NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Wednesday, April 13, 2011

ETI, SASA HUYU NDEGE ATARUKA KWA KASI ZAIDI ???

 • Sote tumeona. Ndege mkongwe amejichojoa manyoya ya zamani na kujiotesha manyoya "mapya" yameremetayo japo kwa staili ya "kiurithirithi". Inavyoonekana ndege huyu mpya-mkongwe ameamua kweli kweli kujijengea mazingira mapya na ameanzisha "vita" kuhakikisha kwamba manyoya ya zamani yanabakia kuwa chojozi. Japo baadhi ya waangalizi wa ndege huyu wamefurahia kujichojoa kwake, swali linaloulizwa na mwanakatuni nambari wani wa Tanzania kwa sasa ni hili: Haya manyoya mapya kweli yatamwezesha huyu ndege mnono mpya-mkongwe kuruka kwa kasi zaidi? Tunamtakia urukaji wa kasi mpya mzuri !!! 
 • Wanachama wa CCM waliochaguliwa kuunda sekretarieti mpya  kutoka kushoto ni Mweka Hazina mpya wa CCM taifa Mwigulu Lameck Nchemba, Katibu Itikadi Mwenezi wa CCM taifa Nape Moses Mnauye, Katibu Organaizesheni NEC Bi Asha Abdullah Juma, Naibu Katibu mkuu CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai na January Makamba uhusiano Kimataifa. Picha hii na zingine kuhusu uchojoaji huu wa manyonya zinapatikana HAPA.

  Video kwa hisani ya Kennedy

  ~~~~~~~~~~~~~~~
  Nyongeza (16/4/2011)
   Picha kutoka kwa Mjengwa

  4 comments:

  1. Yawezekana labda baada ya miaka mitano, ataweza kuruka...!

   ReplyDelete
  2. wamewaambia akina lowassa wajitoe wenyewe. kali hii nafikiri ni kiini macho na sio siriasi

   ReplyDelete
  3. Mageuzi yaliyofanyika ndani ya hiki chama kikongwe na chenye historia ya pekee nchini ni makubwa na yanapaswa kupongezwa na wapenda amani na maendeleo nchini. vile vile , kazi iliyofanywa na vyama ya upinzani nchini na hasa CHADEMA haipimiki na siyo ya kubezwa hata kidogo. Labda Swali la kujiuliza, ni kwa nini CCM wameamua kufanya haya mageuzi wanayoita ‘’kujivua gamba’’ kwa sasa na kitu gani kimewapelekea kupata nguvu ya kufanya maamuzi mazito kama haya. Ni vigumu kupata jibu la kikweli katika siasa, hata wanasiasa wahusika hawawezi kutuambia ukweli. Tunabakiwa na fikra za majibu ambazo hatuwezi tukazisema ni sahihi au la.
   Mwalimu Nyerere katika kitabu chake cha Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania, uk 52, alisema, ‘’Kama uongozi ni mbovu, upo kama haupo, au upo kwa maslahi ya wenyewe, watatokea watu waujaze uwazi uliopo; hauwezi kuachwa wazi hivi hivi. Lakini uongozi mbovu ni kama mzoga, una tabia ya kukaribisha mafisi na mainzi. ‘’ , kwa fikra zangu natumaini hili lilikuwa limeisha timilika ndani ya CCM. Baada ya utupu kujazwa na viongozi wabovu, tulianza kushuhudia ‘’mafisi na mainzi’’ yakianza kujongea karibu na matokeo yake, hivi karibuni tumeshuhudia chama kuweweseka na kukosa mwelekeo.
   Mimi kama mpenda maendeleo ya Nchi yetu, Ninampongeza Mwenyekiti wa sasa wa CCM na wazee wa CCM kwa kuliona hili, au labda kwa sasa wamesoma kitabu cha Mwalimu Nyerere na kugundua jamii kwa sasa imeamua tofauti na kusema liwe na liwe kama Mwalimu alivyobainisha katika uk 65 aliposema, ‘’ Kukubali kufanywa vikaragosi vya Viongozi ni dalili ya woga, si dalili ya heshima; na woga na heshima ni vitu viwili mbali mbali. Maadili mema yanatutaka tuwaheshimu Viongozi wetu, madhali wanajitahidi kutimiza wajibu wao. Maadili mema hayatudai tuwaogope Viongozi wetu. Na viongozi makini hupenda kupata heshima ya wananchi wenzao, lakini hawapendi kuogopwa. Kuogopwa ni sifa na ada ya madikteta, viongozi halisi hawapendi kuishiriki. Kujenga mazoea ya kutii viongozi hata katika mambo haramu ni dalili ya woga, ni kukaribisha udikteta’’
   Pamoja na safu mpya ya uongozi kuonekana kama ya ‘’kaurithirithi’’ kama Ndugu yangu Matondo anavyobainisha, hili naliona halina tatizo kwa vile hawa ni vijana wachapa kazi, wana misimamo halisi katika maamuzi, vilevile, uchapakazi wao unaendana na karne ya sasa(sayansi na tekinologia).
   Uhai wa chama chochote unahitaji mabadiliko yanayoendana na mazingira yaliyopo au yanayokuja. Kwa mabadiliko haya, CCM wameonyesha wanauwezo wa kukabiliana na weweseko ndani ya chama na serikali linalosababishwa na ‘’Mapapa’’ kama Mzee Reginald Mengi alivyoita. Vile vile, wamezihirisha kuwa hakuna mkubwa ndani ya chama zaidi ya chama.
   Vilevile, labda msemo usemao ‘’Siku njema huonekana asubuhi’’ utakuwa ni kweli.

   ReplyDelete
  4. Kwa Meghji na Kinana JK amelipa fadhila kwani ndiyo waliochangia kwa kiasi kubwa kumweka madarakani kwa awamu zote mbili alizogombea urais. Kwa Mnauye na January ni mwendelezo wa utawala wa kifalme(NEPOTISM)

   ReplyDelete

  JIANDIKISHE HAPA

  Enter your email address:

  Delivered by FeedBurner

  VITAMBULISHO VYETU