NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Friday, April 8, 2011

BAJAJI YA ZIMA MOTO !!!

Inaonekana bajaji zimegeuka kuwa mkombozi wetu. Tunazo za kubebea wagonjwa; na sasa zima moto.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda akikagua Bajaj ambayo imetengenezwa ili kumudu kazi ya kuzima moto hasa kwenye maeneo yenye barabara nyembamba katika maonesho yaliyoandaliwa na Kampuni ya Spray and Fumigation Services Limited, bungeni Dodoma Alhamisi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu). 

Chanzo: Habari Leo (8/4/2011)

3 comments:

 1. Zinafanya kazi lakini ? Hasa ukizingatia zima moto kubwa kazi zake ni nanihino kinamna fulani!

  Nashukuru angalau kuna jitihada ingawa nawasiwasi na uwezo wa wake wa hizo ndude wa kutuliza tu watu wakati hatari iko palepale kihatari!:-(

  Samahani wote kwa wazo HASI!

  Mkuu Matondo ukipata nafasi pilia kwangu kwenye MADA ihusuyo MISOSI ambayo maswala ya majina ya MISOSI -Samahani majina ya MILO,...
  ....kwa kiswahili yamenishinda na nimeshindwa kumsaidia MDAU kupata jibu.
  Mada yenyewe komenti iliyonishinda ni:``LUGHA haina MANENO ya kutosha hata ya KUTUKANIA ........´´.

  Ntashukuru ukichomekezea neno pale!:-(

  ReplyDelete
 2. Tanzania sasa imegeuka nchi ya mataahira. Kabla hatujaondokana na aibu ya vikombe, sasa wasanii wetu wamekuja na mpya-Bajaj for everything! Tangu lini Bajaj ikazima moto? Badala ya kujidanganya na kuwadanganya wananchi jengeni miji kwa mpangilio. Hapa tatizo si kutokuwapo magari bali miundombinu kama barabara. Kwanini karne ya 21 kuendelea kujenga kama panya?
  Bajaj imegeuka fasheni. Ambulance, Bajaj, zima moto, bajaj, bado treni na meli za Bajaj.Basi tuiite nchi ya vikombe na vi-Bajaj. Bahati mbaya hata watu na watawala wetu wanafikiri ki-Bajajbajaj!
  Suluhu ya tatizo lolote ni kulikabili kisayansi badala ya kuliahirisha.

  Wakati nchi za wenzetu wanatumia madege kuzima moto sisi tunatumia Bajaj! Laiti Pinda angejua aibu iliyoko nyuma ya kadhia hii asingepoteza muda. Sijui kama wataalamu wa viwango na moto wataruhusu upuuzi huu. Hivi Bajaj inabeba maji kiasi gani kiasi cha kuweza kuzima nyumba? Sitashangaa kesho akiitwa rais kuzindua chupa ya chai ya kuzimia moto. Ama kweli wanajua kututenda. Hivi kweli haya ndiyo maisha bora mliyotuahidi? Kwanini nyinyi hamtumii hizo Bajaj kama Bajaj ni deal sana?

  ReplyDelete
 3. Hata magari yetu ya zimamoto yana tabia ya kwenda kwenye moto bila kuwa na maji ya kutosha. Sasa bajaj zijui itakuwaje. Ngoja tuone lakini ni wazi kwamba hatuko siriazi !!!

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU