NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Wednesday, April 13, 2011

SALA YA KUOMBEA KUSHUKA KWA BEI YA MAFUTA HAPA MAREKANI !!!

Picha hii iko HAPA
 • Galoni moja sasa inakaribia kuwa dola 4. Hii ni bei kubwa mno kwa Wamarekani ambao, japo ndiyo watumiaji wakuu wa nishati hapa duniani, pia wamezoea kuipata nishati hiyo kwa bei rahisi. Naamini huko Uingereza na kwingineko (ambako mafuta yanauzwa kwa lita) pengine bei ni kubwa zaidi.  
 • Kama imani yaweza kuhamisha milima, bila shaka yaweza hata kushusha bei ya mafuta. Tazama HAPA kuhusu pasta mmoja kule Georgia ambaye ameamua kuendesha sala ili kuombea kushuka kwa bei ya mafuta.

   2 comments:

   1. Ukilinganisha bei ya mafuta hapo kwenu na hapa Kanada, nyie bado mna nafuu. Mie huwa navuka mpaka kwenda kununua Marekani na kuokoa takribani senti 27 kwa kila lita ninayotumia.
    Hali ya nishati ni mbaya sana hasa kwa wenye magari mazito. Hapa ni kubadili mazoea. Ingawa magari ya kijapani ni aghali hapa, jipatie moja utaokoa pesa nyingi. Mjini kwangu taxi zote zinatumia Toyota.

    ReplyDelete

   JIANDIKISHE HAPA

   Enter your email address:

   Delivered by FeedBurner

   VITAMBULISHO VYETU