NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Friday, March 4, 2011

FIKRA YA IJUMAA: KWA MNAOPIGANIA "UKOMBOZI" WETU - HEBU SIKILIZENI NA MUUTAFAKARI USHAURI HUU WA FRIEDRICH NIETZCHE (aka MWANAFALSAFA KICHAA)

 • Na ukikaza macho kwa muda mrefu katika ombwe, ombwe nalo pia linakukazia macho. Sijui nani anakuwa anamkazia macho nani. Ndiyo maana kuna imani pia kwamba ukikiangalia kitu kwa muda mrefu sana, kitu hicho ukiangaliacho hatimaye kinaanza kujishabihisha na kuanza kufananafanana nawe. Tutafakari !!!
******************************

   5 comments:

   1. Nafikiri swala hili lilijitokeza sana katika nchi NYINGI AFRIKA baada ya UKOLONI kwa kuwa waliochukua nchi wakaanza kuwa kama wakoloni wao wenyewe!:-(

    ReplyDelete
   2. WaIsrael ni mfano nao mzuri. Jinsi walivyokuwa wanapewa uzito kwa magumu na Hitler sasa wao wana "lipiza kisasi" kwa Wapalestina.

    Afrika Kusini kwetu hapa tumeshuhudia tendo la kutisha sana na serikali ya Zuma, kwani juzi (tarehe 02 Mar 11) polisi walivamia ofisi ya Msimamizi Wa Uma??? (PUBLIC PROTECTOR) na kusaka nyaraka fulani zinazohusu mkubwa wa Polisi nchini Bw Bheki Cele na mambo yake yenye gizagiza.


    Sasa demokrasia yetu, baada ya kupigana kwa mafanikio dhidhi ya Makaburu, ilijengwa juu ya misingi fulani mmoja yake ikiwa ni kuheshimiwa kwa ofisi ya PUBLIC PROTECTOR na serikali.


    Lakini polisi wa huyo Cele wameingia mule bila kibali chochote hata kibali sha hakimu hawakuwa nacho, mithili ya vitendo vya Makaburu dhidhi ya wazalendo enzi za Apartheid.

    Zuma mwenyewe aliwahi kuingiliwa na polisi usiku wa manane wakitaka kampyuta zake na mambo kama hayo miaka mitatu kama hivi iliyopita walipokuwa wanamsingizia ameiba hela nasi wananchi tukamwonea huruma Mzulu wawatu aliyekuwa anapingwa na Watembu (kabila la Mandela) pia na Waingereza ila asiyingie madarakani.


    Hatukujua kwamba punde Zuma huyohuyo, baada ya kuingia madarakani tuliempa sisi wananchi licha kwamba ana elimu yake ya Darasa la nne tu shuleni rasmi atakuja kutugeuka na kushambulia moja ya nguzo za demokrasia yetu: PUBLIC PROTECTOR.


    Kwako Mkuu Nzuzullima (MMN), nasema Asante kwa kunipa moyo wakumsoma yule Mwanafalsafa: wakati wote nilikuwa namwonea uvivu!

    ReplyDelete
   3. wanasiasa lao moja, kuna wanaotumia mapungufu ya waliomadarakani ili nao wapate madaraka

    soma mafundisho ya jamaa aitwaye OSHO kuhusu uchaguzi

    ReplyDelete
   4. ...akizizungumza rais wake Kikwete, halafu hapo hapo jamaa akajisahihisha na kusema "akizizungumza rais WETU Kikwete...

    Mna bahati Kikwete ni mpole na mwoga. Ningekuwa mimi rais wewe na makengeza yako pamoja na huyo padri wako sa ivi mngekuwa mko Segerea. Mnachezea amani yetu hivi hivi wakati nyie ni matajiri tayari. Mambo yakichafuka haoooo mnakimbia na kwenda zenu Ulaya na kutuacha sisi Walalahoi tukionja joto ya serikali. Kama hamuwezi kutumia njia sahihi basi acheni mmeshashindwa. God Bless My Bueatiful country Tanzania !!!!

    ReplyDelete
   5. haya makengeza haya yanatupeleka pabaya Watanzania. Tujihadhari !!!

    ReplyDelete

   JIANDIKISHE HAPA

   Enter your email address:

   Delivered by FeedBurner

   VITAMBULISHO VYETU