NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Friday, March 25, 2011

SERIKALI YAWAPIGA MARUFUKU WAGANGA WA KIENYEJI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu wa bunge ), William Lukuvi (wa pili kulia) na Rosemary Nyerere wakipata kikombe cha babu Loliondo. Picha kutoka kwa Mjengwa.********************
Angalizo langu

Ati, waganga wa kienyeji ni tatizo? Au tatizo ni jamii yenyewe na wale wanaoiongoza? Ni kweli kwamba kupiga marufuku waganga wa kienyeji (kujitangaza) ndiyo suluhisho? Serikali inajua ni kwa nini watu wanakimbilia kwa waganga wa kienyeji; na kutafuta tiba zingine mbadala? Ni kwa nini imani za kishirikina zinazidi kujiimarisha katika jamii wakati huu ambapo dunia imepiga kasi kubwa ya kimaendeleo?  Waganga wote ni walaghai? Kutoa amri bila kuangalia hasa kiini cha tatizo lenyewe ni kupoteza muda tu.

***************************
Serikali yawapiga marufuku waganga 
(Alhamisi, 24/3/2011)
Anthony Mayunga, Musoma

WAGANGA wa tiba za jadi nchini ,wanatakiwa kuacha mara moja kudanganya watu kuwa wanatibu magonjwa kama kifua kikuu, kisukari na Ukimwi kwa kuwa sheria haziwataki kujitangazana badala yake wanapaswa kutangazwa na wanaopata tiba na kupona.

Onyo hilo kali limekuja wakati maelefu ya watu kutoka ndani na nje ya nchi wakiwa wanaendelea kumiminika katika Kijiji cha Samunge kupata tiba kutoka kwa Mmchungaji mstaafu Ambilikile Mwasapile.

Mchungaji huyo amekuwa akitibu  magonjwa sugu yakiwemo kifua kikuu, kisukari, Ukimwi, degedege na shinikizo la damu. Onyo dhidi ya waganga, lilitolewa jana na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk Lucy Nkya, katika hotuba yake kuhusu maadhimisho ya Siku ya Kifua kikuu Duniani yaliyofanyika  kitaifa mkoani Mara. Alisema kuenea ugonjwa wa kifua kikuu unaenea kwa kasi kwa sababu  wananchi wanakubali kudanganywa na waganga hao.

“Nasema kuanzia sasa ni marufuku kwa waganga wa kienyeji, kuwadanganya wagonjwa kuwa wanatibu magonjwa kama hayo, maana mnadanganya watu na wanazidi kufa. Hatutaruhusu tena mchezo huo, narudia ni marufuku, tiba halisi inatolewa hospitalini si kwingineko," alisema Naibu Waziri.

Alisema waganga wazuri hawajitangazi na kwamba wanaopaswa kujitangaza ni wafanyabiashara tu  ambao kazi yao kudanganya watu kwa kutumia matangazo mazuri mazuri.

Hata hivyo Naibu Waziri huyo hakugusia tiba inayotolewa na Mchungaji Mwasapile, ambayo watu mbalimbali wakiwemo viongozi waandamizi wa serikali, wamewahi kuitumkia.

Akizungumzia mikakati ya serikali kupambana na ugonjwa wa kifua kikuu, alisema wizara imeanza kusambaza aina mpya ya darubini za kisasa za LED, zenye uwezo mkubwa zaidi wa  kugundua vimelea vya kifua kikuu katika makohozi.

“Hadi kufikioa mwisho wa mwaka huu, asilimia 95 ya hospitali zote za wilaya, zitapata darubini hizi mpya na ifikapo mwishoni mwa 2012 hospitali zote zikiwemo za mashirika ya dini zitakuwa zimepata, vifaa vipya vya kuoteshea vimelea vya kifua kikuu,”alisema na kuongeza.

Alisema  vifaa hivyo vitafungwa katika maabara za Hospitali za Muhimbili, Mbeya, Bugando na Kibong’oto.

Alikiri kuwa wizara hiyo inakabiliwa na upungufu wa wataalam wakiwemo mafundi sanifu wa maabara na uelewa mdogo wa jamii  kuhusu ugonjwa wa kifua kikuu. 

Chanzo: Mwananchi

2 comments:

  1. Huyo Lukuvi si waziri wa serikali huyo. Sasa kama serikali yenyewe inakunywa vikombe kwa waganga, mbona tena inawapiga marufuku. Hatuna dira. Tunakwenda tu kama wehu, kila mtu na lwake. Mungu Atusaidieeee

    ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU