesema mfanyabiashara atakayepandisha bei ya sukari zaidi ya sh. 1,700 atanyang'anywa leseni yake ya biashara.

CHANZO: Dar Leo

3 comments:

 1. CCM inanifurahisha sana. CCM Oyeeee. Tutakuwa madarakani kwa miaka mingine 50 ijayo. Uwiiiiiiiiiiii....

  ReplyDelete
 2. Ningependa kuisikia CCM ikiongelea masuala ya maslahi ya Taifa. Nimeshachoka kuwasikia walivyo na mawazo finyu ya kuongelea uchaguzi tu na suala la kuingia Ikulu. Angalau CHADEMA inaongelea maslahi ya Taifa, kama vile kupambana na ufisadi.

  Je, iwapo Dr. Slaa atagombea mwaka 2015 na wananchi wakampa kura za ushindi, inamaanisha CCM itazuia?

  Mimi ni raia ambaye si mwanachama wa chama chochote cha siasa. Natafuta ukweli. Jambo moja la ukweli ni kuwa CCM ina historia ya kusababisha mauaji nchini. Uthibitisho wa hilo ni kutoka taasisi huru si vyama vya siasa. Kwa mfano, soma hapa.

  Vile vile, wa-Tanzania tuzingatie kuwa Mwalimu Nyerere, katika miaka yake ya mwisho alikuwa akiishutumu CCM na kututahadharisha wa-Tanzania kuhusu CCM. Kwa mfano soma hapa.

  Kadiri siku zinavyozidi kupita, naendelea kuhofia hatima ya Tanzania, kutokana na ubovu wa uongozi wa CCM kama alivyoelezea Mwalimu Nyerere.

  Tungekuwa na uongozi wenye busara na wenye kuzingatia haki, hatungefika hapa tulipo, kwani uongozi wa kweli unategemea kile kinachoitwa "emotional intelligence." Kwa kigezo hiki, CCM ni sifuri, na ndio maana amani ya nchi inaendelea kudidimia.

  ReplyDelete
 3. Profesa Mbele - sijui kwa nini CCM hawawezi kusimama kifua mbele na kujibu hoja za Chadema. Ni kweli hawana mema ambayo wamefanya kwa miaka 34 waliyokaa madarakani? Kama yapo, mbona wasisimame kifua mbele na kuyanadi majukwaani? Mbona wanakimbilia kulalamika na kutisha kutumia nguvu za dola?

  Kauli kama hizi za kejeli hazikisaidii chama hiki na viongozi kama hawa pengine wanaonyesha kwamba bado hawajaweza kusoma alama za nyakati na kuona kwamba mambo kidogo yameanza kubadilika. Inashangaza sana !!!

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU