NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Sunday, April 10, 2011

KUTIMULIWA KWA AKINA MAKAMBA NA WENZAKE: CCM IMEANZA KUJISAFISHA (AKA KUJIVUA MAGAMBA)!?!?

 • Na gamba mojawapo lililovuliwa ni la Mbunge wangu! Na kama alivyosema Mjengwa, ngoja tuone CCM itafanyaje na magamba haya yaliyovuliwa ambayo mimi napenda niyaite magamba sugu! Itayafukia, itayaacha yakitapakaa au itayachoma moto kabisa na kuyateketeza? Baada ya kusukwasukwa huku na huko katika uchaguzi uliopita, ni wazi kwamba CCM imeamka na naamini kwamba hatua hii ni mwanzo (mzuri) katika kujaribu kurudisha imani yake kwa wananchi kwani mwaka 2015 si mbali sana. Ikishupalia ufisadi inaweza kujiokoa! Ngoja tuone! Kwa habari zaidi soma HAPA na HAPA
 • Habari zaidi zinapatikana kutoka gazeti la Majira na Uhuru. Majigambo ya CHADEMA kuhusu suala hili yanapatikana HAPA.

4 comments:

 1. Siasa hizo mkuu, nakumbuka swali lile vyema kabisa `siasa ni uongo wenye ukweli ndani yake jadili...'

  ReplyDelete
 2. Hivi somo lile la siasa,lilikuwa linakidhi haja ya wanafunzi kuelewa siasa?.kama ndiyo kwanini wamelifuta? na kama siyo walilobadilisha linawasaidia wanafunzi? mnewaza kunisaidia tafakari yangu na kuelimishana wapendwa!!!!

  Samahani kaka yangu Matondo kwa kuongezea vjimaswali hapa!!!!!!!

  ReplyDelete
 3. Hivi somo la Siasa lilishafutwa? Mimi wala nilikuwa sijui. Walifuta na kuweka somo gani mbadala? Civics ama?

  Mungai aliparaganya kweli mitaala yetu pamoja na kufuta michezo mashuleni.

  emu-three: ulijibuje hilo swali? Ni kweli hatuna wanasiasa wakweli? Kuna binadamu mkweli? Tujiulize tu!

  ReplyDelete
 4. Nasikia kuna somo jipya linaitwa URAIA,Kama sipo sahihi wanaojua zaidi mtueleweshe!

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU