NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Sunday, April 3, 2011

SI WOTE WANAOKWENDA LOLIONDO NI WAGONJWA. WENGINE WANAKWENDA HUKO "OUT OF CURIOSITY" NA KUONA JINSI HIYO DAWA INAVYO"TASTE" (ANZIA DK. YA 2:20)

8 comments:

 1. Naomba kuuliza je tanzania lugha ya taifa ni ipi ? maana huyu Waziri anachanganya lugha mbili kingereza na kiswahili kwenye maelezo yako je serekali inalalisha madawa ya kienyeji ? sio baya serekali kujua kwamba madawa yanatipu ila nivizuri yakfanyia uchunguzi zaidi maana nasikia pia mti huo ni wa sumu je tukipanda kila mahali sio ndio tutakufa na pia Babu alisema kuwa dawa anatoa kwa maombi na pia nilazima watu waende loliondo. je mti ukipandwa kila mahali na ni lazima babu atoa dawa na ni loliondo tu sio mahali pengine ? je faida yake ni nin ? hii ndio maana waziri anatokea kwenye vyombo vya habari kutangaza mambo bila ya kufikiria. je vyombo ya habari tanzania vipo wapi maana nchi zilizoendelea wanahabari wantafuta watu wagonjwa na wasio na uwezo ili wapelekea kwa babu na akishapata kikombe na baadaye mgonjwa akipoa utoa maelezo yake . maana mpaka sas hivi ninasikia habari hizi kwa magazeti na watu yaani maneno ya kwa watu, ninaomba tupate maelezo kwa watu waliopoa ili na mimi niweze kuwaeleze marafiki zangu ambao sio watanzania, asante sana

  ReplyDelete
 2. Hakuna wajasiliamali ambao hawajaanza kutengeneza JUISI na cola za kikombe cha BAU ili kukidhi mahitaji ya wapendao tu TASTE ya kikombe cha BABU?

  ReplyDelete
 3. Huyu waziri anachekesha kweli. Watu wanakata wiki mbili wakiwa mbugani ili wakapate ahueni ya magonjwa yanayowasumbua yeye anakwenda huko kwa ajili ya curiosity na kuonja ladha ya hiyo dawa. Alikaa kwenye foleni kama wagonjwa wengine au kwa vile yeye ni mnene alikwenda moja kwa moja.

  Mtu ukiwa na madaraka sijui tu tunakuwaje.

  QN: Ina maana sasa matumaini na sera zetu mf. kupambana na magonjwa sugu kama kansa ni officially kwa Babu? Naona anasema watoto na wajukuu zetu wakija kuumwa kansa huu mti uwepo. Hapa ndipo tulipofikia as a society?

  ReplyDelete
 4. Msukusi huyu mgonjwa. Maana ukiangalia umri wake na umbo wake utaona ukweli. Hakuna cha taste wala nini bali kuficha maradhi. Pia kiingereza chake cha hakijaenda shule. Hajui kiswahili wala kiingereza heri angeongea kisukuma mwana wetu. Makoye ga mbiti ng'wana kangwa!

  ReplyDelete
 5. jamani toeni maoni yenye maana hujasikia kiswangilishi acheni ushamba sijaona ubaya wowote alivochanganya lugha by the way kila mtu anakosea kingereza kwani is not our mother tongue,huo mti utafiti wa kenya na india inaonesha ni dawa kwa hiyo ni vizuri kupreserv nyie vipi.na aliesema hajapata uhakika wa mgonjwa aliepona hukumsikia yule dr aliesema alishangaa kumpima mgonjwa wake kukuta hana virus wakati alikuwa akinywa arvs muwe mnafuatilia mambo not from no where unakurupuka

  ReplyDelete
 6. Pamoja na kwamba mimi siyo mtaalamu wa lugha ya mwili(body language), lakini nikimwangalia tu kwa haraka huyu Waziri wetu wa Maliasili na Utalii ninagundua kama anadanganya uma. ishara zinazonipelekea kuamini ni jinsi anavyogusa pua yake, uchezeshaji wa macho na mikono, zaidi ni jinsi anavyoshindwa kupangilia maneno kutokana na kushitukizwa na swali.
  Nikiwa Mmoja wa Wasukuma, Ndugu yangu, Mheshimiwa Ezekiel Maige ananiaibisha sana nikifikilia jinsi Ndugu John M. Masuha alivyotumwagia sifa katika kitabu chake cha Masimulizi ya Wasukuma.
  Nashindwa kuelewa ni kwa nini wanasiasa wengi nchini bado hawataki wajulikane kama wameenda kwa ''Babu'', na hata kama wakijulikana hawataki kuuambia umma ni nini kinachowasibu katika miili yao mpaka wakaenda kwa ''Babu''. wanakuwa wa kwanza kutaka wajulikane katika vyombo vya habari kama wanawakodishia usafili wapiga kura wao waende kupata kikombe. Kwa nini wasiwe kama Mzee wa kilalacha, Lyatonga Mrema ambaye aliueleza umma ukweli wa sababu iliyomfanya kwenda kwa ''Babu'' wa Loliondo.
  Swala la ugonjwa halina aibu wala siri. Inashangaza kuona watu ''mashuhuri'' mpaka wanatafuta magari yenye vioo vyeusi ili wakiwa wanajipanga kwenye foleni ya kupata kikombe watu wasiwatambue.
  Tatizo ni kuwa wanasiasa wanasutwa na uchanganyaji wa Imani katika utendaji serikalini mpaka wanashindwa kwa sasa kutoa ufafanuzi kwa wananchi kama kikombe cha ''Babu'' kina ponya au la, wakati huo huo wao kila kukicha wanapishana kwa ''Babu'' kupata kikombe na wakiulizwa wanasema eti ''OUT OF CURIOSITY''.
  Ama kweli nchi yetu bado ina safari ndefu kufikia karne ya 21.

  ReplyDelete
 7. Ng'wanaMwamapalala: Wanasiasa ni watu "wanaoona mbali" Pengine wanaogopa kujitangaza ili hapo baadaye ikija kuthibitishwa kisayansi kwamba tiba ya babu haiponyeshi (pengine ni placebo effect tu!) basi wasije kuaibika kwa kuipigia debe. Ndiyo maana wanaenda huko kwa siri na hata hao wanaokwenda huko, hawasemi kilichowapeleka na kama wamepona maradhi yaliyokuwa yakiwasumbua. Kama wanasiasa wote waliokwenda huko wangesema kilichokuwa kimewapeleka na kama wamepona basi huu ungekuwa uthibitisho tosha wa tiba hii kwa umma.

  Ndiyo maana kuna watu wanaodai kwamba pengine wanasiasa hawa wanafanya hivi ili kuendelea kuuchochoea moto huu wa Loliondo ambao umegubika vyombo vyote vya habari kiasi kwamba masuala muhimu na kero zingine zinazowakabili wananchi hazipewi uzito tena. Kila kitu sasa ni Loliondo utafikiri kwamba matatizo yetu yote tuliyonayo utatuzi wake ni Loliondo na vikombe vingine vinavyozuka kila kona.

  Siamini kwamba Mh. Waziri eti alikunywa hii dawa kwa "out of curiosity" tu na kuonja ladha yake. Hata kama asingetaka kusema kilichompeleka huko, angegusia angalau anavyojisikia sasa baada ya kunywa dawa hiyo. Sasa hapa anajitahidi kweli kudanganya tena bila sababu yo yote ya msingi. Wanasiasa!

  Sifa tulizomwagiwa na Ndugu John M. Masuha nadhani anazo. Sijamsikia akihusika katika kasheshe hizi tulizozizoea.

  ReplyDelete
 8. Ndugu yangu Matondo, Kama wanasiasa wetu ni waona mbali, hilo nakubaliana nawe.
  Na kama wanafanya hivi ili kuendelea kuchochea moto wa Loliondo ili maswala muhimu yasahaulike katika jamii, basi nitaamini serikali ya Kikwete inaongoza katika uwajibikaji wa pamoja(collective responsibility), kitu ambacho sikiamini hata kidogo.
  Ya kwetu ni macho, tusubili hii kasheshe mwisho wake.

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU