NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Friday, March 25, 2011

HEBU SIKILIZA "MKASA" WA HUYU AJUZA WA MIAKA 92

 • Ni juzi tu hapa hapa Florida. Ajuza huyu pichani kwa jina Helen Staudinger (miaka 92) alikwenda kwa jirani yake mwanaume aitwaye Dwight Bettner (miaka 53). Jirani akamwomba mzee huyu aondoke. Ajuza wa watu akaomba apigwe angalau busu kwanza ndiyo aondoke. Dwight akakataa katakata.
 • Basi mwishowe Bi mkubwa akaondoka kwa shingo upande. Alipofika nyumbani akachukua bunduki yake na kuanza kuungurumisha risasi kibao kuelekea nyumba ya jirani yake aliyemnyima malavidavi. Bahati nzuri hakuna risasi zilizompata jirani yake Dwight. Polisi wakaitwa na ajuza wa watu akatupwa rumande. Masharti ya dhamana ni dola 15,000. Dwight anadai kwamba ajuza huyu ameonyesha kumzimia (kimapenzi) tangu ahamie hapo anapoishi karibu miezi sita hivi iliyopita, na hajui ni kwa nini.Tangu hapo mapenzi hayachagui rangi, umri, tabaka wala umbo ati!
Mkasa huu unapatikana HAPA na HAPA.

6 comments:

 1. HE!!! LOL!! I am so sorry for laughing but I really can't pull a picture to imagine this whole picture. Sote tungekuwa tunafanya hivi pale tunapokataliwa, mbona tungeisha! Poor lady

  ReplyDelete
 2. Homoni za bibi bado zinafanya kazi au kama sivyo basi ni msukumo wa kisaikolojia au pengine vyote!

  ReplyDelete
 3. wakati wa usichana wake aliwabania ma-agemate wake sasa anajuta

  ReplyDelete
 4. Bi mkubwa anachohitaji ni affection wajua binadamu tunahitaji kupendwa na si mara zote tunahitaji sexual intercorse bila shaka alichojitaji ni maneno mazuri naogopa kuamini alitaka kutoa tundi kwa mjukuu wake maana sielewi kama uso tu una hali hiyo maeneo mengine yanafanana vipi.

  Yote kwa yote alihitaji kuoneshwa upendo. Hebu jaribu kuvuta hisia ni jinsi gani uliyempenda kabla hajakukubalia ulivjojihisi? Ni wazi kama ungekuwa na bunduki karibu ungemtandika, mapenzi yanauma ati!

  Nakumbuka mimi mpenzi wangua kabla hajanikubali hakuelewa mapenzi ya dhati niliyokuwa nayo juu yake ilikuwa ni kuzungushwa kusikokuwa nma mwisho, sijui kama ningekuwa na jibunduki ningethubutu kuelekeza uelekeo wake.

  Si ajabu wengine kuwa na uhusiano na wanyama maana hakuwa wa kuwaliwaza, lakini anaweza kupata babu na wakawa marafiki hata kama si wa kula tundi ilmradi hata wa kumshika mkono.

  Simlaumu pia huyo jamaa maana bi mkubwa umri umekwenda na aweza hata kufa ktk purukushani za kutoa tundi kama ndo alichokihitaji alipokwenda kwa mpenzi aliyemwogopo.

  Je kaka Mat angekutokea wewe ungefanyaje????????????!!!!!!!!!!!!!!!

  ReplyDelete
 5. Mapenzi hayana umri, na ampenzi sio lazima vile tunavyojua, hata busu, au kusema `nakupenda' au kushikana mkono, inatosha,...!

  ReplyDelete
 6. Je kaka Mat angekutokea wewe ungefanyaje????????????!!!!!!!!!!!!!!!

  ---Pengine ningemkumbatia na kumpiga busu la shavuni. Hakuna ubaya wa kufanya hivyo. Au pengine ningempa maneno mazuri tu...

  Lakini pia hatujui mambo ambayo huyu jirani alikuwa tayari ameshafanyiwa na huyu Bi. Mkubwa mpaka kujua kwamba (Bi Mkubwa) alikuwa amemzimia.

  Au inawezekana pia ikawa ni haya maisha ya wenzetu ya umimi. Mtu mko jirani lakini hamsalimiani wala kuongeleshana utafikiri mmeshagombana.

  Lakini Bi. Mkubwa naye ukomandoo wote huu wa nini?

  We kamala weweeee !!!!

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU