NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Wednesday, March 30, 2011

WASUKUMA MPO? HAPA MNASEMAJE? MAKABILA MENGINE JE?

 • Ndiyo tu nimemaliza kukisoma kitabu hiki juu ya masimulizi ya Wasukuma. Kitabu kimeandikwa na John M. Masuha, kina kurasa 71 na kimechapishwa na East African Literature Bureau mwaka 1963.
Sura ya saba, ukurasa wa 40
 • Kwa vile hakuna jamii ambayo imesimama tisti, ni wazi kwamba mambo mengi yameshabadilika; na sina uhakika kuhusu uhusiano wa uchapakazi na ndoa miongoni mwa vijana wa kisasa. Ati, ni lazima kweli kijana wa Kitanzania wa kisasa awe mchapakazi ndiyo apate mwenzi kama ilivyokuwa kwa Wasukuma na makabila mengine?
Angalizo

Mimi ni mkereketwa wa mambo ya kitamaduni na nitakuwa nawaletea habari juu ya makabila na tamaduni zetu kila ninapozipata. Naamini kwamba hili ni jambo jema!

6 comments:

 1. Unadhani kwa utandawazi wizi huu bado ari ya kufanya kazi kwa wasukuma bado ipo?

  Siku hizi kila mtu anataka good time mjini :-(

  ReplyDelete
  Replies
  1. Hicho kitabu cha Simlizi za Wasukuma nimekimind nakipataje?

   Delete
 2. Hii nii kweli, Wasukuma ni wachapaji kazi wazuri, ...hata lishe yao sio mchezo, chakula ni ugali, kifungua kinywa nini vile?...lol

  ReplyDelete
 3. Si nilisikia siku hizi mambo yote pochi lako tu na kama unapochi la kutosha hata kwa njia za ajabu MTOTOZ MZURIZ fulu kukubali maswala ya ule mpango vipi?:-(

  ReplyDelete
 4. We emu-three - tutanie tu. Yaani hata breakfast ni ugali? Mambo yamebadilika bwana.

  Mtakatifu - Japo ni hivyo pengine wapo wachache ambao bado wanajali maadili na ubinadamu!

  Ng'wanambiti - Kama kila mtu anapata good time mjini, kwa nini Wasukuma waachwe nyuma? Mambo yamebadilika kwa kila mtu.

  ReplyDelete
 5. Utafiti wangu wa haraka haraka unaonyesha popote msukuma anapokuwa matunda ya uchapakazi wake unaonekana. Nilienda wilaya ya Kilembero nikakuta wafugaji wakubwa na wakulima wakubwa wa mpunga huko ni wasukuma. Nilishangaa kukuta mpaka huko Mchinga, Lindi, kuna kijiji ambacho wakazi wa kule walikuwa wanategemea chakula kutoka kwa wasukuma waliohamia huko na mifugo yao. Hata ukienda huko Kigamboni, Kimbiji, mazao mengi ya chakula, matunda na mbogamboga yanayotoka huko kuja mjini yanatokana na wasukuma waliohamia huko

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU