NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Wednesday, March 16, 2011

TATIZO LA WANAUME KUPIGWA NA WAKE ZAO LINAZIDI KUJIIMARISHA !!!

Inaonekana hili tatizo la wanaume kupigwa katika ndoa zao ni kubwa. Nimeshangaa kusikia katika video hii kwamba nchini Kenya eti theluthi moja ya wanaume wanakung'utwa majumbani mwao. Pengine ndiyo maana wenzao wa Tanzania waliamua kuanzisha chama chao kabisa. Jamii, hata hivyo, imekazania tu kupigania haki za wanawake. Na wanaume hawa je?


12 comments:

 1. Nadhani wanahitaji kuwezeshwa....najua unajua ninamaanisha nini mkuu....lol!

  ReplyDelete
 2. Nimemwogopa huyo mama....Lakini sijaelewa huu mtindo wa kupiga je? wanafikiri wampigapo mtu ndo atajirekebisha au ndo itakuwaje?

  ReplyDelete
 3. hahahahaha@kaka Matondo asante na Hongera sana kwa kuweka hiki kisa!

  jamani wale waliokuwa wanasema hivi kweli Wanaume wanapigwa haya mambo hayo!

  Swali kwa Wanaume je kutokana na hari hii,mnaona bora kuwe na chama cha kuwa tetea au bado manajikaza Kiume?

  pole kaka uliyepigwa!.

  ReplyDelete
 4. Sijui kwanini mimi nahisi hata Lucy mke wa Rais anampiga Rais Kibaki kutokana tu na navyoona chemistry yao hadharani!:-(

  ReplyDelete
 5. @Swahili na Waswahili

  Maoni yangu wasifanye chama chao kwani ndipo hapo watakung'utwa zaidi. Bora wabembeleze vyama hivyo vya wanamama vibadili katiba yazo ili kuwakubali nao wanababa mule.


  Kusmema ukweli haya mambo ya kupigana ndoani ni moja ya mbinu za kuendeleza nguvu za kiuchumi, ninavyoona.

  Kwa maana ingine, kadiri akinamama wanavyopata madaraka zaidi ndoanani KIUCHUMI ndivyo watakavyoendelea kutunyuka tu sisi wanaume!

  ReplyDelete
 6. Dah, hii kali. Mi siku nikipigwa na mwanamke ni afadhali nijiue tu.

  Kuna tetesi nyingi zinazosema kwamba Kibaki huwa anapigwa na mkewe Lucy na kuna wakati eti aliwahi kumfinya hadharani.

  ReplyDelete
 7. Anony: Ukijiua inamsaidia nani? wewe ama huyo mwanamke? Ukitaka kujiua toa taarifa ili upate waridhi wasobwengwa....lol!

  ReplyDelete
 8. Swali kubwa ni `kwanini wapigwe?' kwasababu haiwezekani mtu akatoka from no where akatembeza mkong'oto!
  Kwa uoni wangu ni kuwa;
  -Hakuna mapenzi na kama yapo dhana nzima ya nini maana ya ndoa haijulikani
  -Kama ni mila na desturi, kwa mfano kuna kabila fulani bila kupigwa mke unakuwa hujaonyesha mapenzi(brutal love) wanajua wenyewe!
  Kwahiyo tukijua sababuu ya mkongoto tunaweza tukasema ipo sababu ya chama cha utetezi au la...huenda midume yenyewe kazi ni tungi kwa kwenda mbele, au hawatimizi wajibu wao kama `wanaume'
  Nawaza tu

  ReplyDelete
 9. Wapendwa, asanteni kwa maoni yenu. Inaonekana hili tatizo lipo miongoni mwetu na wanaume wengi wanajikaza kiume tu wakiogopa aibu mbele ya jamii. Afadhali huyu jamaa yeye kajitokeza na mke wake anavyoonekana ni mkali kweli na hataki mchezo.

  @Manyanya - wanawake watakubali kweli tujiunge na vyama vyao vya kupigania haki na usawa? Pengine kuunda vyama vyetu wenyewe ndiyo njia sahihi zaidi.

  @Mtakatifu - huyu mama pia anafananafanana na Lucy Kibaki. Huenda ni mtu na dadake hawa LOL !

  @Ng'wanambiti - ukinikorofisha nitamwambia dadangu aanze kukupa kibano cha nguvu. Mkurya kutiwa kibano na mwanamke patachimbika eeh!

  Huyu jamaa unataka tumwezeshe kivipi? Inavyoonekana anakunywa si mchezo na mama ndiye anaendesha nyumba. Ndiyo maana akileta za kuleta anaishia kuambulia mkong'oto. Hata tukimwezesha si ajabu akakimbilia baa huyu; na halafu tutarudi pale pale skwea wani!

  @Anony - kutishia kujiua ni dalili ya ufinyu wa mawazo; na au ugonjwa. Kama wazo hili huwa linakujia mara kwa mara, nenda kwa daktari wa akili au watu wa ushauri nasaha ukapate tiba. Wanaume hupambana, ati! Na kama Ng'wanambiti alivyokuuliza, ukijiua itamsaidia nani? Utajiua na utawaachia jamaa mkeo. Pambana!

  @emu-three: nakubaliana nawe kuhusu utungi wa jamaa huyu; na kwa hili pengine mwanamke huyu anastahili kupongezwa. Angelegeza kamba tu huyu mlevi hata hiyo biashara angeivuruga na familia hii ingedidimia. Badala yake mama amejidhatiti kwa mkong'oto!

  Ni kweli huelewi maana ya ndoa? Hata ile maana "sisisi" ya "kuwa mwili mmoja" ya kwenye Biblia? Isije ikawa nawe unaungana na jamaa wanaodai eti "marriage is the greatest hoax invented by man!"

  @Yasinta - Kwa nini huyu mama amekuogopesha. Msikilize vizuri utamwelewa. Ungekuwa yeye ungefanyeje?

  @ Dada Rachel (Swahili na Waswahili) - mada hiii ni mwendelezo wa mada uliyoianzisha kule kibarazani kwako. Huu ni ushahidi kwamba kweli kuna wanaume wanaokung'utwa na wanawake majumbani mwao. Mtusaidie jamani!

  ReplyDelete
 10. Kaka Matondo hii imenichekesha mno leo, imebidi niisogeze pale kibarazani kwangu.

  Nakubaliana na wewe kwamba nadhani hili tatizo lipo sana ila mnajikaza kisabuni.

  Kazi njema.

  ReplyDelete
 11. Da Mija, nasubiri nione wanaume watakavyosema katika kibaraza chako.

  Fikiria, Mkurya kama Ng'wanambiti eti atandikwe na mwanamke? Kweli?

  Ukimsikiliza vizuri huyu mwanaume katika video hii, ni ukosefu wa nguzu za kiuchumi unaomfanya avumilie mkong'oto - sababu ile ile inayowafanya wanawake wengi kuvumilia mateso kutoka kwa waume zao. Uchumi !

  ReplyDelete
 12. Duh! Kweli hata mimi sipati picha, Ng'wanambiti kutandikwa na maiwaifu, ila hatuwezijua labda ndo maisha yake kila siku.

  Halafu umeongea jambo la msingi sana kwamba umasikini ni chanzo cha yote si kwa mume au mke, naona sasa umefika wakati wa kuziacha hizi dhana za nani afanye kazi na nani aangalie watoto nyumbani, au kushinda baa na vibarazani kucheza bao...

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU