NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Wednesday, April 6, 2011

IT IS OFFICIAL: TANZANIA NI NCHI YA "VIKOMBE". MMOJA AIBUKA IRINGA NA MWINGINE SUMBAWANGA !!!

Kweli mpango mzima sasa ni kumfotokopi Ambilikile tu. 
Hii ni katuni ya Mambo ya Uswazi.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Dkt Antony Mwandulami (58) mkazi wa kijiji cha Itunduma Wangama wilaya ya Njombe Mkoa wa Iringa, ameibuka na kuanza kutoa tiba kwa wagonjwa kwa mtindo wa babu wa Loliondo

******************
 • Ilianzia Samunge Loliondo. Baadaye Rombo, Mbeya (kule Mbarali pia kuna kingine), Bagamoyo, Tabora, Morogoro, Magu na sasa Iringa. Na kote huko kote kunafurika watu, na wengi wanadai kuponywa na kikombe. Na watoa dawa wote hawa wanadai kuwa wameoteshwa ama na Mungu au na ndugu zao ambao ni marehemu. Tuhitimishe nini kuhusu mkururo huu wa tiba hizi za miujiza (aka vikombe)? Ni Mungu Ameanua kuishushia neema Tanzania kwa kuiporomoshea waotaji wengi hivi kwa mpigo ama? 
 • Mjadala mkali kuhusu suala hili ulirindima kule kwa Mjengwa na kwingineko; na inavyoonekana Watanzania wamegawanyika kuhusu suala hili: (1) Wapo wanaoziona tiba hizi kama neema kwa Watanzania wengi ambao ni masikini na wameteseka kwa muda mrefu kutokana na huduma mbovu za kiafya kiasi kwamba wamekata tamaa. (2) Wapo wanaoona matukio haya kama dalili za mwisho wa dunia kama inavyorejelewa katika misahafu mbalimbali ya dini. (3) Wapo ambao hawajui kinachoendelea; na ambao wanasubiri uthibitisho wa kisayansi ili wajue kama kweli tiba hizi zinatibu ama la (bila kujali kwamba mambo ya kiimani kama haya wakati mwingine yanaweza kukinzana na sayansi!). (4) Wapo wanaoona jambo hili kuwa ni njama za wanasiasa ambao wanafurahia kuona kwamba mambo haya yanavutia sana vyombo vya habari kiasi kwamba mambo mengine ya muhimu hayapewi uzito wo wote. (5) Wengine wanaamini kwamba huu ni utapeli tu unaopoteza maisha ya watu bure!
  • Wakati huo huo kuna watu ambao wamekiri kabisa kuwa tiba hizi za kiimani zimewaponya magonjwa yao sugu. Wapo pia ambao wanadai tiba kama hizi hazikuwasaidia. Na kwa vile (eti) imani yako ndiyo inakuponya - ni vigumu kuweka tathmini ya kisayansi kuhusu madai haya na kufikia majumisho yenye kuelezeka. Imani!
  Kombora kwa Babu kutoka Global Publishers HAPA.
   • Ni nini hasa kinaendelea katika suala hili. Kwa nini Tanzania? Kwa nini wakati huu? Ni wazi kwamba maswali ni mengi kuliko majibu. Ngoja tuone hili sokomoko la vikombe litakakoishia. 
   Kwa picha na habari zaidi kuhusu kikombe cha Iringa bofya HAPA. Kikombe cha Sumbawanga bofya HAPA

    7 comments:

    1. Katika mazingira haya ya vikombe kuvuma na kukimbiliwa kila kona, hata serikali ikimlipa Dowans mabilioni yake hakuna atakayejua.

     ReplyDelete
    2. Mwenye akili, mwenye macho na mwenye utambuzi, atajua ni kwanini iwe hivyo...chakuomba ni salama.

     ReplyDelete
    3. Profesa Mbele - si ajabu Dowans keshalamba kilicho chake na kutoweka. Katika harakati, vurugu na mvuvumko huu wa vikombe, ni nani anayejali tena?

     Emu-three - najua wewe ni mwenye akili, mwenye macho na mwenye utambuzi. Kwa nini imekuwa hivi? Nakubaliana nawe kwamba cha kuomba ni salama.

     ReplyDelete
    4. Ngoja na mimi niseme, labda ni wakati wa waafrika kuzirudia dawa zetu za asili, dawa tulizoambiwa ni za kishenzi..

     ReplyDelete
    5. Huu ni ushindi wa kishindo kwa mafisadi! vyombo vya habari vimetekwa kisawasawa!

     ReplyDelete
    6. Tuachane na hili la uponyaji. Hebu tuangalie picha kwa ukubwa. Matukio haya ya kikombe yananipelekea kugundua kuwa Nchi yetu ina matatizo makubwa sana. Siasa za Mwalimu Nyerere pamoja na mila na desturi zetu zimeiacha nchi iliyojaa wananchi wengi wasio wabunifu na wakosefu wa nadhari. (Kwa sasa kila mtu anataka kuwa ''Babu''). Kwa mtaji huu, ninasikitika na kuhoji kama kwa sasa kuna faida ya kuwepo ndani ya jumuiya ya afrika mashariki zaidi ya kuwa ni ''dodoki''. Bila ubunifu na nadhari katika ulimwengu wa soko huria, matokeo yake ni jamii kuachwa nyuma. Sipendi kusema kama Tanzania hii hii katika miaka ya nyuma uchumi wake na siasa zake silikuwa sawa na Indonesia, leo hii ukitembelea Indonesia unajisikia hata aibu kuwa Mtanzania wa leo.
     Nakubaliana na Olijino Komedi katika ujumbe wao ambao unagusa katika nyanja zote za kijamii nchini. Tatizo hii ni kubwa, linahitaji nguvu za kipekee ili kuliondoa. Mfano mdogo tu, Mpaka sasa serikali haijajua ni lugha ipi ya kufundishia mashuleni wakati takwimu zinaonyesha kuwa uchanganyaji wa lugha za kufundishia mashuleni unachangia kushusha kiwango cha elimu nchini. siyo ajabu kuona mtu anatoka mlimani na digrii nzuri wakati hawezi kuzungumza kiingeleza kinagaubaga pamoja na kwamba anaweza kukiandika vizuri, halafu tunategemea aingie katika soko huria la africa mashariki apambane na Wakenya na Waganda bila kuwasahau Waafrika Kusini.
     Kama hatutabadilika na kuachana na viatu vingine vya Mwalimu Nyerere alivyoviacha tutaendelea kudidimia na kubakia kuwa taifa la watumiaji na walaji.
     Hata watu wa mashariki ya mbali(Saudi Arabia, Gulf states) baada ya kugundua kuwa mafuta siyo kila kitu pamoja na kuwapa utajiri mkubwa, wameanza kuweka msukumo zaidi kuibadilisha jamii ili iwe bunifu na nadhifu na kuachana na dhana ya utumiaji na ulaji.

     Sikubaliani kidogo na Profesa Mbele anaposema huu ni muda ambao serikali inaweza kufanya madudu na yasijulikane. Jamani, Tanzania yetu inaendeshwa kidemokrasia(Africa demokrasi). pia, si kuna kambi ya wapinzani serikalini ambayo imejengwa na mawaziri vivuri ambao ndio nguzo katika kukosoa na kuirekebisha serikali katika utendaji wake. pia kambi hii tunategemea kuwa ndio nguzo katika kuhabarisha umma kwa yale serikali inayoyafanya(mazuri au mabaya). siamini kama midomo yao kwa sasa imezibwa kutokana na matukio ya kikombe cha ''babu''.

     ReplyDelete
    7. Taifa lina teketea na kuangamia!!yaani wamenasa sijui nani wakuwanasua?.kwa sababu huo mtego wenyewe na serikali wanashiriki kuutega!

     Mungu ibariki Tanzania!!!.

     ReplyDelete

    JIANDIKISHE HAPA

    Enter your email address:

    Delivered by FeedBurner

    VITAMBULISHO VYETU