NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Wednesday, April 27, 2011

Hatimaye Obama Awakata Ngebe Wanaodai Kwamba Hakuzaliwa Marekani

Picha hii ya kejeli iko HAPA
 • Hivi karibuni, Donald Trump, bilionea mhafidhina na mpenda majivuno amelifufua suala hili kwa nguvu zote wakati akijiandaa kupambana na Obama katika kinyang'anyiro cha urais mwaka kesho. Ngoja tuone kama cheti hiki kipya kitawanyamazisha hawa wahafidhina. Donald Trump mwenyewe tayari anajivuna kwamba juhudi zake ndizo zimemlazimisha Obama kutoa hiki cheti chake cha sasa. 
Nakala ya cheti kipya. 

3 comments:

 1. Nishakutana na watu mtandaoni wanadai tayari hii ni feki pia! Na kachagua mpaka Daktari ayekufa kwenye sahihi ili asiwepo wa kuhojiwa , tukiachia wadaio hafai kuwa Rais wa Marekani kwa kuwa cheti kinadai ni MUAFRIKA.


  Kuna watu sababu watapata tu hata mtu ujitetee vipi!

  ReplyDelete
 2. Kwa wanaomfahamu Donald Trump hawasiti kutoa hukumu kuwa akili yake ina walakini. Wachambuzi wengi makini wanamdharau. Huyu kimsingi hana tofauti na Ze Comedy kule kwetu. Hata Ze Comedy wana nafuu kwani huwachekesha watu na si kuwafedhehesha kama Trump. Amekuwa akisikika akisema eti atagombea urais jambo ambalo wengi wanaona ni kama kushusha hadhi ya ofisi hii.
  Obama ni intellectual wakati Trump ni just a mere opportunist.
  Obama kaishakuweka historia ya kuwa rais wa Marekani hata kama hawataki. Ajabu hawa hawa wahafidhina ni wale wale walioiingiza Marekani kwenye balaa linalotishia kufanya ipitwe na Uchina muda si mrefu. Maana inakopa karibu kila ndururu toka Uchina. Tungoje tuone.

  ReplyDelete
 3. Watake wastaki Obama ni raisi wa Marekani, na kama wanataka au wanuwezo huo wapande juu wakazibe!

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU