NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Wednesday, March 9, 2011

TAARIFA YA HABARI YA ITV KUHUSU LOLIONDO

Nyongeza

(1) Serikali yasitisha huduma za Loliondo kwa sababu za usafi
   

  (2) Masharti ya Tiba ya Loliondo (Channel Ten)

  Ni lazima babu akupe dawa mwenyewe. Usipolipa sh. 500 huponi. 
  Ni lazima unywee hapo hapo. Imani yako ndiyo itakuponya!  (3) Serikali Haijazuia tiba ya Loliondo (12/3/2011)  Video hizi ni kutoka kwa Kennedy.

  3 comments:

  1. kumekuwa na baadhi ya watu kukosa imani na matibabu ya mchungani mwasapile maarufu BABU. pengine niseme tu kuwa watu hawa wenye imani haba hawajaugua, wakiugua watakuwa na imani tu na watashangaa wamefikaje loliondo.

   ugonjwa ni nini na tiba ni nini. ugonjwa ni hali ya kutojisikia sawasawa katika maungo ya mtu. ndipo mtu huyo huitaji msaada wa kugangwa. ni mtu huyu ndio ataitwa 'mgonjwa' baada ya kufanyiwa vipimo na kuthibitisha ugonjwa wake. hapa atahitaji matibabu (tiba). kwa sasa, magonjwa mengine hayana tiba hivyo kupelekea wagonjwa kuendelea kuwa wagonjwa pengine wakisubiri neema na remema za mungu kuendelea kuishi.

   inapotokea mtu mmoja anatoa dawa kutoka kwenye miti na wagonjwa wanakunywa na kutojisikia kuumwa tena basi wanakuwa sio wagonjwa tena. nani alisema tiba shurti itolewe kunako hospitali.

   ReplyDelete
  2. Mwaipopo - ngoja tuone "miujiza" hii itakakoishia. Kama watu wangekuwa hawaponi,kwa sasa wangekuwa wamegundua ukweli na wasingekuwa wanamiminika kwenda huko.

   Kwa wanasayansi na watu wanaolitazama hili katika mtazamo wa elimu "ya kisasa" ambapo dawa - hata zile zilizothibitishwa kutibu magonjwa husika vizuri - hutolewa kwa dozi maalumu na huchukua muda mpaka mgonjwa apate nafuu. Hii ya kunywa dawa mara moja tu na kupona papo hapo haiingii akilini pengine kama ni miujiza au ni aina fulani ya tiba ambayo hatujaizoea.

   Wasiwasi mwingine ni ule ukweli kwamba kumeshakuwa na watu wengi, wakiwemo watu wa dini, waliodai kuwa na tiba za magonjwa haya ya hatari ukiwemo UKIMWI, watu wakakimbilia huko na kudai kuwa wamepona lakini baadaye ikagundulika kwamba haikuwa kweli.

   Pamoja na wasiwasi wangu kuhusu tiba za aina hii, naomba tiba hii iwe ya kweli kwani itasaidia sana watu masikini ingawa hata vigogo nao wamevamia huko!

   ReplyDelete
  3. hapa inafanya kazi ilekanuni ya imani, kuna watakaopona (japo wachache) na watakaougua zaidi baada ya kwenda hukuo.

   ndo jamii yetu hiyo, hata mimi nikitaka kutajirika nazusha ishu kama hii.

   cha kujiuliza ni unataka upone ili iweje?

   anyway mfumko wa bei, kupanda gharama za maisha, huleta hofu, kutokuwa tayari kukabiliana na hali halisi ay kujisimamia, tunatafuta pa kuegemea, akitokea kama huyu, twakimbilia kuponywa sio kujiponya

   watu wanataka kupona ukimwi ili wakafanye ngono zaidi!

   ReplyDelete

  JIANDIKISHE HAPA

  Enter your email address:

  Delivered by FeedBurner

  VITAMBULISHO VYETU