NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Friday, May 6, 2011

Al-Qaeda Wakiri Osama Ameuawa. Watoa Mikwara Kibao Dhidi ya Marekani

 • Al-Qaeda hatimaye wamekiri kwamba kiongozi wao "mpendwa", Osama Bin Laden ameuawa. Al-Qaeda pia imechimba mkwara kwa kusema kwamba furaha ya Wamarekani itageuka na kuwa huzuni muda si mrefu ujao; na kwamba kifo cha Osama kichukuliwe kama kichochezi tu na kwamba Al-Qaeda kamwe haitakufa. Sijui kama taarifa hizi zitasaidia kuwanyamazisha wale wanaodai kwamba Osama hajauawa na kwamba hizi ni njama za Obama kujiongezea umaarufu kuelekea uchaguzi mkuu ujao. Habari kamili kuhusu habari hii zinapatikana HAPA

4 comments:

 1. Kama wamekiri basi wanakubaliana na ile namna (VERSION) iliotolewa na Wamerikani kuhusu kifo na mazishi.

  Suali: Je, wanajihadi wataendelea kumla samaki?

  ReplyDelete
 2. Hawana lolote zaidi ya kuanza kufa taratibu. Kwa wanaokumbuka kundi la kigaidi la Red Brigade lililomteka na kumuua waziri mkuu wa Italy Aldo Moro watakubaliana nami uwa sasa al Qaeda ndiyo kwishinei. Rest in Hell al Qaeda.

  ReplyDelete
 3. Kila nafsi itaonja umauti...yeye siku yake imefika hivyo, hakuna cha ajabu, kwani yeye sio Mungu kuwa hatakufa. Cha muhimu ni kutafuta njia ya kuishi kwa amani, na sio kuwekeana visasi, najiuliza `tunauana ili iweje'...na je tunapoua wenzetuu ina maana sisi hatutakufa?

  ReplyDelete
 4. Goodman - japo wamekiri lakini bado kuna watu wanaodai kwamba hizi ni blah blah tu za Wamarekani na kwamba jamaa bado yupo hai; na au alishakufa zamani kutokana na ugonjwa wa figo. Inavyoonekana bado wataendelea na falsafa ya mwanzilishi wao ya kutumia vitisho ili kuleta mabadiliko wanayoyataka ingawa umma katika nchi za Kiarabu umewaonyesha kwamba unaweza kujiletea mabadiliko kwa njia za amani ukitaka.

  Mwalimu Mhango - Ni pigo kubwa hili kwani nyaraka zilizokwapuliwa na Wamarekani zinaonyesha kwamba jamaa alikuwa ana mipango kibao ya kushambulia mifumo ya treni hapa Marekani na kwingineko. Itawachukua muda kuweza kujipanga vizuri.

  Emu-Three: "Tunauana ili iweje?" Swali zuri. Pengine ni kwa sababu sisi nasi ni wanyama tu na tuna hulka ile ile ya simba kumla pundamilia na hata kumyang'anya windo simba mwenzake japo awe amelihangaikia vipi. Ukiangalia hata vita vingi tulivyopigana ni katika kugombea "mawindo" tu na si vinginevyo. Binadamu!

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU