NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Tuesday, March 1, 2011

HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MH. DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE JANA TAREHE 28/2/2011

 
 • Kwa habari zaidi na maoni mengi ya wananchi kuhusu hotuba hii tembelea HAPA, HAPA na HAPA. Unaweza kuisoma hotuba hii nzima nzima HAPA. Wakati haya yakijiri, habari zinasema kwamba CHADEMA wanaandaa tamko kali ili kujibu hotuba hii ya raisi ambaye kwa sasa yuko Paris nchini Ufaransa. Mungu Ibariki Tanzania !!!
Nyongeza
 • Tamko kali la CHADEMA naona limeshatoka. Bofya HAPA na HAPA kulisoma pamoja na kufuatilia maoni ya wadau.  Baraza la vyama vya siasa nalo limeitisha kikao ili kuijadili CHADEMA (Bofya HAPA).
  ************

  Hapa chini ni maandamano ya CHADEMA mkoani 
  Shinyanga (kuanzia dakika ya 3:40)

  8 comments:

  1. Hotuba dhidi ya Chadema ni dalili tosha za kujihami(defensive mechanism) kwa kile ambacho kinaweza kumtokea kama mambo yalivyokuwa kule Misri na Tunisia endapo yeye na serikali yake watashindwa hatajirekebisha na kukabiliana na matatizo mbali mbali yanayowakumba wananchi wa Tanzania. Mojawapo,ni hili la U-Vasco da Gama!

   ReplyDelete
  2. Matiya U-Vasco da Gama ni tatizo gani? Fafanua kidogo.

   ReplyDelete
  3. Mapinduzi yaliyotokea Tunisia, Misri na hatimaye kujitandaza katika nchi nyingine za Kiarabu ni matunda ya unyanyapaa, dharau, kujiamini kupita kiasi kwa watawala, ufisadi, umasikini, ukosefu wa uhuru, maisha magumu kwa wananchi walio wengi na kadhia nyinginezo. Binadamu ni kiumbe mwenye utashi na japo anaweza kuvumilia madhila na kadhia mbalimbali, ukiendelea kumbana sana hatimaye hufikia hatua ya "liwalo na liwe". Historia inaonyesha kwamba hatua hii ikishafikiwa, hata ungekuwa na silaha kali na jeshi lenye nguvu namna gani ni kazi bure!


   Ningeshauri kwamba raisi wetu na serikali yake pamoja na chama kinachoongoza wakae chini na kufikiri kwa makini sana kuhusu kero za msingi za wananchi na waandae mikakati ya haraka ya kuzitatua. Na hapa nazungumzia wananchi wa kawaida ambao maisha yamewachachia. Wananchi hawa ukiwasikiliza kwa makini wana madai ya msingi sana (mf. ugumu wa maisha, ukosefu wa ajira, kupanda kwa bei za bidhaa za msingi na hasa vyakula, kuchoshwa na ufisadi na mengineyo). Serikali iliyoko madarakani inabidi ionyeshe kwa vitendo nia thabiti ya kutaka kutatua matatizo haya yanayowakabili wananchi wa kawaida. Bila kuyashughulikia matatizo haya ya wananchi, ni wazi kwamba tunakoelekea si kuzuri. Wananchi wamechoka na siasa na sasa wanataka kutatuliwa matatizo yao. Kikwete ni kiongozi mzuri na sipendi kuamini kwamba atakubali machafuko na kuparaganyika kwa amani kuwe katika wasifu wake. CCM - nendeni huko mikoani. Wasikilizeni wananchi wa kawaida na jaribuni kuwatatulia matatizo yao. Mkifanya hivi basi hamtakuwa na haja ya kuwa na wasiwasi na CHADEMA !!!

   CHADEMA kwa sasa wanaonekana kama chama cha "ukombozi" kwa sababu wanagusa na kutonesha hisia za wananchi. Ni matumaini yangu kwamba wataitumia nafasi hii vizuri na kuhakikisha kwamba nchi yetu haiingii katika machafuko.

   Kukaa na kulaumu CHADEMA si suluhisho kwani CHADEMA si tatizo. Tatizo ni uongozi mbovu. Sikilizeni matakwa ya wananchi and CHADEMA will never be a threat !!!!


   God Bless Tanzania !!!

   ReplyDelete
  4. Tukubaliane. Kikwete anapwaya kiasi cha kuonekana kama ajali ya kisiasa kwa nchi yetu. Tujifunze kutorudia kura kwa kuchagua watu kwa sura zao badala ya uwezo wao.

   ReplyDelete
  5. Matondo, U-Vasco da Gama kwa maana ya rais mpenda safari za nje ya nchi ambazo kwa tafsiri ya watanzania wengi ni mzigo kwa serikali.

   ReplyDelete
  6. ...Nimefurahiswa na kupendezwa na hii hotuba ya kiongozi mkuu wa nchi. Kidogo nimepata majibu ya maswala ambayo nalikuwa yananikeleketa moyoni, pamoja na kwamba Mkuu wa Nchi bado analalamika kama mwananchi wa kawaida wakati yeye ni Amiri mkuu.
   Tanzania ya leo kila mtu ni Mwanasiasa,na siasa zetu zimekuwa ni ''dodoki'', kila tunachosikia tunakubaliana nacho na kila tunachokifikili tunakihalalisha na tunataka kifanyike kulingana na matakwa tunayotaka.
   Kama sikosei, Rais amezungumuzia mambo makuu matano yanayolikabili taifa kwa muda huu; 1)milipuko ya mabomu, 2)hali ya chakula nchini, 3)bei ya sukari, 4)swala la umeme, na 5)hali ya usalama nchini
   Kitu kinachonishangaza ni kundi kubwa la watu kuamua kujadili sana swala ta tano(hali ya usalama nchini) na kuamua kuyasahau maswala mengine manne ambayo kwa mtazamo wangu ndiyo yanayozaa swala la tano. Wengi wanasema, Rais hakupaswa kuzungumzia swala hili huku akikituhumu Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) kuwa ndiyo chachu!!.
   Ninapata sana matumaini ninapoona wananchi wanapojua wajibu wao katika uendeshaji wa nchi(demokrasia), vilevile, ninapatwa na wasiwasi kuwa Nchi yetu inaelekea kusikojulikana pale ninapogundua wengi hawajui mipaka yake. Na kutokana na hili, wengi wanakuwa kama ''dodoki'' au wanageuzwa na siasa za ''dodoki'' kuwa kama ''dodoki''.
   Nilipigwa na butwaa kusikia wanasiasa maarufu wanadiriki kusema Tanzania inaweza kuwa kama Tunisia, Misri au Libya. Kweli!!!
   Kijiographia na Kisiasa haingiliki akilini Tanzania ikalinganiswa na nchi hizi za mashariki ya mbali na kama milinganisho inafanywa na wanasiasa na kukubaliwa na jamii, basi nitaamini siasa za Tanzania ni ''dodoki''

   ReplyDelete
  7. Binti Kombo - sijui kama blogu hizi zinasomwa na wahusika. Kama zinasomwa basi watakuwa wamekusikia bila shaka! Asante kwa maoni yako mazuri na ya kujenga.

   Ng'wanaMwamapalala - Umegusia jambo la muhimu sana. Mambo mengine yaliyozungumziwa, japo ni ya muhimu sana, yanaonekana kupuuzwa. Leo nilikuwa naongea na watu kutoka Bariadi na wanasema kwamba mwaka huu hakuna mvua kabisa na ni wazi kwamba kutakuwa na njaa kali sana. Ng'ombe waliokuwa wanauzwa kwa laki mbili na nusu sasa wanauzwa kwa laki moja na nusu na bado kungali mapema kabisa. Vipi kufikia mwezi wa sita kama mvua itakuwa haijanyesha? Sijui kama serikali imejiandaa vilivyo kupambana na hali hii.

   Matiya - asante kwa ufafanuzi. Hivi ni kweli kwamba hakuna tunachofaidika kutokana na "Uvasco da Gama" wa kiongozi wetu? Tukipewa data kuhusu tulivyofaidika utabadili msimamo wako?

   Mwalimu Mhango - sina uhakika. Yawezekana ikawa tu kwamba tunapita katika kipindi kimojawapo cha muhimu - kipindi cha uhuru wa habari na mtandao ambapo kila kitu kiko wazi? Fikiria tungekuwa na uhuru na uwazi wa aina hii tulikotoka ingekuwaje? Tatizo kubwa pekee ninaloliona kwa rais wangu wa awamu ya nne ni upole na kutopenda kuchukua maamuzi mazito, na kwa hili anapoteza nafasi ya muhimu sana ya kuandika Historia nzuri. Ngoja tuone miaka minne iliyobakia.

   ReplyDelete

  JIANDIKISHE HAPA

  Enter your email address:

  Delivered by FeedBurner

  VITAMBULISHO VYETU