NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Friday, March 11, 2011

KWA WOTE MLIOKO JAPAN NA HASA WATANZANIA WENZETU: POLENI SANA NA TUNAWAOMBEA !!!

Ukurasa wa mbele wa Huffington Post leo
 • Poleni kwa kukumbwa na tetemeko hili kubwa pamoja na Sunami iliyofuatia. Mungu Awashike mkono na kuwatia nguvu. Tunaomba na kutumaini kwamba hakuna Mtanzania aliyepoteza/atakayepoteza maisha. Amina !!!

  7 comments:

  1. Mungu na awalinde Wote,maana inasikitisha.

   ReplyDelete
  2. tawire matondo

   tawire edna

   mungu awape rehema na uvumilivu watu wote waliokumbwa na gharika kuu hili.

   ReplyDelete
  3. Amina jamani tunashukuru kwa maombi yenu,kwani tumetokea dirishani kujiokoa japokuwa hujui huko uendako kupoje, Maana majumba yalivyomarefu,aisee inatisha lakini ni kama sinema vile.

   ReplyDelete
  4. SWAHILI WANASEMA DUNIA RANGI RANGILE ASOHILI ANA LILE. TUKIANGALIA KIUTAFITI DUNIA INAZIDI KUDUMA
   KATIKA NCHI AMBAZO KUNA ZULUMA NDANI YAKE HAKUNA KITU KIBAYA MUNGU HAKIPENDI KAMA ZULUMA. BINADAMU IMEFIKA MPAKA DUNIA WANAIZULUMU. KWA KUJENGWA VISIVYOTAKIWA KUJENGWA. HAYA YALIO TOKEZEA NCHINI JAPANI KWA UPANDE WETU SISI TUNA SEMA MAJUJUU WA MAJUJU. NABADO ITAZIDI KUTOKE MPAKA PALE MWANADAMU WATAKAPOACHA KUZULUMU.

   KAKA MZUZULIMA NAOMBA NA MIMI UNIPANDISHIE BLOG YANGU KATIKA MLINGOTI WAKO WA BLOGLIST ZAKO KAMA ITAPENDEZATAFADHALI.
   http://swahilivilla.blogspot.com/

   ReplyDelete
  5. Hali inazidi kutisha kwani sasa vinu kadhaa vya Nyuklia navyo vimeanza kuleta kasheshe! Mungu Awasaidie jamani!

   Bwana Ebou - hata sijui unazungumzia dhuluma gani. Pengine ukifafanua na kutoa mifano tutaelewa zaidi.

   Unajua binadamu ni kiumbe mbunifu sana na ubunifu wake huu umemletea Neema na wakati mwingine maafa. Japan ni kisiwa na kina watu wengi. Kama unataka kusema kwamba wamekosea kujenga maghorofa, nchi yao ni kisiwa na njia pekee ya kukidhi mahitaji ya nyumba ni kwenda juu. Na teknolojia waliyonayo imewafanya kukabiliana vyema na matetemeko haya. Maangamizi makubwa yametokana na sunami na siyo kuanguka kwa majumba.

   Kama nilivyosema hapo juu fafanua unachotaka kusema ili tukuelewe vizuri.

   Na pengine badala ya kuanza kulaumu ni vyema kuombeana na kusaidiana wakati wa janga kama hili. Halafu janga likipita ndiyo tukae chini na kuaanza kuangalia vyanzo na visababishi vyake na nini cha kufanya.

   Je, kule Haiti nako ambako tetemeko "dogo" la 7.0 liliua watu zaidi ya laki 5 tena bila sunami nako walikuwa wamefanya dhuluma gani?

   ReplyDelete
  6. hapa sitamung'unya maneno. tatizo alilonalo ndugu Ebou ni kuwaacha wengine wasome na wamsimulie ili yeye aamini tu. hasomi mwenyewe na kupambanua mwenyewe. amejazwa imani bila yeye kujiuliza ukweli na uwongo wa imani mbalimbali ikiwemo ya kwake.

   anataka kutuambia kila kunako janga kuna dhuluma. profesa matondo umeenda mbali kutoa mfano wa haiti. yale mafuriko ya kilosa mwaka jana watu wa kule kilosa walimdhulumu nani? mabomu ya mbagala na gongo la mboto wale wahanga wamemdhulumu nani.

   tatizo lake keshaambiwa nchi zote zilizoendelea zilidhulumu pahala na zote ziko ulaya.

   ReplyDelete
  7. Mwacheni Mungu Aitwe Mungu. We Ebou hebu na ushindwe na ulegee pamoja na kiblogu chako kisicho na mbele wala nyuma cha http://swahilivilla.blogspot.com/.

   Huna ustaarabu kabisa na unakera. Hebu na upate pigo kubwa mpaka ulegee kabisa !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

   ReplyDelete

  JIANDIKISHE HAPA

  Enter your email address:

  Delivered by FeedBurner

  VITAMBULISHO VYETU