NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Tuesday, March 1, 2011

MKAZI WA BUKOBA AMTIMUA KAKAKE HOSPITALINI AKIFIKIRI KUWA NI KWAKE - UCHESHI

 • Japo huu (hapa chini) ni ucheshi ni lazima tukiri kwamba mambo siku hizi yamebadilika sana. Undugu umeisha. Upendo umepungua; na ushirikiano wa kindugu kama ule wa zamani sasa hakuna. Kukosana kwa ndugu (wa tumbo moja) sasa ni jambo la kawaida tu. Jambo hili huwa linanisikitisha sana. Ni kwa nini ndugu wa tumbo moja mkosane hata mfikie hatua ya kutosalimiana na kujuliana hali?
 • Na ukichunguza kwa makini unakuta kwamba ni sababu za kipumbavu tu. Mara nyingi ni wivu na ubinafsi - huyu kaendelea sana na ndugu zake wamekuwa mzigo. Au eti huyu mmoja kaoa mke "mkorofi" ambaye hataki mume wake awe na uhusiano wo wote na ndugu zake. Au ndugu mmoja kawa mlokole na anawaona hawa ndugu zake ambao hawajaokoka kama vile makapi na kwa hivyo anawatenga. Na wakati mwingine ndugu mmoja "aliyeendelea" sasa ana dhana mpya kuhusu familia, dhana ya Kimagharibi kwamba familia ni yeye, mke na watoto wake tu na hataki uhusiano wo wote na mtu mwingine ye yote katika familia yake - wakiwemo ndugu zake wa tumbo moja!
 • Katika hili mimi huwa napenda kujifanya "mjinga" huku nikiomba msamaha na kujinyenyekeza. Kwa nini ndugu wa tumbo moja, ndugu mlionyonya ziwa moja la mama na kukulia katika nyumba moja mkosane kiasi cha "kurogana", kutakiana mabaya na kutojuliana hali? Kwa nini ??? 
*******************************
 • Hebu tuburudike na hiki kipande cha "Nshomile". Kihaya changu hata hivyo karibu chote kimepotea na sasa napata shida hata ya kujua nini kinaimbwa hapa...Kamala na Mzee wa Changamoto pengine watasaidia kututonya mada kuu katika wimbo huu.

6 comments:

 1. Mimi ni mmoja wa watu ambao sisalimiani na ndugu zangu wa tumbo moja na wala sitaki hata kuwasikia. Haya mambo ya kijamaa na kushirikiana ndiyo yametufanya Waafrika kuwa masikini, wazembe na tusioendelea. Mtu unazaa mtoto wako mmoja ili umsomeshe vizuri hata eti wajomba, mashangazi na ndugu wengine wanakuletea matoto yao uyasomeshe. Aka, wazae walee na wasomeshe mwenyewe. Kwangu haki ya mama hawakanyagi na sitaki kusikia cha ndugu, mzazi wala upuuzi mwingine.

  And surprisingly, nimeweza kuendelea sana tangu niwacut off. Hii mila ya kusaidiana kama ndugu ilikuwa ni upumbavu mtupu na wala sitaki hata kuisikia 1

  ReplyDelete
 2. Hahahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

  Naogopa NIKISEMA MAANA YA WIMBO NTAKUWA NATEKELEZA LINALOIMBWA KISHA NIWE MFANO HAI WA KIIMBWACHO
  Hahahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
  Oooh My God.

  You made my night

  ReplyDelete
 3. Mzee wa Changamoto - kinachoimbwa ni kibaya? Mi nimeona wanafunzi wa shule nikajiaminisha kwamba lazima litakuwa ni jambo la muhimu.

  Tunusishe angalau kamuhtasari tu...

  Kamala - kwa nini huna oni?

  Na anony - hilo nalo neno. Pengine ndiyo maana umeendelea. Ndiyo faida ya "usomi" hiyo ati! Hongera sana !!!

  ReplyDelete
 4. Mbaya zaidi ukikaa nao na kuwasaidia inafika kipindi wanataka watunge sheria. Wasome shule wanazoenda wanao, kila kitu wapate kama wanao. Nimesaidia mayatima, lakini sasa inatosha. Mungu anisamehe kama ntakuwa nakosea, lakini inafika point najiuliza kama mimi nikifa watoto wangu wataweza pata hata robo ya hicho nilichojitolea.

  Wimbo mzuri na wanacheza vizuri sana japo sielewi wanachosema. Kwa kweli wanacheza vizuri sana.

  ReplyDelete
 5. Mwalimu, Mwalimu, Mwalimu
  Unaamini kuwa UWEPO wa wanafunzi unamaanisha kitu kizuri? Kwanini si uwepo wa WAALIMU? Hasa kwa kuwa waalimu wanawafunza wanafunzi. Utaaminije kuwa akiwepo mwanafunzi atakuwa na muonekano bora iwapo mwanafunzi huyo anafunzwa na mwalimu ambaye (pengne) usingeona kuwa anawakilisha tabia njema?
  Mmhhhhhhh!!!
  Kubwa ni MAJIGAMBO ya waHaya kuwa "wanatuonea wivu kwa kuwa tumesoma".
  Na naamini umesema NIGUSIE na hapo nimegusa
  ENJOY
  Hahahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU