NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Thursday, March 17, 2011

LOLIONDO, LOLIONDOO, LOLIONDOOO - MPAKA LINI ???

 • Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi Bw. James Mbatia amedai kwamba  serikali imefikia kikomo cha kufikiri kuhusu utatuzi wa matatizo ya wananchi hasa wakati huu ambapo juhudi zote zimeelekezwa Loliondo badala ya kumakinikia masuala ya msingi yanayoikabili jamii. Msikilize Mbatia hapa chini (video kwa hisani ya Mtaa kwa Mtaa Blog.) Kwingineko

(1) Mke na mume wanapofumaniana kwa babu


(2) Wenye pesa zao sasa wanatua kwa helikopta

Picha inapatikana HAPA

(3) Mzee wa Kiraracha akitoa ushuhuda

 • Inasemekana sasa watu kutoka mataifa ya nje mpaka Afrika Kusini wanakuja kwa babu (Bofya HAPA). Dawa hiyo pia inasemekana inasaidia kurudisha "netiweki" kwa wanaume. Wanasiasa nao eti wanajaribu kufaidika kisiasa na tiba hiyo. Mungu Ibariki Tanzania!

  5 comments:

  1. ....kama sinema vile lakini ndio kweli, wanasemaga nabii hakubaliwagi kwao...

   ReplyDelete
  2. Kumbe watanzania na watawala wao wote ni wagonjwa! siku watakapogundua ukweli mchungu kuwa wadhaniacho ndicho sicho watalia na kusaga meno.
   Japo Loliondo imeleta nafuu kwa mafisadi, kupuuzia kadhia ya umeme italigharimu taifa vibaya sana.Leo babu wa Loliondo kesho shehe wa Mtakuja na baadaye tunarudi kule kule kwenye chanzo cha matatizo, ndiyo Bongolalaland na wabongolalanders,

   ReplyDelete
  3. Du Mrema amaeisha mwili akili roho hata sauti! Hivi hawa waliomchagua mbona hawakumuonea huruma? Au ni wana CCM na mafisadi walioamua kumdhalilisha naye akadhalilika? Tangulia Lyatonga ukale ugali na Nyerere. Oh sorry na Kawawa. Yethu na Maria arawa umekwisha hivi. Kwani hakuna kisusio marangu au umekataa kuiba. Utakula mafi yako.

   ReplyDelete
  4. Tangu tuache kuwa Nchi ya Nyerere tukageuka kuwa nchi ya kitu kidogo...nchi ya kikombe cha babu!

   ReplyDelete

  JIANDIKISHE HAPA

  Enter your email address:

  Delivered by FeedBurner

  VITAMBULISHO VYETU