NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Thursday, March 3, 2011

MUUNGWANA NI KITENDO: TABIA YA KUKAA VIJIWENI NA KUSUBIRI MAENDELEO YASHUKE KUTOKA MBINGUNI KAMA MVUA !!!


Hii tabia ya kukaa vijiweni kutwa imeshalalamikiwa sana na wanaharakati wengi kuwa ni kikwazo cha maendeleo. Vijana wenye afya na nguvu zao wanakaa kijiweni siku nzima na kusubiri serikali iwaletee maendeleo. Pengine ni kweli kwamba hakuna ajira, lakini kukaa kijiweni bila kuchacharika ni kujiangamiza kabisa. Hongera FeDe kwa kuikemea tabia hii ya uvivu !!!

3 comments:

 1. Hili ni tatizo kubwa kwakweli na linazidi kukua siku hadi siku, na baya zaidi vijana nguvu kazi wanakimbia kijijini kuja mjini, wakiwa hawana malango maalumu, na wakija hapa mjini ndio hiyo kukaa kijiweni huku wakisubiri `kengele'...USICHEZE MBALI...wanavyoita wenyewe!

  ReplyDelete
 2. Watanzania wote ni wavivu period kuanzia Vasco da Gama wao mpaka balozi wa nyumba kumi na mzee wa familia. Kutoendelea kwetu ni kosa letu wote na tusimbebeshe JK mzigo huu. We are all to blame.

  When did you go into the office and worked real hard since morning till end of the day??? Kwa wenzetu huku you get paid FOR WORKING na siyo kupiga umbea. And if you ask me. JK is the BEST president we have ever had, period !!!!

  ReplyDelete
 3. Halafu, hao wa-Tanzania wanaopiga usingizi chini ya mwembe kwenye hiyo katuni wanangojea ajira milioni na nusu walizoahidiwa na serikali. Hapo ng'ambo ya barabara unaweza kukuta maktaba ya mkoa. Hawajawahi kuingia humo hata siku moja wakasome vitabu angalau kujiongezea ujuzi na maarifa ili ikitokea intavyuu ya ajira, waweze kufanya vizuri. Hawawazii kuwa kusomasoma vitabu vya kiIngereza, kwa mfano, kungewaongezea ujuzi wa lugha hiyo. Lakini wao wako hapo chini ya mwembe kila siku, mwaka hadi mwaka. Wakenya wakija wanashinda intavyuu kirahisi na kujitwalia ajira zilizopo, na kuwaacha hao wa-Tanzania hapo chini ya mwembe wakingojea ajira walizoahidiwa na serikali.

  Ingawa maktaba ipo hapo hapo mjini, utawasikia baadhi ya hao wa-Tanzania wakidai kuwa hawajasoma kwa sababu ya sera za maaskofu. Utadhani kwamba kuna maaskofu kwenye mlango wa maktaba wanaowazuia kuingia.

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU