NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Monday, March 28, 2011

UTAFITI: UWEZEKANO WA KUPATA MSHTUKO WA MOYO HUONGEZEKA MARA TATU BAADA YA KUFANYA NGONO NA MARA TANO BAADA YA KUFANYA MAZOEZI MAKALI !!!

 Picha hii inapatikana HAPA
 • Sote tumeshasikia kuhusu wanamichezo walioanguka viwanjani na kukata roho. Pia tumeshasikia kuhusu watu waliofia kwenye majumba ya kulala wageni ambako walikuwa wamekwenda na wapenzi wao kujifurahisha. Vifo vya aina hii hutajwa sana katika vyombo vya habari na huonekana kwamba siyo vya kawaida.
 • Kwa mfano, mwaka jana nilipokuwa nyumbani, jamaa mmoja mashuhuri pale Bariadi kwa uuzaji wa bia za jumla jumla, na mwenye mke na watoto, alifia katika nyumba ya kulala wageni akiwa na mwanamke mwingine. Kifo hiki kilileta gumzo kubwa pale mjini na kama kawaida imani za kishirikina zilichukua nafasi kubwa huku wengine wakidai kwamba marehemu alikuwa amewekewa mtego. Wengine walidai kwamba pengine ni papara za kuzini ndizo zilikuwa zimemtoa roho. Tangu hapo mkamia maji hayanywi ati!
 • Wanasayansi sasa wanadai kwamba matukio kama haya, japo ni ya nadra sana, hayapaswi kutushangaza yanapotokea kwani wamegundua ushahidi kwamba uwezekano wa mtu kupata mshtuko wa moyo na kukata roho mara moja huongezeka mara tatu zaidi baada ya kufanya ngono na karibu mara tano baada ya kufanya mazoezi.
 • Watafiti hawa wanasisitiza kwamba japo hakuna haja ya kuogopa kufanya ngono au mazoezi, ni vizuri kuwa waangalifu na kuzingatia ushauri wa madaktari.
Habari zaidi kuhusu utafiti huu zinapatikana HAPA

4 comments:

 1. utafiti huu unatukumbusha kuwa "too much is harmful". Sio kwa kuwa mazoezi ni muhimu, basi ufanye kupita hata na uwezo wa mwili; hapana!

  ReplyDelete
 2. tatizo la kufanya ngono ni kuishia kuwa frastrated kila mara baada ya gori!

  ReplyDelete
 3. `Dont over do...' huu ni usemi wa mwalimu wangu ikifika wikiendi. Kila kitu na mahala pake kwa wakati kwa nafasi yake, na kadiri yake..!

  ReplyDelete
 4. Albert na emu-three: Asanteni. Ni kweli. Kila kitu kwa kiasi chake. Ole wake yule asiyejua nguvu na udhaifu wake...

  Kamala - frustrations za nini tena wakati mtu umeshapata ulichokuwa unakitafuta?

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU