NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Tuesday, March 22, 2011

ETI, KUTUMIA LUGHA YENYE KUONYESHA USAWA WA KIJINSIA KATIKA BIBLIA (ZA KISASA) NI "KUCHAKACHUA" NENO LA MUNGU?

Kwa tunaoamini kwamba Biblia ni neno la Mungu, ni sawa kweli kuibadilishabadilisha mara kwa mara ili lugha yake iendane na wakati uliopo na mazingira tuliyomo? 

Swali hili limezuka baada ya wafasri wa toleo jipya la mwaka huu la Biblia inayopendwa sana ya New International Version Bible (NIV) kuamua kutumia lugha inayoakisi usawa wa kijinsia. Kwa mfano, badala ya kusema, "If anyone says, 'I love God,' yet hates his brother, he is a liar.", sasa Biblia hiyo inasomeka "If anyone says, "I love God,' yet hates his brother or sister, he is a liar."

Kuna wanaodai kwamba Biblia ni neno la Mungu na kamwe haipaswi kuwa inabadilishwabadilishwa kila mara mikondo au matapo ya mawazo yanapobadilika  katika jamii kwani kwa kufanya hivyo itafikia mahali tutakuwa tunapotosha kabisa maana iliyokusudiwa. Wewe unasemaje kuhusu suala hili?

Kwa habari zaidi kuhusu utata huu wa tafsiri bofya HAPA (Tazama maoni mengi yaliyotolewa hapo). Unaweza pia kusoma kitabu kinachochambua japo hili kwa kina HAPA (pdf - kurasa 357)

3 comments:

 1. ngoja nitulie pahala nisome viungo vyote hivyo viwili kisha nitarejea nikiwa na bahasha ya maoni.

  ReplyDelete
 2. Haya Bwana Mtanga lete mambo, tunakusubiri. Nilikwua naongea na mdau mmoja kuhusu suala hili na aliniambia kwamba pengine Waislamu wana sababu nzuri kwa kutaka Korani yao isiguswe wala kubadilishwa. Tafsiri tofauti zinaweza kufanyika hata bila kuanza kubadilisha kilichoandikwa katika vitabu hivi vitakatifu.

  ReplyDelete
 3. siamini sana kama biblia ni neno la Mungu ila kwenye agano jipya kuna aksi kidogo maneno ya Mungu hasa kwenye zile injili nne za mwanzo mwa agano la kileo

  ila unachokilalamikia sikioni sana kwani hata haya maandiko yaliyopo uliyakuta na huna uhakika kama yalichakachuliwa au la, achilia uwezekano wa kuwa yaliannikwa na mwendawezimu, kichaa au mpotoshaji au yako sahihi

  kwa hiyo, kama NIV na wengine walikuandikia bible ukaiamini, kubali pia mabadiliko wayatakayo

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU